Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Ufunua wa Yohana 17-19

Adhabu Ya Babiloni

17 Mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na yale mabakuli saba akaja akaniambia, “Njoo, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aliyeketi juu ya maji mengi. Wafalme wa dunia wamezini naye, na watu waishio duniani walilewa divai yake ya uzinzi.” Kisha nikiwa katika Roho malaika akanipeleka nyikani, nikamwona mwanamke mmoja ameketi juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya kumtukana Mungu mwili mzima. Mnyama huyo alikuwa na vichwa saba na pembe kumi. Huyo mwanamke alikuwa amevaa mavazi ya rangi ya zambarau na nyekundu na kujipamba kwa dhahabu, vito vya thamani na lulu. Mkononi mwake alishika kikombe cha dhahabu kilichojaa mambo ya kuchukiza na uchafu wa uasherati wake. Na kwenye kipaji cha uso wake yaliandikwa maneno yenye maana iliyofichika: “Babiloni Mkuu, Mama wa Makahaba na wa Machukizo yote ya Duniani.” Nikaona kuwa huyo mwanamke alikuwa amelewa damu ya watu wa Mungu na damu ya watu waliouawa kwa kumshuhudia Yesu. Nilipomwona, nilistaajabu sana. Lakini yule malaika akaniambia, “Kwa nini unastaajabu? Nitakufunulia siri ya huyo mwanamke na huyo mnyama aliyembeba, mwenye vichwa saba na pembe kumi. Huyo mnyama uliyemwona alikuwapo lakini sasa hayupo , naye atapanda kutoka katika shimo la kuzimu kwenda maangamizoni. Na watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu ulimwengu kuumbwa, watashangaa kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwapo, na hayupo, na kwamba atakuwapo.

Jambo hili linahitaji hekima na maarifa. Vile vichwa saba ni milima saba ambapo huyo mwanamke ameketi. 10 Pia hivyo vichwa saba ni wafalme saba ambao kati yao watano wamekwisha kuanguka, mmoja yupo na mmoja hajaja bado, naye akija, atalazimika kukaa kwa muda mfupi tu. 11 Na huyo mnyama aliyekuwapo ambaye hayupo, yeye ni wa nane, lakini ni wa kundi la wale saba naye pia ataan gamizwa.

12 Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawaja tawazwa bado, lakini watatawazwa kwa muda wa saa moja tu pamoja na yule mnyama. 13 Hawa wana nia moja nao watampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao. 14 Watampiga vita Mwana-Kondoo na Mwa na-Kondoo atawashinda kwa kuwa yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme, na wale walio pamoja naye wanaitwa wateule na waami nifu.”

15 Kisha akaniambia, “Yale maji uliyoyaona alipokuwa amekaa yule kahaba, ni watu na umati wa watu na mataifa na lugha. 16 Na zile pembe kumi ulizoziona, pamoja na huyo mnyama watamchukia huyo kahaba; watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake na kumteketeza kabisa kwa moto. 17 Maana Mungu amefanya mioyo yao kutimiza mapenzi yake, kwa kuwafanya wawe na nia moja ya kumpa mamlaka yao ya kifalme huyo mnyama, mpaka maneno ya Mungu yataka potimizwa. 18 Na yule mwanamke uliyemwona ni ule mji mkuu wenye mamlaka juu ya wafalme wa dunia.”

Kuanguka Kwa Babiloni

18 Baada ya haya nikaona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni akiwa na uwezo mkuu. Ulimwengu wote uliangazwa kwa utu kufu wake. Naye akasema kwa sauti kuu, “Ameanguka, Babiloni mkuu, ameanguka! Amekuwa maskani ya mashetani, makazi ya kila roho mchafu, kiota cha kila ndege mchafu na wa kuchukiza. Maana mataifa yote yamekunywa divai ya uasherati wake, na wafalme wa duniani wamezini naye; na wafanya biashara wa duniani wametaji rika kutokana na tamaa yake mbaya isiyo na mipaka.”

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, tokeni kwake msije mkashiriki dhambi zake mkapati kana na maafa yatakayompata; maana dhambi zake zimelundikana hadi mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. Mtendee kama yeye alivyotenda, umlipe mara mbili zaidi kwa matendo yake; mchanganyie kinywaji mara mbili zaidi ya kile kinywaji alicho changanya. Kama yeye alivyojitukuza kwa uasherati wake, mpe mateso na maombolezo kwa kipimo hicho hicho. Kwa kuwa kama ase mavyo moyoni mwake, ‘Mimi naketi kama malkia, si mjane wala sita pata msiba kamwe.’ Hivyo ndivyo maafa yatakavyomjia kwa siku moja; tauni na msiba na njaa, naye atachomwa kwa moto; kwa maana amhukumuye ni Bwana Mungu mwenye uweza.

Na wafalme wa mataifa waliozini naye na kushiriki tamaa zake watalia na kuomboleza watakapoona moshi wa kuungua kwake. 10 Watasimama mbali kwa hofu ya mateso yake na kusema, “Ole wako! Ole wako, mji mkuu, Babiloni, mji wenye nguvu! Hukumu yako imekuja katika saa moja!” 11 Na wafanya biashara wa duniani watalia na kuomboleza kwa maana hakuna anunuaye bidhaa zao tena. 12 Bidhaa za dhahabu, fedha, vito vya thamani na lulu, kitani safi, nguo za rangi ya zambarao, hariri, na nguo nyekundu, aina zote za mti wa udi, vifaa vya meno ya tembo, vifaa vyote vya mbao ya thamani, shaba, chuma na marumaru, 13 mdalasini, hiliki, uvumba, marhamu, ubani, divai, mafuta ya mzeituni, unga mzuri, ngano, ng’ombe, kondoo, farasi na magari, na watumwa, pia na roho za wanadamu. 14 Watasema, ‘Yale matunda ambayo roho yako iliy atamani yametoweka, na utajiri wako wote na ufahari vimetoweka, wala hutavipata kamwe!’

15 Wale wafanya biashara wa bidhaa hizo waliopata utajiri wao kwake watasimama mbali kabisa kwa kuogopa mateso yake, nao watalia na kuomboleza kwa nguvu wakisema, 16 ‘Ole wako! Ole wako! mji mkuu, ulikuwa umevikwa mavazi ya kitani safi, rangi ya zambarau na nyekundu, uking’aa kwa dhahabu na vito vya thamani na lulu! 17 Katika muda wa saa moja utajiri wote huu umeharibiwa!’ Manahodha wote, mabaharia na wote wasafirio baharini na wote wafanyao kazi melini watasimama mbali kabisa.

18 Watakapoona moshi wake wakati mji ukiteketezwa watalia wakisema, ‘Kuna mji gani ambao umepata kuwa kama mji huu mkuu?’ 19 Nao watajimwagia vumbi vichwani na kulia na kuomboleza wakisema, ‘Ole wako, Ole wako mji mkuu, mji ambapo wote wenye meli baharini walitajirika kwa mali yake! Maana katika saa moja tu umeteketezwa. 20 Fura hini juu yake, enyi mbingu, watakatifu na mitume na manabii; Kwa kuwa Mungu ameuhukumu kwa ajili yenu!”’

21 Kisha malaika mkuu akachukua jiwe kama jiwe kubwa la kusagia akalitupa baharini akisema, ‘ ‘Hivyo ndivyo mji mkuu wa Babiloni utakavyotupwa chini kwa nguvu wala hautaonekana kamwe. 22 Wala sauti za wapiga vinanda, na wapiga zomari, wapiga fil imbi na sauti ya wapiga tarumbeta hazitasikika kwako kamwe. Hata patikana kwako fundi mwenye ujuzi wo wote; wala sauti ya jiwe la kusaga haitasikika kamwe. 23 Na nuru ya taa haitaangaza ndani yako tena; Wala sauti ya bwana harusi na bibi harusi haitasikiwa ndani yako kamwe. Maana wafanya biashara wako walikuwa watu maarufu wa duniani, na mataifa yote yalidanganyika kwa uchawi wako. 24 Na ndani yake ilikutwa damu ya manabii na watakatifu na watu wote waliouawa duniani.”

Wimbo Wa Ushindi

19 Baada ya haya nikasikia sauti kama sauti kuu ya umati mkubwa wa watu mbinguni ikisema kwa nguvu, “Haleluya! Wokovu na utukufu na uweza ni wa Mungu wetu. Maana hukumu zake ni za kweli na haki, amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeuharibu ulimwengu kwa uasherati wake. Mungu amelipiza kisasi kwa ajili ya damu ya watumishi wake.” Kwa mara nyingine wakasema kwa nguvu, “Hale luya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” Wale wazee ishirini na wanne pamoja na wale viumbe wanne wenye uhai walianguka kifudifudi wakamwabudu Mungu aliyekuwa ameketi katika kiti cha enzi. Wakasema kwa sauti kuu, “Amina! Hale luya!”

Na sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, “Msi funi Mungu wetu ninyi watumishi wake wote, nyote mnaomcha, wadogo kwa wakubwa.”

Kisha nikasikia sauti kama sauti ya umati mkubwa wa watu, kama sauti ya maporomoko ya maji mengi na kama ngurumo kuu ya radi kubwa ikisema, “Haleluya! Kwa maana Bwana Mungu wetu Mwe nyezi anatawala. Tufurahi na kushangilia na kumtukuza maana harusi ya Mwana-Kondoo imefika na bibi harusi wake amejitayar isha. Alipewa kitani safi nyeupe inayong’aa ili avae.” Hiyo kitani safi ni matendo ya haki ya watakatifu.

Na malaika akaniambia, “Andika haya: ‘Wamebarikiwa wal ioalikwa kwenye karamu ya harusi ya Mwana-Kondoo.”’ Na akaniambia, “Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”

10 Ndipo nikaanguka kifudifudi miguuni pake kumwabudu, lakini yeye akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi pia ni mtumishi pamoja na wewe na ndugu zako wanaoshikilia ushuhuda wao kwa Yesu. Mwabudu Mungu! Maana ushuhuda wa Yesu ndio kiini cha unabii.”

Aliyepanda Farasi Mweupe

11 Kisha nikaona mbingu imefunguka na mbele yangu nikaona farasi mweupe! Aliyeketi juu ya huyo farasi aliitwa Mwaminifu na Kweli, naye huhukumu na kupigana vita kwa ajili ya haki. 12 Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna vilemba vingi; na ameandikwa jina ambalo hakuna mwingine anayeli jua isipokuwa yeye mwenyewe. 13 Amevaa vazi lililochovywa katika damu na jina analoitwa ni “Neno la Mungu”. 14 Na majeshi ya mbinguni yaliyovaa kitani safi nyeupe walimfuata wakiwa wamepanda farasi weupe.

15 Kinywani mwake mlitoka upanga mkali wa kuyapiga mataifa. Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kukamua divai katika mtambo wa kutengenezea divai ya ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. 16 Kwenye vazi lake na paja lake liliandikwa jina hili: “Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”

Bwana wa mabwana.”

17 Kisha nikamwona malaika amesimama ndani ya jua, akaita ndege wote warukao angani kwa sauti kuu, “Njooni, kusanyikeni kwa ajili ya karamu kubwa ya Mungu. 18 Njooni mle nyama ya wafalme na nyama ya majemadari, na nyama ya watu hodari; nyama ya farasi na wapanda farasi, nyama ya wanadamu wote, wakubwa kwa wadogo, watumwa na watu huru.”

19 Na nikamwona yule mnyama na wafalme wa duniani pamoja na majeshi yao wakikusanyika kumpiga vita yeye aketiye juu ya yule farasi pamoja na jeshi lake. 20 Yule mnyama akatekwa pamoja na yule nabii wa uongo, aliyefanya ishara za uongo, kwa niaba yake, akawadanganya wale waliopokea alama ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. 21 Waliobakia waliuawa kwa upanga wa yule aketiye juu ya farasi, kwa ule upanga utokao kinywani mwake; na ndege wote wakala nyama yao mpaka wakakinai.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica