Beginning
1 Kutoka kwa Mzee. Kwa mama mteule pamoja na watoto wake niwapendao katika kweli. Wala si mimi tu niwapendaye bali wote wanaoifahamu kweli; 2 kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itakuwa nasi hadi milele.
3 Neema, huruma, na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wake zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
Kweli Na Upendo
4 Nimefurahi sana kuona kwamba baadhi ya watoto wako wanadumu katika kweli, kama Baba alivyotuamuru. 5 Na sasa, mama mpendwa, sikuandikii amri mpya, bali ile ile ambayo tumekuwa nayo kutoka mwanzo: kwamba tupendane. 6 Na upendo ni huu: kwamba tuishi kwa kuzifuata amri za Mungu. Na kama mlivyosikia tangu mwanzo, amri yake ni kwamba muishi maisha ya upendo.
7 Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, watu wasiokiri ya kwamba Kristo alikuja kama mwanadamu. Mtu kama huyo ni mdanganyifu na mpinga-Kristo. 8 Jihadharini msije mkapoteza yale mliyoyafanyia kazi, bali mpewe thawabu kamili.
9 Mtu ye yote anayevuka mpaka wa mafundisho ya Kristo, na kuyaacha, huyo hana Mungu. Na mtu anayedumu katika mafundisho ya Kristo, huyo anaye Baba na Mwana pia. 10 Mtu ye yote akija kwenu bila kuwaletea mafundisho haya, msimkaribishe nyumbani kwenu, wala msimsalimu. 11 Kwa maana mtu anayemsalimu anashiriki kazi zake za uovu.
12 Ninayo mengi ya kuwaandikia, lakini sipendi kutumia kara tasi na wino. Badala yake ninatarajia kuwatembelea na kuongea nanyi uso kwa uso, ili furaha yetu ikamilike.
1 Kutoka Kwa Mzee. Kwa mpendwa wangu Gayo, nimpendaye katika kweli. 2 Mpendwa, ninakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kwamba uwe na afya njema ya mwili; kwa maana najua roho yako ni salama. 3 Nilifurahi sana walipokuja ndugu kadhaa wakashuhudia jinsi ulivyo mwaminifu katika kweli na jinsi unavyoendelea kuishi katika kweli. 4 Hakuna kitu kinachonifurahisha zaidi kuliko kusi kia kwamba watoto wangu wanafuata kweli.
Uaminifu Wa Gayo
5 Mpendwa, wewe umekuwa mwaminifu kwa yote unayowatendea hao ndugu, ingawaje wao ni wageni kwako. 6 Wamelishuhudia kanisa kuhusu upendo wako. Tafadhali wasaidie waendelee na safari yao kwa namna itakayompendeza Mungu. 7 Kwa maana wanasafiri kwa ajili ya Bwana na wamekataa kupokea cho chote kutoka kwa watu wasiomjua Mungu . 8 Kwa hiyo tunawajibu wa kuwasaidia watu wa namna hiyo ili tuwe watenda kazi pamoja nao kwa ajili ya kweli.
Diotrefe Na Demetrio
9 Niliandika barua kwa hilo kanisa; lakini Diotrefe apendaye kujiweka mbele kama kiongozi wao, hatambui mamlaka yangu. 10 Kwa hiyo nitakapokuja nitaeleza mambo anayofanya; na kuhusu maneno maovu anayosema juu yangu. Wala hatosheki na hayo bali anakataa kuwakaribisha ndugu. Pia anawazuia wale ambao wanataka kuwakarib isha na anawafukuza kutoka katika kanisa. 11 Mpendwa, usiige ubaya bali iga wema. Atendaye mema ni wa Mungu. Atendaye uovu hajapata kumwona Mungu. 12 Demetrio anashuhudiwa wema na kila mtu na hata kweli yenyewe inamshuhudia. Mimi pia ninamshuhudia wema, na wewe unajua kwamba ushuhuda wangu ni wa kweli.
Salamu Za Mwisho
13 Ninayo mengi ya kukuandikia, lakini afadhali nisitumie kalamu na wino. 14 Natarajia kukuona karibuni na tutaongea uso kwa uso.
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo. Nawaandikia wale walioitwa na kupendwa na Mungu Baba na kulindwa na Yesu Kristo. 2 Ninawatakieni rehema, amani na upendo tele.
Hukumu Ya Watu Wasiomcha Mungu
3 Wapendwa, ingawa nilikuwa na hamu kubwa kuwaandikieni kuhusu wokovu wetu, nimeona ni muhimu niwaandikieni nikiwasihi mwendelee kuipigania kwa nguvu imani ambayo Mungu amewakabidhi watakatifu mara moja tu kwa wakati wote. 4 Hii ni kwa sababu watu wasiomcha Mungu ambao tangu zamani wamekwisha kuandikiwa hukumu hii, wamejiingiza miongoni mwenu kwa siri. Hawa ni watu ambao wanapotosha neema ya Mungu wetu na kuitumia kama kisingizio cha kutenda maovu. Wao wanamkana Yesu Kristo ambaye pekee ndiye Mkuu na Bwana wetu.
5 Sasa nataka kuwakumbusha jambo ambalo tayari mnalijua: kwamba, Bwana aliwaokoa watu wake kutoka Misri, lakini baadaye akawaangamiza wale ambao hawakuamini. 6 Na malaika ambao hawaku tunza madaraka yao wakaacha maskani yao halisi; hao amewafungia gizani kwa minyororo ya milele hadi wahukumiwe katika siku ile kuu. 7 Vivyo hivyo watu wa Sodoma na Gomora na miji ya kando kando yake ambao hali kadhalika walifanya uasherati na kujifurah isha katika matendo yaliyo kinyume cha maumbile, waliadhibiwa kwa moto wa milele kama fundisho kwa watu wote.
8 Ndivyo walivyo hawa watu. Ndoto zao huwaongoza wachafue miili yao, wasitii mamlaka; na watukane viumbe watakatifu walioko mbinguni. 9 Lakini hata Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na shetani kuhusu mwili wa Musa, hakuthubutu kutamka hukumu juu ya shetani, bali alisema, “Bwana akukemee!” 10 Lakini hawa watu hushutumu cho chote wasichokielewa; na yale mambo wanayotambua kwa asili, kama wanyama ambao hawawezi kujizuia kwa kutumia fikira, hayo ndio yanayowaangamiza. 11 Ole wao! Kwa maana watu hao wamefuata mfano wa Kaini, na kama Balaamu wako tayari kufanya lo lote kwa ajili ya fedha; na kama Kora wamejiangamiza wenyewe kwa kumwasi Mungu.
12 Watu hawa ni madoa katika karamu zenu za ushirika. Wanak ula nanyi bila kuwa na kiasi, wakicheka na kujishibisha na kunywa bila kujali wengine. Wao ni kama mawingu yanayochukuliwa na upepo huku na huku pasipo kuleta mvua; ni kama miti ya kiangazi iliy opukutika bila kuwa na matunda, ambayo imekufa kabisa na kung’olewa pamoja na mizizi yake. 13 Matendo yao ya aibu ni dha hiri kama vile mapovu ya mawimbi ya bahari. Wao ni kama nyota zinazotangatanga, na mahali pao ni katika lile giza kuu ambalo Mungu amewawekea milele. 14 Henoki, ambaye alikuwa wa kizazi cha saba baada ya Adamu, alitoa unabii kuhusu watu hawa akasema, “Sikilizeni! Nilimwona Bwana akija na watakatifu wake maelfu kwa maelfu 15 kutoa hukumu kwa wote na kuwaadhibu wasiomcha Mungu, kwa ajili ya matendo yao maovu waliyoyatenda na kwa ajili ya maneno makali ambayo hao waovu wasiomcha Mungu walisema juu yake.”
16 Watu hawa ni wanung’unikaji, wakaidi, wenye kufuata tamaa zao, wenye majivuno, wenye kujigamba na ambao huwasifu watu wen gine ili mambo yao yafanikiwe.
Maonyo Na Maagizo
17 Lakini ninyi wapendwa, kumbukeni yale mliyoambiwa na mitume wa Bwana wetu Yesu Kristo kwamba yatatokea. 18 Waliwaam bieni kwamba, “Katika siku za mwisho, watatokea watu watakaowad hihaki , watu wafuatao tamaa zao mbaya.” 19 Watu hawa ndio wanaosababisha mafarakano, watu wafuatao tamaa za dunia, wasio na Roho wa Mungu. 20 Lakini ninyi wapendwa, jengeni maisha yenu juu ya imani yenu takatifu; ombeni katika nguvu na uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Jitunzeni katika upendo wa Mungu; ngojeeni rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo itakayowafikisha kwenye uzima wa milele. 22 Wavuteni wale wenye mashaka. 23 Okoeni wengine kwa kuwany akua kutoka katika moto; wengine wahurumieni, lakini mwogope, mkichukia hata mavazi yao yaliyochafuliwa kwa tamaa zao za dhambi.
24 Basi, utukufu ni wake yeye awezaye kuwalinda msianguke na kuwafikisheni bila hatia mbele ya utukufu wake mkiwa na furaha.
Copyright © 1989 by Biblica