Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
1 Wathesalonike 1-5

Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wath esalonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. Tuna watakieni neema na amani.

Shukrani Kwa Imani Ya Wathesalonike

Tunamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu wote na kuwaom bea pasipo kukoma. Tunakumbuka daima mbele za Mungu Baba yetu, kazi yenu inayotokana na imani, juhudi yenu kubwa katika upendo, na uvumilivu wenu unaotokana na tumaini mlilonalo kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Ndugu zetu mnaopendwa na Mungu, tunafahamu kwamba Mungu amewachagua kwa maana Injili yetu haikuwajia kwa maneno matupu bali ilidhihirishwa kwa nguvu na kwa Roho Mtakatifu, mkawa na uhakika kamili. Ninyi mnajua jinsi tulivyoishi pamoja nanyi kwa faida yenu. Nanyi mkatuiga sisi, mkamuiga na Bwana; kwa maana mlilipokea neno kwa furaha mliyopewa na Roho Mtakatifu ingawa mlipata mateso makali. Kwa hiyo mkawa kielelezo kwa waamini wote wa Makedonia na Akaya.

Maana neno la Mungu limeenea kutoka kwenu, sio mpaka Make donia na Akaya tu, bali imani yenu kwa Mungu imejulika na mahali pote. Kwa hiyo hatuhitaji kusema lo lote kuhusu imani yenu; kwa maana wao wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea. Wanasimulia jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha ibada za sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli; 10 na kumngoja Mwanae kutoka mbin guni, ambaye alimfufua kutoka kwa wafu, yaani Yesu. Yeye anatu komboa kutoka katika ghadhabu ijayo.

Huduma Ya Paulo Huko Thesalonike

Wapendwa, ninyi wenyewe mnajua kwamba tulipokuja kwenu haikuwa bure. Kama mjuavyo tulikuwa tumeteswa na kutukanwa huko Filipi, lakini hata hivyo, kwa msaada wa Mungu, tulikuwa na uja siri wa kuwaambia Habari Njema ya Mungu pamoja na kwamba uliku wapo upinzani mkali. Ujumbe wetu kwenu hautokani na kutokujua au nia mbaya au udanganyifu. Kinyume chake, tunahubiri kama watu tuliopata kibali cha Mungu tukakabidhiwa Habari Njema. Nia yetu si kuwapendeza wanadamu bali kumpendeza Mungu anayejua mawazo ya mioyo yetu. Mnafahamu kuwa hatukutumia maneno matamu ya kujipendekeza kwenu, wala hatukutumia hila kuficha tamaa ya kujipatia fedha, kwa maana Mungu ni shahidi yetu. Hatukutafuta kupata sifa kutoka kwa mwanadamu ye yote, kwenu au kwa mtu mwin gine.

Kama mitume wa Kristo tungaliweza kudai heshima kutoka kwenu, lakini tulikuwa wapole kwenu kama mama anayetunza watoto wake wadogo. Tuliwapenda sana, kiasi kwamba tulifurahi kushiri kiana nanyi, si Habari Njema ya Mungu tu, bali hata maisha yetu, kwa maana tuliwathamini mno. Ndugu zetu, bila shaka mnakumbuka juhudi yetu na kutaabika kwetu. Tulifanya kazi usiku na mchana kusudi tusiwe mzigo kwa mtu ye yote wakati tunawahubiria Habari Njema ya Mungu. 10 Ninyi ni mashahidi na Mungu pia ni shahidi yetu kwamba tulikuwa watakatifu, wenye haki na wasio na lawama kati yenu mlioamini. 11 Maana mnajua jinsi tulivyowatendea kama baba awa tendeavyo watoto wake: 12 tuliwatia moyo, tuliwafariji na kuwa himiza muishi maisha yampendezayo Mungu, ambaye anawaita mshiriki ufalme wake na utukufu.

13 Nasi tunamshukuru Mungu bila kukoma pia kwa sababu mlipo lipokea neno la Mungu mlilosikia kutoka kwetu, hamkulipokea kama neno la wanadamu. Bali mlilipokea kama lilivyo hasa, yaani, neno la Mungu, ambalo linafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. 14 Kwa maana ninyi ndugu zetu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu ndani ya Kristo Yesu yaliyoko Yudea. Mliteswa na watu wenu wenyewe kama vile makanisa hayo yalivyoteswa na Wayahudi. 15 Wao walimwua Bwana Yesu na manabii, wakatufukuza na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu na tena ni adui wa kila mtu kwa kuwa 16 wanajaribu kutuzuia tusiwahubirie watu wa mataifa mengine ujumbe ambao utawaokoa. Kwa njia hii wanazidi kujilundikia dhambi zao. Lakini hatimaye ghadhabu ya Mungu imewafikia.

Paulo Atamani Kuwaona Wathesalonike

17 Lakini ndugu zetu, tulipotenganishwa nanyi kwa muda, ingawa kutengana huko kulikuwa kwa mwili tu si kwa moyo, tulizidi kwa hamu kubwa kufanya kila jitihada tuonane uso kwa uso. 18 Maana tulitaka kuja huko, hasa mimi Paulo, nilijaribu zaidi ya mara moja, lakini shetani akatuzuia. 19 Kwa maana ni nini tumaini letu, furaha yetu au taji yetu ya utukufu mbele za Bwana Yesu Kristo atakapokuja? Si ninyi? 20 Hakika ninyi ndio utukufu wetu na furaha yetu.

Timotheo Atumwa Kwenda Thesalonike

Hatimaye tuliposhindwa kuvumilia zaidi, tuliona afadhali tubaki Athene peke yetu. Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika kuieneza Habari Njema ya Kristo, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo ili asije mtu akababaishwa na mateso haya. Kama mjuavyo, tumepangiwa mateso. Hata tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa, na kama mjuavyo ndivyo ilivyokuwa. Ndio maana niliposhindwa kuvumilia nilituma mtu ili nifahamu msimamo wenu katika imani. Niliogopa kuwa pengine yule mjaribu shetani alikuwa amewajaribu na kwamba pengine juhudi yetu kwenu ingekuwa ni bure.

Taarifa Ya Timotheo

Lakini sasa Timotheo amekwisha rejea kutoka kwenu na ameleta taarifa nzuri kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuam bia kwamba mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna hamu siku zote kutuona kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaona. Kwa sababu hiyo ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa ajili yenu, kutokana na imani yenu. Maana sasa hakika tunaishi kwa kuwa ninyi mmesimama imara katika Bwana. Tutawezaje kumshu kuru Mungu kiasi cha kutosha kwa ajili yenu, kutokana na furaha tuliyo nayo mbele za Mungu wetu kwa sababu yenu? 10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tuwezeshwe kuwaona tena na kuwapa tieni kile ambacho bado kinapungua katika imani yenu.

11 Tunamwomba Mungu, Baba yetu mwenyewe na Bwana wetu Yesu atutayarishie njia ya kuja kwenu. 12 Bwana na awawezeshe ninyi kupendana zaidi na zaidi na kuwapenda watu wote kama sisi tunav yowapenda ninyi. 13 Tunamwomba awaimarisheni mioyo ili msiwe na lawama bali muwe watakatifu mbele za Mungu Baba yetu, wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na watakatifu wake wote.

Maisha Yanayompendeza Mungu

Hatimaye, ndugu wapendwa, tuliwaelekeza namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli ndivyo mnavyoishi. Sasa tunawaombeni na kuwasihi katika jina la Bwana Yesu, mwendelee kufanya hivyo zaidi na zaidi. Mnafahamu maelekezo tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Yesu.

Mungu anapenda ninyi muwe watakatifu, mjiepushe na maisha ya zinaa; na kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuishi na mke wake mwenyewe kwa njia ya utakatifu na heshima; si kwa kutawaliwa na tamaa mbaya kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Katika jambo hili mtu asije akamkosea au kumdanganya ndugu yake. Kama tulivy okwisha kuwaambia na kuwaonya, Bwana atawaadhibu watu watendao dhambi zote za aina hii. Kwa maana Mungu hakutuita tutawaliwe na mawazo machafu, bali tuishi maisha ya utakatifu. Kwa hiyo mtu ye yote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.

Hatuna haja ya kuwaandikia kuhusu upendo kati ya ndugu, kwa maana ninyi wenyewe mmekwisha kufundishwa na Mungu mpendane ninyi kwa ninyi 10 na kwa kweli mnawapenda ndugu wote wa Makedonia yote. Hata hivyo, ndugu zetu, tunawasihi mwendelee kuwapenda zaidi sana. 11 Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akishughulikia mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaambia. 12 Kwa njia hii maisha yenu ya kila siku yatawaletea sifa kutoka kwa watu wasioamini na wala hamtahi taji kuwategemea watu wengine.

Kufufuliwa Kwa Wafu Na Kuja Kwa Bwana

13 Ndugu wapendwa, hatupendi mkose kujua kuhusu wale wanaokufa, au mhuzunike kama watu wasiokuwa na tumaini. 14 Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, kwa hiyo tunaamini kwamba Mungu atawainua wale waliokufa pamoja na Kristo wakiwa ndani yake. 15 Kama alivyosema Bwana mwenyewe, tunawaambieni kuwa sisi ambao tuko hai bado, tutakaokuwa hai mpaka Bwana arudi, kwa hakika hatutawatangulia wale waliokwisha kufa.

16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka toka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu pamoja na sauti ya malaika mkuu na sauti ya tarumbeta ya Mungu; na wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuka kwanza. 17 Kisha sisi tulio hai bado, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu tukutane na Bwana angani. Na hivyo tutakuwa na Bwana milele. 18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.

Bwana Atakuja Ghafla

Basi, ndugu wapendwa, hatuna haja ya kuwaandikieni kuhusu nyakati na tarehe atakayokuja Bwana, kwa maana mnajua wazi kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Wakati watu bado wanasema, “Kuna amani na usalama’

Bali ninyi, ndugu wapendwa, hamko gizani kuhusu mambo haya hata siku ile iwashtue kama mwizi. Ninyi nyote ni wana wa nuru, wana wa mchana. Sisi sio watu wa giza au wa usiku. Kwa hiyo basi, tusiwe kama baadhi ya watu wengine, waliolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. Maana wale wanaolala hulala usiku, na wale wanaolewa hulewa usiku. Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukivaa imani na upendo kama kinga ya kifuani na kuvaa tumaini letu la wokovu kama kofia ya chuma. Maana Mungu hakutuchagua ili tupate ghadhabu yake bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. 10 Yeye alitufia ili kama tuko hai au hata kama tumekufa, tuishi pamoja naye. 11 Kwa hiyo farijianeni na kujengana kama mnavyofanya sasa.

Maagizo Ya Mwisho Na Salamu

12 Sasa tunawaomba, ndugu wapendwa, muwaheshimu wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu; ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya. 13 Wapeni heshima kubwa na kuwapenda kwa ajili ya kazi yao. Ishini kwa amani kati yenu. 14 Na tunawasihi, ndugu wapendwa, muwaonye wale walio wavivu, watieni moyo walio waoga, wasaidieni walio dhaifu na muwe na subira na kila mtu. 15 Hakikisheni kuwa mtu hamlipi mwenzake ovu kwa ovu bali daima jitahidini kutendeana wema ninyi kwa ninyi na watu wengine wote.

16 Furahini wakati wote, 17 ombeni pasipo kukoma, 18 shu kuruni katika kila hali; kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu mkiwa ndani ya Kristo Yesu. 19 Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu; 20 msidharau unabii. 21 Pimeni kila kitu. Yash ikeni kwa makini yaliyo mema. 22 Epukeni uovu wa kila namna.

23 Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase kabisa. Roho zenu, nafsi zenu na miili yenu na ihifadhiwe bila kuwa na lawama kwa wakati atakapokuja Bwana wetu Yesu Kristo. 24 Yeye aliyew aita ni mwaminifu naye atafanya haya.

25 Ndugu wapendwa, tuombeeni. 26 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27 Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica