Beginning
Karama Za Roho Mtakatifu
12 Sasa kuhusu karama za Roho Mtakatifu ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu. 2 Mnajua kwamba mlipokuwa hamumjui Mungu mlivutwa na kupotoshwa na sanamu bubu.
3 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kukiri, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu. 4 Basi kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni mmoja. 5 Pia kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni mmoja. 6 Kisha kuna aina tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule anayeongoza kazi zote kwa kila mtu. 7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila mtu kwa faida ya wote.
8 Maana mtu mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe apendavyo.
Mwili Mmoja, Viungo Vingi
12 Kama vile mwili ulivyo mmoja lakini una viungo vingi, na viungo vyote ingawa ni vingi vinafanya mwili mmoja, ndivyo ilivyo na Kristo. 13 Kwa maana tumebatizwa na Roho mmoja katika mwili mmoja, kama ni Wayahudi au Wagiriki, kama ni watumwa au watu huru; nasi tumepewa tunywe, huyo Roho mmoja.
14 Mwili si kiungo kimoja, bali una viungo vingi. 15 Kama mguu ungesema, “Kwa kuwa mimi si mkono basi mimi si sehemu ya mwili.” Hiyo isingefanya huo mkono usiwe sehemu ya mwili. 16 Na kama sikio lingesema, “Kwa kuwa mimi si jicho, basi mimi si sehemu ya mwili.” Hiyo isingefanya hilo sikio lisiwe sehemu ya mwili. 17 Kama mwili mzima ungelikuwa jicho, ungelisikiaje? Au kama mwili wote ungelikuwa sikio, ungelinusa namna gani? 18 Lakini kama mwili ulivyo, Mungu alipanga viungo vyote katika mwili, kimoja kimoja, kama alivyopenda. 19 Kama vyote vingekuwa kiungo kimoja mwili ungekuwa wapi? 20 Kama mwili ulivyo, kuna viungo vingi, lakini mwili ni mmoja.
21 Jicho haliwezi kuuambia mkono, “Sikuhitaji!” Na kichwa hakiwezi kuiambia miguu, “Sikuhitaji!” 22 Kinyume chake, vile viungo vya mwili ambavyo vinaonekana kuwa dhaifu ndivyo ambavyo ni vya muhimu sana. 23 Na vile viungo vya mwili ambavyo tunav iona havina heshima ndivyo tunavipa heshima ya pekee. Na vile viungo vya mwili ambavyo hatuwezi kuvionyesha, tunavitunza kwa adabu 24 ambayo vile viungo vyenye uzuri wa kuonekana havihi taji. Lakini Mungu ameviweka pamoja viungo vya mwili na akavipa heshima zaidi vile visivyokuwa na heshima, 25 ili pasiwe na mga wanyiko katika mwili, bali viungo vyote visaidiane kwa usawa. 26 Kama kiungo kimoja cha mwili kikiteseka, viungo vyote vinateseka pamoja; kama kiungo kimoja kikipewa heshima, viungo vyote vinafurahi pamoja.
27 Basi ninyi ni mwili wa Kristo, na kila mmoja wenu ni kiungo cha huo mwili. 28 Na Mungu ameteua katika kanisa, kwanza mitume, pili manabii, tatu walimu, kisha watenda miujiza, kisha waponyaji, wasaidizi, watawala, wasemaji wa lugha mbalimbali. 29 Je, wote ni mitume? Au wote ni manabii? Wote ni walimu? Wote wanafanya miujiza? 30 Je, wote wana karama ya kuponya? Wote wanasema kwa lugha ngeni? Wote wanatafsiri lugha? 31 Basi takeni kwa moyo karama zilizo bora. Nami nitawaonyesha njia iliyo bora kupita zote.
Upendo
13 Kama ningekuwa na uwezo wa kusema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kama kelele ya kengele au toazi. 2 Na kama nina uwezo wa unabii, na kuelewa siri zote na maarifa yote; na hata kama nina imani kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, mimi si kitu. 3 Kama nikitoa mali yote niliyo nayo, na kama nikitoa mwili wangu uchomwe moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
4 Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.
5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.
8 Upendo hauna mwisho. Lakini penye unabii, utakoma; zikiwepo lugha zitakoma; yakiwepo maarifa yatakwisha. 9 Kwa maana tunafa hamu kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu. 10 Lakini uka milifu utakapokuja, yale yasiyo kamili yatakwisha. 11 Nilipokuwa mtoto mdogo, nilisema kama mtoto mdogo, niliwaza kama mtoto mdogo, nilifikiri kama mtoto mdogo. Nilipokuwa mtu mzima niliacha mambo ya kitoto. 12 Kwa maana sasa tunaona sura kama ya kwenye kioo, lakini wakati huo tutaona uso kwa uso. Sasa nafahamu kwa sehemu, wakati huo nitafahamu kikamilifu, kama vile ninavyo faha mika kikamilifu.
13 Basi sasa, mambo matatu yanadumu: imani, tumaini na upendo. Lakini lililo kuu kati ya haya ni upendo.
Karama Za Unabii Na Lugha
14 Fuateni upendo na kutaka sana karama za Roho, hasa karama ya unabii. 2 Kwa maana anayesema kwa lugha, hasemi na watu bali anasema na Mungu. Hakuna mtu anayemwelewa, kwani anasema siri katika Roho. 3 Lakini anayetamka neno la Mungu anasema na watu akiwasaidia kupata nguvu, na kuwatia moyo na kuwafariji. 4 Anayesema katika lugha anajijenga mwenyewe, lakini anayetoa neno la Mungu analijenga kanisa. 5 Ningependa ninyi nyote mseme kwa lugha ngeni, lakini ningependa zaidi nyote muweze kutoa una bii kwa kuhubiri neno la Mungu. Kwa kuwa anayehubiri neno la Mungu ni mkuu kuliko anayesema kwa lugha, isipokuwa kama kuna mtu wa kutafsiri, ili kanisa zima liweze kusaidika.
6 Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha ngeni, nitapata faida gani kama sikuwaletea mafunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho? 7 Hata vyombo vya muziki visivyo na uhai kama vile filimbi au kinubi, visipotumiwa kwa mpangilio wa sauti, ni nani atakayeweza kufahamu ni wimbo gani unaimbwa? 8 Na kama baragumu ikitoa sauti isiyoeleweka, ni nani atakayej iandaa kwenda vitani? 9 Hali kadhalika na ninyi. Kama mkisema kwa lugha isiyoeleweka, watu watafahamuje mnachosema? Kwa maana mta kuwa mnasema hewani.
10 Bila shaka ziko lugha nyingi ulimwenguni, na hakuna lugha isiyo na maana. 11 Lakini ikiwa sielewi maana ya lugha inayotu mika nitakuwa mgeni kwa yule anayezungumza, naye atakuwa mgeni kwangu. 12 Hali kadhalika na ninyi. Kwa kuwa mna hamu ya kuwa na karama za Roho, wekeni bidii katika karama zinazolijenga kanisa.
13 Kwa hiyo anayesema kwa lugha aombe kupewa kipawa cha kutafsiri lugha. 14 Kwa maana nikiomba kwa lugha roho yangu inaomba, lakini akili yangu haishiriki. 15 Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho na nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia. 16 Vinginevyo, kama mkim sifu Mungu katika roho, mtu mwingine ambaye anashiriki katika mkutano wenu na ambaye haelewi atawezaje kusema, ‘Amina 17 Mnaweza kuwa mnatoa shukrani kweli, lakini huyo mtu mwingine hajengeki. 18 Namshukuru Mungu kwamba mimi ninasema kwa lugha kuliko ninyi nyote. 19 Lakini hata hivyo, nikiwa kanisani, ni afadhali niseme maneno matano ya kueleweka ili niwafundishe wengine kuliko kusema maneno elfu kumi kwa lugha.
20 Ndugu zangu, msiwe kama watoto wadogo katika kufikiri kwenu. Kuhusu uovu muwe kama watoto wachanga, lakini katika kufi kiri, muwe watu wazima. 21 Imeandikwa katika sheria, “Kwa njia ya watu wenye lugha ngeni na kupitia midomo ya wageni, nitazun gumza na hawa watu, lakini hata hivyo hawatanisikiliza, asema Bwana.”
Bwana.”
22 Kwa hiyo lugha ngeni ni ishara kwa watu wasioamini, na si kwa ajili ya waamini. Lakini unabii ni kwa ajili ya waamini, na si kwa ajili ya wasioamini. 23 Kwa hiyo kama kanisa lote likiku tana na wote wakasema kwa lugha, kisha akaingia mgeni au asi yeamini, je, si atadhani wote mna kichaa? 24 Lakini ikiwa wote wanahubiri unabii wa neno la Mungu, na akaingia mtu asiyeamini au mgeni, atakuwa na uhakika kuwa yeye ni mwenye dhambi kutokana na yale yanayosemwa na wote, 25 na siri zote za moyo wake zitawekwa wazi. Kwa hiyo ataanguka chini na kumwabudu Mungu akisema, “Kweli Mungu yupo pamoja nanyi!”
Kumwabudu Mungu Kwa Mpango
26 Tuseme nini basi ndugu zangu? Mnapokutana pamoja, kila mtu ana wimbo, au neno la mafundisho, mafunuo, ujumbe katika lugha ngeni, au tafsiri ya lugha. Kila jambo lifanyike kwa sha baha ya kujengana. 27 Kama mtu akisema kwa lugha, basi waseme si zaidi ya wawili au watatu, mmoja baada ya mwingine; na lazima awepo mtu wa kutafsiri. 28 Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, huyo mzungumzaji akae kimya kanisani na aseme na nafsi yake mwe nyewe na Mungu. 29 Watu wawili au watatu walio na unabii wa neno la Mungu waseme, na wengine wapime kwa makini yale yanayosemwa. 30 Kama mmoja wa wale waliokaa akipata mafunuo kutoka kwa Mungu, anayezungumza aache kusema. 31 Kwa maana wote mnaweza kutoa una bii, mtu mmoja mmoja, ili kila mtu anayesikiliza apate kufund ishwa na kutiwa moyo. 32 Roho za unabii ziko chini ya mamlaka ya manabii. 33 Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko bali ni Mungu wa amani. Kama ilivyo desturi katika mikutano ya watu wa Mungu,
34 wanawake wanapaswa kukaa kimya kanisani. Hawaruhusiwi kusema, bali wanyenyekee kama sheria inavyosema. 35 Kama wakitaka kuu liza kitu, wawaulize waume zao nyumbani. Kwa maana ni aibu kwa mwanamke kuzungumza kanisani. 36 Je, mnadhani neno la Mungu lil itoka kwenu? Au ni ninyi tu ambao neno la Mungu limewafikia?
37 Kama mtu anadhani yeye ni nabii, au ana karama za kiroho, basi akubali kwamba haya ninayoandika ni amri kutoka kwa Bwana. 38 Kama mtu asipotambua haya hatatambuliwa. 39 Kwa hiyo ndugu zangu, takeni sana kutoa unabii na msikataze watu kusema kwa lugha. 40 Lakini kila kitu kitendeke kwa utaratibu mzuri.
Copyright © 1989 by Biblica