Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Ufunua wa Yohana 4-8

Kiti Cha Enzi Kilichoko Mbinguni

Baada ya hayo nilitazama, nikaona mlango ulio wazi mbin guni. Na ile sauti niliyokuwa nimeisikia ikisema nami kama tar umbeta ikasema, “Njoo huku juu nami nitakuonyesha yatakayotokea baada ya haya. ” Ghafla nilikuwa katika Roho, na mbele yangu kilikuwapo kiti cha enzi mbinguni, kikiwa kimekaliwa. Aliyeketi kwenye kiti hicho cha enzi alionekana kama jiwe zuri jekundu na akiki, na upinde wa mvua ulizunguka kile kiti cha enzi, ukione kana kama zumaridi. Kiti hicho kilizungukwa na viti vingine ishirini na vinne vya enzi ambavyo juu yake walikaa wazee ishi rini na wanne waliokuwa wamevalia mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani. Na katika kile kiti cha enzi kulitoka umeme, ngurumo na sauti. Taa saba za moto zilikuwa zinawaka mbele ya kile kiti cha enzi, ambazo ni zile roho saba za Mungu. Mbele ya kile kiti cha enzi kulikuwa na kitu kinachofanana na bahari ya kioo iking’aa kama jiwe la kioo. Katikati, kuzunguka kile kiti cha enzi, walikuwapo viumbe hai wanne, wenye macho kila mahali, mbele na nyuma.

Kiumbe hai wa kwanza alifanana na simba, wa pili alifanana na ng’ombe dume, wa tatu alikuwa na uso kama wa mwanadamu, wa nne alifanana na tai arukaye. Na hawa viumbe hai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita na macho kila mahali, hata chini ya mabawa. Usiku na mchana hawakuacha kuimba, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako, aliyeko na atakayekuja.”

Kila mara viumbe hao wanne walipomtukuza na kumheshimu na kumshukuru yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na aishie milele na milele, 10 wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele zake yeye aliyeketi kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Wakaziweka taji zao mbele ya kile kiti cha enzi wakisema, 11 “Bwana wetu na Mungu wetu, wewe umestahili kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa maana ni wewe uliyeviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako vitu vyote viliumbwa na vinapata kuwapo.”

Hati Na Mwana-Kondoo

Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwe nye kile kiti cha enzi hati iliyoandikwa ndani na nje, ambayo ilikuwa imefungwa na mihuri saba. Tena nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, “Ni nani anayestahili kufungua hati hii na kuvunja mihuri yake?” Lakini hakupatikana mtu mbinguni, juu ya nchi, wala chini ya nchi aliyeweza kufungua hati hiyo, wala kuitazama. Nililia sana kwa sababu hakupatikana mtu aliyestahili kuifungua hati hiyo wala kuitazama. Kisha, mmoja wapo wa wale wazee akaniambia, “Usilie! Tazama, yule simba wa kabila la Yuda, wa ukoo wa Daudi, ameshinda. Yeye anaweza kufun gua hati hiyo na kuvunja mihuri yake saba.” Katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wanne na wale wazee, nikaona Mwana- Kondoo amesimama, akionekana kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba, na macho saba, ambayo ni wale roho saba wa Mungu waliotumwa ulimwenguni kote . Huyo Mwana-Kondoo akaenda, akaichukua ile hati kutoka kwenye mkono wa kulia wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi. Alipokwisha kuichukua ile hati, wale viumbe wanne pamoja na wale wazee ishirini na wanne walianguka mbele ya yule Mwana-Kondoo. Kila mmoja wao alikuwa na kinubi, nao walikuwa wameshika mabakuli ya dhahabu yaliyojaa ubani , ambao ni maombi ya watu wa Mungu. Nao wakaimba wimbo mpya: “Wewe unastahili kuichukua hati na kuifungua mihuri yake. Kwa sababu wewe uliuawa na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu kutoka katika kila kabila na kila lugha; watu wa kila jamaa na kila taifa. 10 Umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, na watata wala ulimwenguni.” 11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti za mal aika wengi sana wakizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi ya hao mal aika ilikuwa ni maelfu na maelfu na kumi elfu mara kumi elfu. 12 Nao waliimba kwa sauti kuu, “Mwana -Kondoo aliyeuawa anasta hili kupewa uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima, na utukufu na sifa!” 13 Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, juu ya nchi na chini ya nchi, baharini na vyote vilivy omo baharini wakiimba, “Baraka na heshima na utukufu na uweza ni wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi; na kwa Mwana-Kondoo, hata milele na milele! 14 Na wale viumbe wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi wakaabudu.

Mwana- Kondoo Avunja Mihuri Saba

Kisha nikamwona Mwana -Kondoo akifungua mhuri wa kwanza kati ya ile mihuri saba. Nikasikia mmoja wa wale viumbe wanne akisema kwa sauti kama ya ngurumo: “Njoo!” Nikaangalia, na hapo mbele yangu nikaona farasi mweupe na aliyempanda alikuwa na upinde, na alipewa taji akatoka kama mshindi akaendelee kushinda.

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa pili, nikamsikia yule kiumbe hai wa pili akisema, “Njoo!” Akatoka farasi mwingine mwekundu sana na aliyempanda alipewa uwezo wa kuondoa amani duniani na kuwafanya watu wauane. Yeye alipewa upanga mkubwa.

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tatu, nilimsikia yule kiumbe hai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikaona farasi mweusi, na aliyempanda alikuwa na mizani mkononi mwake. Nikasikia kitu kama sauti kati ya hao viumbe wanne hai, ikisema, “Kibaba kimoja cha ngano kwa mshahara wa siku moja! na vibaba vitatu vya shayiri kwa mshahara wa siku moja! Lakini usi haribu mafuta wala divai!”

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa nne, nilisikia sauti ya yule kiumbe hai wa nne ikisema, “Njoo!” Nikaangalia na mbele yangu nikamwona farasi mwenye rangi ya kijivu. Aliyempanda huyo farasi aliitwa mauti, naye alikuwa akifuatana na kuzimu. Nao wal ipewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia.

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa tano, niliona chini ya madhabahu, roho za watu waliouawa kwa ajili ya neno la Mungu na kwa ushuhuda wao. 10 Wakalia kwa sauti kuu wakisema, “Bwana Mwenyezi, uliye mtakatifu na mwaminifu, utakawia mpaka lini kuwa hukumu na kulipiza kisasi juu ya watu wote waishio duniani kwa ajili ya damu yetu?” 11 Kisha kila mmoja wao akapewa kanzu nyeupe. Wakaambiwa wasubiri kidogo zaidi mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao wanaopaswa kuuawa kama wao walivyouawa, ita kapotimia.

12 Nilitazama Mwana-Kondoo alipokuwa akifungua muhuri wa sita. Pakatokea tetemeko kuu la nchi na jua likawa jeusi kama gunia lililotengenezwa kwa manyoya ya mbuzi. Mwezi wote ukawa mwekundu kama damu. 13 Nyota zikaanguka ardhini kama vile mat unda ya mtini yasiyokomaa yaangukavyo wakati mti wake unapoti kiswa na upepo mkali. 14 Anga ikatoweka kama vile karatasi inav yosokotwa; na kila mlima na kila kisiwa vikaondolewa mahali pake.

15 Ndipo wafalme wa duniani, wakuu wote, majemadari, mata jiri , wenye nguvu; na kila mtu, mtumwa na aliye huru, wakajifi cha mapangoni na kwenye miamba ya milima. 16 Wakaisihi milima na miamba wakisema, “Tuangukieni, mkatufiche tusionwe na uso wake yeye aketiye kwenye kiti cha enzi na mtuepushe na ghadhabu ya Mwana-Kondoo. 17 Kwa maana siku ile kuu ya ghadhabu yao imekuja, na ni nani awezaye kusalimika?”

Watu 144,000 Wawekewa Muhuri

Baada ya haya nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe zote nne za dunia wakizuia pepo nne za dunia, ili upepo usivume nchi kavu wala baharini wala kwenye mti wo wote. Kisha nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki akiwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akawaita kwa sauti kuu wale malaika waliokuwa wamepewa mamlaka kuidhuru nchi na bahari, akisema, “Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, mpaka tutakapoweka mihuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.”

Ndipo nikasikia idadi ya wale waliowekewa mihuri, watu 144,000 kutoka katika kila kabila la Waisraeli. Kabila la Yuda, 12,000, kabila la Rubeni 12,000, kabila la Gadi 12,000, kabila la Asheri 12,000, kabila la Naftali 12,000, kabila la Manase 12,000, kabila la Simioni 12,000, kabila la Lawi 12,000, kabila la Isakari 12,000, kabila la Zabuloni 12,000, kabila la Yusufu 12,000, kabila la Benyamini 12,000.

Umati Wa Watu Waliokombolewa

Kisha nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu ambao hakuna mtu awezaye kuwahesabu: watu wa kila taifa, kila kabila, kila jamaa na kila lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi na mbele ya Mwana-Kondoo. Walikuwa wamevaa mavazi meupe na wameshika matawi ya mitende mikononi mwao. 10 Nao walikuwa wakisema kwa sauti kuu, “Ukombozi hutoka kwa Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na kwa Mwana-Kondoo!” 11 Na wale malaika wote wakasi mama kuzunguka kile kiti cha enzi na wale wazee na wale viumbe hai wanne, wakaanguka chini mbele ya kile kiti cha enzi wakamwab udu Mungu, 12 wakisema, “ Amina! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na nguvu na uweza ni za Mungu wetu milele na milele! Amina”. 13 Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “Hawa watu waliovaa mavazi meupe, ni kina nani? Nao wametoka wapi?” 14 Nikamjibu, “Bwana, wewe ndiye unayefahamu.” Naye akasema, “Hawa ni wale waliotoka katika ile dhiki kuu; wameosha mavazi yao katika damu ya Mwana-Kondoo yakawa meupe kabisa. 15 Kwa hiyo, wanakaa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu na kumtumikia katika Hekalu lake usiku na mchana; naye aketiye katika kile kiti cha enzi atakuwa pamoja nao na kuwalinda. 16 Kamwe hawataona njaa wala kiu tena; jua wala joto kali halitawachoma tena. Kwa maana Mwana-Kondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchun gaji wao. Naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uzima; na

Muhuri Wa Saba

Mwana-Kondoo alipofungua muhuri wa saba, mbinguni palikuwa kimya kwa muda upatao nusu saa hivi. Kisha nikawaona wale mal aika saba wanaosimama mbele za Mungu, nao wakapewa tarumbeta saba.

Malaika mwingine aliyekuwa na chetezo cha dhahabu, alikuja akasimama mbele ya madhabahu. Akapewa ubani mwingi auchanganye pamoja na sala za watu wote wa Mungu, kwenye madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kile kiti cha enzi. Ule moshi wa ubani ukapanda juu mbele za Mungu, pamoja na maombi ya watu wa Mungu , kutoka mkononi mwa huyo malaika. Halafu yule malaika akachukua kile chetezo akakijaza moto kutoka kwenye ile madhabahu akautupa juu ya nchi. Pakatokea radi, ngurumo, umeme na tetemeko la nchi.

Tarumbeta Za Kwanza Nne

Kisha wale malaika saba waliokuwa na tarumbeta saba waka jiandaa kuzipiga. Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake, pakatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyika na damu, ikanyesha kwa nguvu juu ya nchi; na theluthi moja ya nchi ikateketea, na theluthi moja ya miti ikateketea na majani yote mabichi yakateke tea.

Malaika wa pili akapiga tarumbeta yake na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikageuka kuwa damu, theluthi moja ya viumbe hai waishio bahar ini wakafa na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.

10 Malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake, na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa ilianguka kutoka angani, ikaangukia theluthi moja ya mito na chemchemi za maji. 11 Nyota hiyo inaitwa “Uchungu”. Theluthi moja ya maji yakawa machungu, na watu wengi walikufa kutokana na maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.

12 Kisha malaika wa nne akapiga tarumbeta, na theluthi moja ya jua, theluthi moja ya mwezi na theluthi moja ya nyota, zika pigwa. Kwa hiyo theluthi moja ya mwanga wao ukawa giza. Theluthi moja ya mchana ilikuwa haina mwanga na pia theluthi moja ya usiku.

13 Halafu tena nikatazama, nikasikia tai mmoja akipiga kelele kwa sauti kuu wakati akiruka katikati ya mbingu, “Ole wao! Ole wao! Ole wao watu waishio duniani wakati itakaposikika milio ya tarumbeta ambazo karibuni zitapigwa na malaika watatu waliobakia.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica