Beginning
1 Kutoka kwa Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu. Kwa Kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watu wote wa Mungu walioko Akaya yote.
2 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Faraja Katika Mateso
3 Ashukuriwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa huruma na Mungu wa faraja zote. 4 Yeye anatufariji katika mateso yetu yote ili tuweze kuwafariji wale walio katika mateso yo yote, tukitumia faraja ambayo sisi tumepokea kutoka kwa Mungu. 5 Kama vile tunavyoshiriki mateso ya Kristo yaliyo mengi, ndivyo na far aja yetu inavyomiminika kwa wengine. 6 Kama tunateseka ni kwa faraja yenu na wokovu wenu; kama tukifarijiwa, ni kwa faraja yenu, ambayo mnapata wakati mkivumilia kwa subira mateso hayo hayo tunayopata sisi. 7 Matumaini yetu kwenu ni imara; kwa maana tunajua ya kuwa kama mnavyoshiriki katika mateso yetu, mtashiriki pia katika faraja yetu.
8 Hatupendi mkose kujua, ndugu wapendwa, kuhusu mateso tuliy oyapata huko Asia. Kwa maana tulilemewa na mizigo ambayo ilikuwa zaidi ya uwezo wetu kuvumilia, kiasi kwamba tulikata tamaa kwamba tungeishi. 9 Kwa hakika tulijisikia kana kwamba tumehukumiwa kifo. Lakini hii ilitokea ili tusijitegemee wenyewe bali tumtege mee Mungu ambaye anawafufua wafu. 10 Alituokoa katika hatari hiyo ya kifo, na atatuokoa. Tumeweka tumaini letu juu yake kwamba ataendelea kutuokoa. 11 Ninyi pia mtusaidie kwa maombi ili wengi wamshukuru Mungu kwa niaba yetu kwa ajili ya baraka tulizopokea kama majibu ya maombi ya wengi.
Paulo Abadili Mipango Yake
12 Hii ndio sababu tunajivuna. Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeishi katika ulimwengu, na hasa katika uhusiano wetu na ninyi, kwa utakatifu na ukweli utokao kwa Mungu. Hatukufanya hivyo kwa hekima ya mwanadamu bali kwa neema ya Mungu. 13 Kwa maana hatuwaandikii mambo ambayo hamwezi kusoma na kuyaelewa. Natumaini mtaelewa kikamilifu, 14 yale ambayo sasa mnayaelewa kwa sehemu, ili siku ile ya Bwana Yesu muweze kujivuna kwa ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili yenu.
15 Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa mambo haya, nilipanga kuwatembelea kwanza ili mpate baraka mara mbili. 16 Nilipanga kuwatembelea nikiwa safarini kwenda Makedonia, na kurudi kwenu tena nikitoka Makedonia ili mnisaidie katika safari yangu ya kwenda Uyahudi. 17 Je, nilikuwa kigeugeu nilipotaka kufanya hivi? Au mimi ninafanya mipango yangu kama watu wa dunia, nikiwa tayari kusema, “Ndiyo” na wakati huo huo kusema, “Hapana”?
18 Lakini kama Mungu alivyo mwaminifu, ahadi yangu haikuwa “Ndiyo” na “Hapana” 19 Kwa kuwa Mwana wa Mungu Yesu Kristo, ambaye tulimhubiri kwenu tukiwa na Silvano, Timotheo, na mimi mwenyewe, hakuwa ‘ndio’ na ‘hapana.’ Katika yeye wakati wote ni ndio. 20 Kwa maana ahadi zote za Mungu ni ‘ndio’ katika Kristo. Ndio sababu tunatamka ‘Amina’ kwa ajili yake, kwa utukufu wa Mungu. 21 Ni Mungu mwenyewe ambaye anatuwezesha sisi na ninyi kusimama imara katika Kristo. Ametuweka wakfu; 22 ametutia mhuri wake juu yetu, akatupa Roho wake mioyoni mwetu kama uthibitisho.
23 Mungu ni shahidi wangu kwamba niliacha kurudi Korintho kwa kuwahurumia. 24 Hatutaki kuwaamrisha kuhusu imani yenu bali tunafanya kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu; kwa maana mnasimama imara kwa imani.
2 Kwa sababu hiyo, niliamua kwamba sitafanya safari nyingine kuja kuwahuzunisha. 2 Kwa kuwa kama nawahuzunisha, ni nani ali yebaki kunifurahisha isipokuwa ninyi ambao nimewahuzunisha? 3 Ndio sababu nikawaandikia ili nitakapokuja nisihuzunishwe na watu ambao wangenifanya nifurahi. Nilikuwa na uhakika kwenu kwamba furaha yangu ingekuwa furaha yenu nyote. 4 Kwa maana nili waandikia katika dhiki na kutaabika moyoni na kwa machozi mengi. Shabaha yangu haikuwa kuwahuzunisha bali kuwaonyesha kina cha upendo wangu kwenu.
Msamaha Kwa Mwenye Dhambi
5 Basi ikiwa mtu ye yote amesababisha huzuni, kwa kiasi fulani hakunihuzunisha mimi kama alivyowahuzunisha ninyi nyote; sipendi kuweka uzito zaidi kwa upande wenu. 6 Basi adhabu aliyop ewa na wengi inamtosha. 7 Na sasa mnapaswa kumsamehe na kumfariji ili asikate tamaa kabisa kutokana na huzuni kubwa mno aliyo nayo. 8 Kwa hiyo nawasihi mumhakikishie tena kwamba mnampenda. 9 Nili waandikia kuwajaribu ili nione kama mtakuwa watii kwa kila kitu. 10 Mtu ye yote mnayemsamehe na mimi namsamehe. Cho chote nili chosamehe, kama kulikuwa na cha kusamehe, nimesamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo 11 ili shetani asije akatushinda. Kwa maana tunajua mipango yake.
12 Nilipofika Troa kuhubiri Injili ya Kristo, nilikuta Bwana ameshafungua mlango. 13 Lakini sikuweza kutulia kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito huko. Kwa hiyo nikaagana nao nikaenda Makedonia.
Ushindi Ndani Ya Kristo
14 Lakini Mungu ashukuriwe, ambaye hutuongoza katika ushindi tukiwa ndani ya Kristo. Naye hututumia sisi kueneza maarifa ya kumjua yeye kila mahali kama harufu nzuri. 15 Kwa Mungu sisi ni kama harufu nzuri ya manukato ya Kristo ambayo inatapakaa mion goni mwa wale wanaookolewa na wale wanaopotea. 16 Kwa wale wanaopotea sisi ni kama harufu ya kifo, lakini kwa wale wanaooko lewa sisi ni harufu iletayo uzima. Ni nani basi awezaye kufanya kazi hiyo? 17 Sisi si kama watu wengine ambao wanauza neno la Mungu wajipatie faida. Lakini kama watu wenye moyo safi, tuliot euliwa na Mungu mbele yake mwenyewe, sisi tunazungumza tukiwa ndani ya Kristo.
Wahudumu Wa Agano Jipya
3 Je mnadhani tunaanza kujisifu tena? Au tunahitaji kupata barua za utambulisho kwenu au kutoka kwenu, kama watu wengine wafanyavyo? 2 Ninyi wenyewe ni barua yetu ya utambulisho iliyoan dikwa katika mioyo yenu, ijulikane na kusomwa na kila mtu. 3 Ni dhahiri kwamba ninyi ni barua iliyoandikwa na Kristo, matokeo ya kazi yetu. Barua hii haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai.
4 Hili ndilo tumaini tulilo nalo kwa Mungu ndani ya Kristo. 5 Haina maana kwamba sisi tunaweza wenyewe kupima cho chote tuna chofanya, lakini uwezo wetu unatoka kwa Mungu. 6 Ni yeye ali yetuwezesha sisi kuwa wahudumu wa agano jipya, ambalo limefanywa, si kwa maandishi, bali kwa Roho. Kwa maana maandishi huleta kifo, lakini Roho huleta Uzima.
Utukufu Wa Agano Jipya
7 Sasa ikiwa huduma iliyoleta kifo, ambayo iliandikwa kwa herufi juu ya jiwe ilikuja kwa utukufu hata ikawa Waisraeli wal ishindwa kutazama uso wa Musa kwa sababu ya kung’aa kwake, ingawa ulikuwa ukififia, 8 je? Huduma ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi? 9 Ikiwa huduma inayowahukumu watu ina utukufu, huduma inayoleta haki si itakuwa na utukufu zaidi? 10 Hakika kwa hali hii, kilichokuwa na utukufu hapo mwanzo, sasa hakina utukufu tena kikilinganishwa na utukufu uliopo. 11 Na kama kilichokuwa kina fifia kilikuja kwa utukufu, utukufu wa kile kinachodumu ni zaidi sana!
12 Kwa hiyo kwa kuwa tunatumaini hili, tuna ujasiri. 13 Sisi si kama Musa, ambaye alifunika uso wake kwa kitambaa ili Waisraeli wasione ule mng’ao ulivyokuwa ukififia na kutoweka. 14 Lakini akili zao zilipumbaa, kwa maana mpaka leo akili zao zinafunikwa na kitambaa wakati agano jipya linaposomwa. Hicho kitambaa hakijaondolewa kwa maana ni Kristo peke yake anayeweza kukiondoa. 15 Hata leo, sheria ya Musa inaposomwa, bado kitambaa kinafunika akili zao. 16 Lakini wakati wo wote mtu anapomgeukia Bwana, “kitambaa kinaondolewa.” 17 Basi, Bwana ni Roho, na mahali alipo Roho wa Bwana pana uhuru. 18 Na sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa tunaonyesha, kama kwenye kioo, utukufu wa Bwana. Nasi tunabadilishwa tufanane naye, kutoka utukufu hadi utukufu wa juu zaidi, ambao unatoka kwa Bwana ambaye ni Roho.
Hazina Za Roho Kwenye Vyombo Vya Udongo
4 Kwa hiyo tukiwa na huduma hii kwa rehema ya Mungu, hatu kati tamaa. 2 Tumekataa njia za siri na za aibu. Hatutumii njia za udanganyifu, wala hatupotoshi neno la Mungu. Badala yake, tunaeleza neno la kweli wazi wazi na kujitambulisha kuwa wa kweli kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu. 3 Na hata kama Injili yetu imefichika, basi imefichika kwa wale wanaopotea. 4 Kwa upande wao, mungu wa dunia hii ametia giza akili za wasioamini, ili wasione mwanga wa Injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ana sura ya Mungu. 5 Kwa maana hatujihubiri sisi wenyewe ila tunamhu biri Yesu Kristo kuwa ni Bwana, na sisi ni watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 6 Kwa kuwa ni Mungu aliyesema, “Nuru iangaze katika giza,” ambaye ameangaza mioyoni mwetu kutupatia nuru ya ufahamu wa utukufu wa Mungu ung’aao katika uso wa Kristo.
7 Hata hivyo tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kuonyesha kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, na si kutoka kwetu. 8 Tumegandamizwa kila upande, lakini hatujashindwa. Tumetatanishwa lakini hatukati tamaa; 9 tumeteswa lakini hatuku achwa upweke; tumetupwa chini lakini hatujateketezwa. 10 Tuna chukua katika mwili wetu kifo cha Yesu wakati wote ili uhai wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu. 11 Kwa maana sisi tunaoishi, maisha yetu yako katika hatari ya kifo wakati wote kwa ajili ya Yesu ili uhai wake uweze kuonekana katika miili yetu ya mauti. 12 Kwa hiyo, mauti inatuandama wakati wote, bali uzima unafanya kazi ndani yenu. 13 Maandiko yanasema, “Niliamini, kwa hiyo nimesema.” Sisi pia tunaamini, kwa hiyo tunasema. 14 Kwa maana tunajua ya kuwa aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu na kutufikisha sisi na ninyi mbele zake. 15 Haya yote ni kwa ajili yenu, ili kwa kadiri neema ya Mungu inavyowafi kia watu wengi zaidi, wote watoe shukrani kwa utukufu wa Mungu.
16 Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa miili yetu inachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya kila siku. 17 Maana hii dhiki yetu nyepesi na ya muda mfupi inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa uzima wa milele unaozidi sana matatizo haya. 18 Kwa maana hatuweki mawazo yetu kwenye vitu vinavyoonekana bali kwenye vitu visivyoonekana. Maana vile vinavyoonekana ni vya muda mfupi, lakini vile visivyoonekana vinadumu milele.
Copyright © 1989 by Biblica