Beginning
Neno La Uzima
1 Tunawaandikieni kuhusu kile ambacho kimekuwapo tangu mwanzo, ambacho tumekisikia na kukiona kwa macho yetu; ambacho tumekigusa kwa mikono yetu; yaani Neno la uzima. 2 Uzima huo uli tokea, nasi tumeuona na tunaushuhudia, na tunawatangazieni uzima wa milele uliokuwa kwa Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. 3 Tunawa tangazia hicho tulichokiona na kukisikia ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi. Na ushirika tulio nao ni wetu na Baba na Mwa nae Yesu Kristo. 4 Tunawaandikieni mambo haya ili furaha yetu ikamilike.
Kutembea Nuruni
5 Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake, ambao tunawatan gazia: Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza kamwe. 6 Tukisema tuna ushirika naye huku tunaendelea kuishi gizani tunasema uongo, wala hatutendi yaliyo ya kweli. 7 Bali tukiishi nuruni, kama yeye alivyo nuru, tunakuwa na ushirika sisi kwa sisi na damu ya Mwanae Yesu, inatutakasa dhambi zote. 8 Tukisema kwamba hatuna dhambi tunajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. 9 Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwa minifu na wa haki na atatusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote. 10 Tukisema hatujatenda dhambi tunamfanya yeye kuwa mwongo, na neno lake halimo ndani yetu.
Upendo Na Utii
2 Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye mtetezi wetu kwa Baba, yaani Yesu Kristo mwenye haki. 2 Kristo ndiye sadaka iliyotolewa kwa ajili ya dhambi zetu, na wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.
3 Na tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua Kristo ikiwa tunatii amri zake. 4 Mtu ye yote akisema, “Ninamjua’ 5 Lakini mtu ye yote anayetii neno lake, huyo ndiye ambaye upendo wa Mungu umekamilika ndani yake kwa kweli. Hivi ndivyo tunavy ojua kuwa tumo ndani ya Kristo. 6 Mtu anayesema anadumu ndani ya Kristo anapaswa kuishi kama Yesu Kristo mwenyewe alivyoishi.
7 Wapendwa, siwaandikii amri mpya bali amri ile ambayo mme kuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilok wisha kusikia. 8 Lakini hata hivyo amri hii ninayowaandikieni ni mpya; ambayo ukweli wake unaonekana kwake na kwenu, kwa sababu giza linatoweka na nuru ya kweli imekwishaanza kuangaza. 9 Mtu anayesema kwamba anaishi nuruni, naye anamchukia ndugu yake, bado yumo gizani. 10 Anayempenda ndugu yake anaishi katika nuru na wala hana kitu cha kumfanya ajikwae. 11 Lakini anayemchukia ndugu yake anaishi gizani na anatembea gizani, wala hajui aen dako, kwa sababu giza limempofusha macho.
Kwa Watoto, Baba Na Vijana
12 Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya jina lake. 13 Ninawaandikieni ninyi akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Ninawandikieni ninyi watoto, kwa kuwa mmemjua Baba. 14 Ninawaan dikieni ninyi akina baba, kwa kuwa mmemjua yeye aliyekuwapo tangu mwanzo. Ninawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Msipende Dunia
15 Msiipende dunia wala mambo yaliyomo duniani. Kama mtu akiipenda dunia, hawezi kumpenda Baba. 16 Maana vitu vyote vil ivyomo duniani, yaani, tamaa za mwili, tamaa ya vitu vinavyoone kana kwa macho, na kiburi kiletwacho na mali, vyote hivi havitoki kwa Baba bali hutoka ulimwenguni. 17 Nayo dunia inapita na tamaa zake zote zinapita, lakini mtu anayetimiza mapenzi ya Mungu huishi milele.
Onyo Kuhusu Adui Wa Kristo
18 Watoto wapendwa, huu ni wakati wa mwisho. Na kama mlivy okwisha kusikia kwamba yule mpinga-Kristo anakuja, hata sasa wapinga-Kristo wengi wamekwisha kuja. Kwa hiyo tunajua kuwa huu ni wakati wa mwisho. 19 Watu hao walitoka kati yetu, lakini hawakuwa wa kundi letu. Kama wangekuwa wa kundi letu, wangeende lea kuishi pamoja nasi; lakini waliondoka ili iwe wazi kuwa hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kundi letu.
20 Lakini ninyi mmemiminiwa Roho Mtakatifu na nyote mnaijua kweli. 21 Siwaandikii hivi kwa kuwa hamuijui kweli bali kwa sababu mnaijua na kwa kuwa hakuna uongo utokao katika kweli. 22 Je, mwongo ni nani? Mwongo ni yule anayekana kwamba Yesu si Kristo. Mtu huyo ndiye mpinga-Kristo, anayemkana Baba na Mwana. 23 Mtu anayemkana Mwana hawezi kumjua Baba; mtu anayemkiri Mwana anamjua na Baba pia.
24 Hakikisheni kwamba ujumbe mliosikia tangu mwanzo unadumu mioyoni mwenu. Ujumbe huo ukikaa mioyoni mwenu, ninyi pia mtadumu ndani ya Mwana na ndani ya Baba. 25 Na yeye ametuahidi uzima wa milele.
26 Ninawaandikia mambo haya kuhusu wale wanaojaribu kuwapo tosha. 27 Lakini yule Roho Mtakatifu mliyempokea anakaa ndani yenu wala hamhitaji mtu kuwafundisha. Lakini kama vile huyo Roho Mtakatifu anavyowafundisha mambo yote, naye ni wa kweli wala si wa uongo; kama alivyowafundisha, dumuni ndani yake.
Watoto Wa Mungu
28 Na sasa, wanangu, kaeni siku zote ndani yake, kusudi ata kapotokea tuwe na ujasiri na wala tusijitenge naye kwa kuona aibu atakapokuja.
29 Kama mnajua kwamba yeye ni wa haki, basi mnajua kwamba kila atendaye haki amezaliwa naye.
Watoto Wa Mungu Wanavyopaswa Kuishi
3 Tazameni jinsi Baba alivyotupenda mno, hata tukaitwa watoto wa Mungu! Na hivyo ndivyo tulivyo. Watu wa ulimwengu hawatutambui kwa sababu hawakumjua Mungu. 2 Wapendwa, sisi sasa tu wana wa Mungu. Tutakavyokuwa baadaye haijulikani bado, lakini tunajua kwamba Kristo atakapotokea, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo.
Kujitakasa Na Kuacha Dhambi
3 Na kila mtu mwenye tumaini hili hujitakasa, kama yeye mwe nyewe alivyo mtakatifu.
4 Kila atendaye dhambi ana hatia ya kuvunja sheria; maana dhambi ni uvunjaji sheria. 5 Mnajua kwamba Kristo alikuja kuondoa dhambi naye hana dhambi yo yote. 6 Hakuna mtu anayedumu ndani ya Kristo ambaye anatenda dhambi; na mtu ye yote anayetenda dhambi, huyo hajapata kumwona Kristo wala kumjua.
7 Watoto wadogo, mtu asije akawadanganya. Kila atendaye haki ni mwenye haki, kama Kristo alivyo wa haki. 8 Kila atendaye dhambi ni wa shetani; kwa maana shetani ametenda dhambi tangu mwanzo. Mwana wa Mungu alikuja ili aziangamize kazi za shetani.
9 Mtu aliyezaliwa na Mungu haendelei na tabia ya kutenda dhambi, kwa maana ana asili ya Mungu; hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.
Kutenda Haki Na Kupendana
10 Na hivi ndivyo tunavyoweza kutambua wazi kati ya walio watoto wa Mungu na walio watoto wa shetani. Mtu ye yote asiyet enda lililo haki si wa Mungu; wala asiyempenda ndugu yake si wa Mungu. 11 Na ujumbe mliosikia tangu mwanzo ndio huu: kwamba tupen dane. 12 Msiwe kama Kaini ambaye alikuwa wa yule mwovu akamwua ndugu yake. Na kwa nini alimwua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu lakini matendo ya nduguye yalikuwa ya haki.
13 Ndugu zangu, msishangae watu wa ulimwengu wakiwachukia. 14 Tunajua hakika kwamba tumevuka kutoka kwenye kifo na kuingia kwenye uzima kwa maana tunawapenda ndugu zetu. Asiye na upendo anaishi katika kifo. 15 Kila anayemchukia ndugu yake ni mwuaji, na kama mjuavyo, hakuna mwuaji ambaye ana uzima wa milele ndani yake.
16 Na tumeujua upendo kwa sababu Kristo alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Na sisi tunapaswa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu zetu. 17 Lakini ikiwa mtu ana mali za hapa duniani na akamwona ndugu yake ana shida lakini akawa na moyo mgumu wala asimhurumie, mtu kama huyo anawezaje kusema anao upendo wa Mungu? 18 Wanangu, upendo wetu usiwe wa maneno matupu, bali upendo wetu udhihirishwe kwa vitendo na kweli.
19 Hivi ndivyo tutakavyoweza kuwa na hakika kwamba sisi ni wa kweli na hatutakuwa na wasiwasi mbele ya Mungu 20 hata kama dhamiri zetu zitatuhukumu; kwa maana tunajua kwamba Mungu ni mkuu kuliko dhamiri zetu, naye anajua kila kitu. 21 Wapendwa, ikiwa dhamiri zetu hazituhukumu, tuna ujasiri mbele za Mungu; 22 nasi tunapokea kutoka kwake lo lote tuombalo kwa kuwa tunatii amri zake na kufanya yampendezayo. 23 Na amri yake ndio hii: tuliamini jina la Mwanae Yesu Kristo na kupendana, kama alivyotu agiza. 24 Wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Na hivi ndivyo tunavyojua kwamba anaishi ndani yetu: tunajua kwa njia ya yule Roho aliyetupatia.
Kujihadhari Na Maadui Wa Kristo
4 Wapendwa, msiamini kila roho bali zipimeni roho zote kwa makini muone kama zinatoka kwa Mungu. Kwa maana manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2 Na hivi ndivyo mtakavyomtambua Roho wa Mungu: kila roho inayokiri kuwa Yesu Kristo alikuja kama mwana damu, hiyo inatoka kwa Mungu. 3 Lakini roho yo yote ambayo haim kiri Kristo, si ya Mungu. Hii ndio roho ya mpinga-Kristo, ambayo mmekwisha kusikia kwamba inakuja, na sasa tayari iko duniani.
4 Lakini ninyi watoto wapendwa, ni wa Mungu, nanyi mmekwisha kuwashinda; kwa maana yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yule aliyeko duniani. 5 Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanayoyasema ni ya ulimwengu na watu wa dunia huwasikiliza. 6 Sisi ni wa Mungu. Anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiye wa Mungu hatusikilizi. Na hivi ndivyo tunaweza kutambua kati ya Roho wa kweli na roho wa uongo.
Mungu Ni Upendo
7 Wapendwa, tupendane, kwa sababu upendo hutoka kwa Mungu. Mtu mwenye upendo amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu. 8 Mtu asiye na upendo hamjui Mungu; kwa maana Mungu ni upendo. 9 Na hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha upendo wake kwetu: alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni ili kwa ajili yake sisi tupate kwa kupitia kwake. 10 Na huu ndio upendo: si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi hata akamtuma Mwanae awe sadaka ya kulipia dhambi zetu. 11 Wapendwa, kwa kuwa Mungu ali tupenda kiasi hicho, sisi pia tunapaswa kupendana. 12 Hakuna mtu aliyepata kumwona Mungu; lakini tukipendana, Mungu anaishi ndani yetu, na upendo wake unakamilika ndani yetu.
13 Tunajua ya kwamba tunaishi ndani yake na yeye anaishi ndani yetu kwa sababu ametupatia Roho wake. 14 Na sisi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanae awe mwokozi wa ulim wengu. 15 Kila mtu anayekiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, na yeye hukaa ndani ya Mungu. 16 Kwa hiyo tunajua na kutegemea upendo alio nao Mungu kwetu sisi. Mungu ni upendo, na mtu mwenye upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17 Upendo unakamilishwa ndani yetu ili tuwe na uja siri siku ile ya hukumu; kwa maana hata katika ulimwengu huu sisi tunaishi kama yeye. 18 Katika upendo hakuna woga; upendo ulioka milika hufukuza woga wote, kwa sababu woga hutokana na adhabu. Mtu mwenye woga hajakamilishwa katika upendo. 19 Tunapenda kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20 Mtu akisema, “Nampenda Mungu,” na huku anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Kwa maana mtu asipompenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamwona. 21 Na Mungu mwenyewe ametupa amri hii kwamba, mtu anayempenda Mungu hana budi kumpenda pia na ndugu yake.
Imani Ndani Ya Kristo
5 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ndiye Kristo, ni mtoto wa Mungu; na kila ampendaye mzazi wa mtoto, humpenda pia na mtoto wa mzazi huyo. 2 Na hivi ndivyo tunavyojua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu: tukimpenda Mungu na kuzitii amri zake. 3 Kwa maana kumpenda Mungu ni kuzitii amri zake. Na amri zake hazitule mei. 4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu ameushinda ulimwengu. Nasi tumeushinda ulimwengu kwa imani yetu. 5 Ni nani basi aushin daye ulimwengu isipokuwa yeye aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?
Mashahidi Wa Yesu Kristo
6 Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji na damu; si kwa maji peke yake, bali kwa maji na damu. Roho mwenyewe ndiye anayemshu hudia kwa maana Roho ni kweli. 7 Wapo mashahidi watatu: 8 Roho, maji na damu; na hawa watatu wanakubaliana. 9 Kama tunakubali ushahidi wa wanadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; kwa sababu huu ni ushahidi wa Mungu ambao ameutoa kumhusu Mwanae. 10 Mtu anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushuhuda huo ndani yake. Mtu asiyemwamini Mungu, amemfanya Mungu kuwa ni mwongo, kwa sababu hakuamini ushuhuda alioutoa Mungu kuhusu Mwanae. 11 Na ushuhuda wenyewe ndio huu: Mungu ametupatia uzima wa milele, na uzima huu umo kwa Mwanae. 12 Aliye naye Mwana anao uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana uzima.
Uzima Wa Milele
13 Ninawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini jina la Mwana wa Mungu kusudi mjue kuwa mnao uzima wa milele. 14 Na sisi tunao ujasiri huu mbele za Mungu kwamba, tukiomba cho chote sawa na mapenzi yake, atatusikia. 15 Na tukijua kwamba anatusikia kwa lo lote tunaloomba basi tuna hakika kwamba tumekwisha pata yale tuliyomwomba.
Umuhimu Wa Kuonyana
16 Mtu akimwona ndugu yake akitenda dhambi isiyompeleka kwe nye kifo, amwombee kwa Mungu, naye Mungu atampatia uzima. Ninasema kuhusu wale waliotenda dhambi ambazo si za kifo. Lakini ipo dhambi ambayo humpeleka mtu kwenye kifo. Sisemi kwamba ana paswa kuomba kuhusu hiyo. 17 Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi na kuna dhambi isiyompeleka mtu kwenye kifo.
18 Tunafahamu kuwa kila aliyezaliwa na Mungu haendelei kutenda dhambi; kwa sababu Mwana wa Mungu humlinda na yule mwovu hawezi kumgusa. 19 Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na kwamba ulim wengu wote unatawaliwa na yule mwovu. 20 Tunajua pia kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupa ufahamu ili tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Copyright © 1989 by Biblica