Beginning
Kuhusu Ufunuo Huu
1 Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili apate kuwaonyesha watumishi wake mambo yatakayotokea karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe mtumishi wake Yohana, 2 ambaye ameandika yale yote aliyoyaona, yaani ujumbe wa neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. 3 Amebarikiwa anayesoma maneno ya unabii huu na wale wanaosikiliza na kuzingatia yale yaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia.
Salamu Kwa Makanisa Saba
4 Kutoka kwa Yohana. Kwa Makanisa saba yaliyoko Asia: Ninawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu aliyeko, ambaye alikuwako na atakayekuja; na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;
5 na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake;
6 akatufanya sisi kuwa wafalme na makuhani, tum tumikie Mungu Baba yake. Utukufu na uwezo ni wake milele na milele! Amina.
7 Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. 8 “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi.”
Yohana Alivyopata Ufunuo
9 Mimi ni Yohana, ndugu yenu na mwenzenu katika mateso, na katika ufalme na subira kwa ajili ya Yesu Kristo. Niliwekwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya kutangaza neno la Mungu na kumshuhudia Yesu. 10 Basi, siku ya Bwana nilikuwa katika Roho, nikasikia sauti kubwa kama ya tarumbeta nyuma yangu 11 ikasema, “Andika haya yote unayoyaona kwenye kitabu, kisha ukipeleke kwe nye makanisa saba yafuatayo: Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”
Sardi, Filadelfia na Laodikia.”
12 Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Na nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu. 13 Katikati ya vile vinara, nikaona mtu kama mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu na mkanda wa dhahabu kifuani. 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji; na macho yake yalikuwa kama moto uwakao. 15 Miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa katika tanuru ya moto; na sauti yake ilikuwa kama sauti ya mapo romoko ya maji. 16 Katika mkono wake wa kulia alishika nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling’aa kama jua kali.
17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mfu. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu akasema, “Usiogope. Mimi ni wa kwanza na wa mwisho. 18 Mimi ni Yeye aliye hai; nili kufa na tazama, mimi ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu. 19 Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yatakayotokea baadaye. 20 Maana ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia na vile vinara saba vya taa vya dha habu ni hii: zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni hayo makanisa saba.”
Ujumbe Kwa Kanisa La Efeso
2 “Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: ‘Haya ni maneno ya yule aliyeshika nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. 2 Najua matendo yako, bidii yako na uvumilivu wako. Najua kuwa huwezi kuvumilia watu waovu na kwamba umewapima wale wanaojiita mitume na kumbe sio, na umetambua ya kuwa wao ni waongo. 3 Najua umevumilia na kustahimili mateso kwa ajili ya jina langu, wala hujachoka .
4 Lakini nina neno hili juu yako: kwamba umeacha upendo wako wa kwanza. 5 Kumbuka pale ulipokuwa kabla ya kuanguka. Tubu, uache dhambi zako, ukafanye matendo ya mwanzo. Kama hukuacha dhambi zako, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. 6 Lakini una jambo moja zuri: unayachukia matendo ya Wanikolai kama ninavyoyachukia mimi.
7 Mwenye nia ya kusikia na ayasikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa . Atakayeshinda, nitampa haki ya kula matunda ya mti wa uzima ambao uko katika bustani ya Mungu.”’
Ujumbe Kwa Kanisa La Smirna
8 “Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye wa kwanza na wa mwisho; aliyekufa kisha akawa hai tena.
9 Naijua dhiki yako na umaskini wako, ingawaje kwa kweli wewe ni tajiri! Najua matukano wanayokutukana wale wanaojiita Wayahudi lakini si Wayahudi; wao ni sinagogi la shetani. 10 Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuhakikishia kuwa shetani atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu. Nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
11 Mwenye nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaam bia makanisa. Atakayeshinda hatadhuriwa na kifo cha pili.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Pergamo
12 “Kwa malaika wa Kanisa la Pergamo andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili.
13 Ninajua unakoishi, kule ambako shetani ameweka kiti chake cha enzi. Hata hivyo umelishika jina langu, wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji wenu, ambao ni maskani ya shetani.
14 Lakini nina mambo machache juu yako: baadhi yenu ni wafu asi wa mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki awashaw ishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa dhabihu kwa miungu na kufanya uasherati. 15 Na tena baadhi yenu wanafu ata mafundisho ya Wanikolai. 16 Basi tubuni mwache dhambi zenu: ama sivyo nitakuja hivi karibuni na kupigana na watu hao kwa upanga utokao kinywani mwangu.
17 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho ana waambia makanisa. Atakayeshinda nitampa sehemu ya ile mana iliy ofichwa, nami nitampa jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.’
Ujumbe Kwa Kanisa La Thiatira
18 “Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika hivi: ‘Haya ni maneno ya Mwana wa Mungu ambaye macho yake ni kama moto uwakao, na miguu yake inang’aa kama shaba iliyosuguliwa sana. 19 Nayajua matendo yako, upendo wako, imani yako, huduma na subira yako; na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya mwanzo.
20 Hata hivyo ninalo jambo hili juu yako: unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kwa miungu. 21 Nimempa muda atubu, aache uasher ati, lakini hataki kutubu. 22 Kwa hiyo nitamtupa kitandani kwa ugonjwa, na atapata mateso makali pamoja na hao wanaozini naye wasipotubu matendo yake. 23 Tena nitawaua watoto wake. Ndipo makanisa yote yatajua kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na akili za watu na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 24 Lakini ninawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamfuati mafundisho ya Yezebeli, wala ham kujifunza hayo wengine wanayoyaita ‘siri za ndani’ za shetani, sitawaongezea mzigo mwingine. 25 Bali mshike sana hicho mlicho nacho mpaka nitakapokuja.
26 Atakayeshinda na kuendelea kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa. 27 ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma na kuwavunja vipande vipande kama chombo cha udongo 28 Pia nitampa ile nyota ya asubuhi. 29 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anawaambia makanisa.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Sardi
3 “Kwa malaika wa Kanisa la Sardi andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye na zile Roho saba za Mungu na zile nyota saba. Nayajua matendo yako; na kwamba una sifa ya kuwa hai, na kumbe umekufa. 2 Amka! Imarisha kilichobakia kabla hakijaharibika kabisa, kwa maana nimeona kwamba kazi zako hazijakamilika mbele za Mungu wangu. 3 Kumbuka basi yale uliyoyapokea na kuyasikia, yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi wala huta jua saa nitakayokujia.
4 Bado wako watu wachache huko Sardi ambao hawajachafua mavazi yao. Wao watatembea pamoja nami wakiwa wamevaa mavazi yao meupe kwa maana wanastahili. 5 Atakayeshinda atavikwa vazi jeupe kama wao, nami sitafuta jina lake katika kitabu cha uzima bali nitalikiri jina lake mbele ya Baba yangu na mbele za malaika wake.
6 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anayaam bia makanisa.”’
Ujumbe Kwa Kanisa La Filadelfia
7 “Kwa malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ufunguo wa Daudi. Anachokifungua hakuna awezaye kukifunga, na anachoki funga hakuna awezaye kukifungua.
8 Nayajua matendo yako. Tazama, nimeweka mbele yako mlango ulio wazi ambao hakuna awezaye kuufunga. Ninajua kwamba ingawa nguvu yako ni ndogo lakini umelishika neno langu na hujalikana jina langu. 9 Sikiliza, wale watu ambao ni wa sinagogi la she tani, wale wajiitao Wayahudi kumbe sio, bali ni waongo; nitawafa nya waje wapige magoti mbele yako na wakiri kwamba nimekupenda. 10 Kwa kuwa umeshika agizo langu la kustahimili kwa subira, nitakulinda wakati wa ile dhiki itakayokuja duniani pote kuwajar ibu waishio ulimwenguni.
11 Ninakuja upesi. Shika sana kile ulicho nacho asije mtu akachukua taji yako. 12 Atakayeshinda nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu wala hatatoka humo kamwe. Na nitaan dika juu yake jina la Mungu wangu na jina la mji wake Mungu wangu, Yerusalemu mpya, ambao unakuja kutoka mbinguni kwa Mungu wangu. Pia nitaandika juu yake jina langu jipya.
13 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Ujumbe Kwa Kanisa La Laodikia
14 “Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika hivi: ‘Haya ni maneno yake yeye aitwaye Amina, shahidi mwaminifu na wa kweli, mtawala wa vyote alivyoumba Mungu.
15 Nayajua matendo yako; kwamba wewe si baridi wala si moto. Afadhali kama ungalikuwa baridi au moto. 16 Basi, kwa kuwa wewe ni vuguvugu, si baridi wala si moto, nitakutapika utoke kinywani mwangu. 17 Unajigamba ukisema, ‘Mimi ni tajiri , nimefanikiwa wala sihitaji kitu cho chote.’ Lakini hutambui kwamba wewe ni mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, maskini, kipofu; tena wewe ni uchi. 18 Kwa hiyo ninakushauri ununue kutoka kwangu dhahabu iliyosaf ishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri; na mavazi meupe ili upate kuvaa, ufiche aibu ya uchi wako. Ujinunulie pia mafuta uyapake macho yako ili upate kuona.
19 Wote niwapendao, ninawakaripia na kuwarudi. Kwa hiyo fanya bidii, utubu na kuziacha dhambi zako. 20 Tazama, nasimama mlangoni napiga hodi. Mtu ye yote akisikia sauti yangu na kufun gua mlango, nitaingia ndani na kula pamoja naye, naye pamoja nami. 21 Atakayeshinda nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu kwenye kiti chake cha enzi. 22 Aliye na nia ya kusikia na asikie yale ambayo Roho anay aambia makanisa.’ ”
Copyright © 1989 by Biblica