Beginning
1 Kutoka kwa Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo. Mimi nimetumwa kwa wale ambao Mungu amewateua ili niwaon goze katika imani na katika maarifa ya kweli yanayopatana na kum cha Mungu; 2 na katika tumaini la uzima wa milele ambalo Mungu, ambaye hasemi uongo, aliahidi hata kabla dunia haijakuwepo. 3 Naye kwa wakati aliopanga alidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo nilikabidhiwa kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu.
4 Ninakuandikia wewe Tito, mwanangu halisi katika imani tunayoshiriki pamoja. Ninakutakia neema na amani kutoka kwa Mungu
Kazi Ya Tito Kule Krete
5 Nilikuacha huko Krete kusudi urekebishe mambo yote yal iokuwa hayakunyooka na uchague wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na lawama yo yote; awe mume wa mke mmoja; awe ni mtu ambaye watoto wake ni waamini na wala sio jeuri au wasiotii. 7 Kwa kuwa askofu amekabidhiwa kazi ya Mungu, anapaswa kuwa mtu asiye na lawama. Asiwe mwenye majivuno, mwepesi wa hasira, mlevi, mgomvi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyokuwa ya halali. 8 Bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye kujitawala, mnyofu, mtakatifu na mwe nye kudhibiti na si yake. 9 Ni lazima alishike kwa uthabiti neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwafundisha wengine na kudhihirisha makosa ya wale wanaolipinga.
Walimu Wa Uongo
10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.
16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.
Mafundisho Sahihi
2 Lakini wewe, mafundisho yako ni lazima yawe sahihi. 2 Wafundishe wazee kuwa na kiasi, watulivu, wenye busara na tha biti katika imani, upendo na subira. 3 Hali kadhalika akina mama wazee wawe na mwenendo wa unyenyekevu. Wasiwe wachonganishi, wala wasiwe watumwa wa pombe; bali waonyeshe mfano mwema. 4 Hivyo wawafundishe akina mama vijana kuwapenda waume zao na watoto wao 5 na kuwa wenye kiasi na safi, wakitumia wakati wao kushughulika nyumbani mwao. Wawe wema na watii kwa waume zao, ili neno la Mungu lisije likadharauliwa kwa ajili yao. 6 Vile vile uwahimize vijana kuwa na kiasi. 7 Katika mambo yote wewe mwenyewe uwe kielelezo cha matendo mema. Uonyeshe usa hihi na uthabiti katika mafundisho yako. 8 Maneno yako yawe na kina na mantiki safi, mtu asiweze kuyatoa kasoro na hata yule anayepinga aaibike kwa kukosa lo lote baya la kusema juu yetu.
9 Wahimize watumwa kuwatii mabwana wao na kuwapendeza katika mambo yote; wasijibishane nao 10 wala kuwaibia, bali watumwa waonyeshe kuwa wanaweza kuaminika kabisa ili katika kila hali mafundisho ya Mungu Mwokozi wetu yapate sifa njema.
11 Kwa maana neema ya Mungu iletayo wokovu imedhihirishwa kwa watu wote. 12 Neema hiyo inatufundisha kukataa uovu na tamaa za dhambi, tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya kumcha Mungu, katika ulimwengu huu. Wakati huo huo 13 tukingojea tumaini letu lenye baraka - kuja kwa utukufu wa Mungu wetu Mkuu na Mwokozi wetu, Yesu Kristo. 14 Yeye alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu ili atukomboe katika uasi wote, na kutufanya tuwe safi kwa ajili yake; na tuwe watu wake kabisa, ambao wana juhudi katika kutenda mema.
15 Fundisha mambo haya; himiza na kemea kwa mamlaka yote. Mtu ye yote asikudharau.
Kutenda Mema
3 Wakumbushe watu kujinyenyekeza kwa watawala na watu wenye mamlaka; wawe watii na wepesi kufanya kazi yo yote halali. 2 Wakumbushe wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wapole na waonyeshe unyenyekevu kwa kila mtu.
3 Maana kuna wakati ambapo sisi wenyewe tulikuwa wajinga, wakaidi; tukidanganywa na daima kutawaliwa na tamaa mbaya na anasa za kila aina. Tulikuwa tukiishi maisha ya uovu na wivu, tukichukiwa na watu na kuchukiana sisi kwa sisi. 4 Lakini wakati wema na upendo wa Mungu Mkombozi wetu ulipodhihirishwa, 5 ali tuokoa, si kwa sababu ya matendo mema ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya huruma yake. Alituokoa kwa kuoshwa na kuzaliwa mara ya pili na kufanywa wapya kwa njia ya Roho Mtakatifu, 6 ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kwa njia ya Yesu Kristo Mwokozi wetu. 7 Na tukishahesabiwa haki kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele tunaoutumainia . 8 Neno hili ni kweli kabisa. Ninataka uyatilie mkazo mambo haya ili wale waliomwamini Mungu waone umuhimu wa kutenda mema wakati wote, maana mambo haya ni mazuri na tena ni ya manufaa kwa watu.
9 Lakini jiepushe na ubishi wa kipuuzi: mambo kama orodha ndefu za vizazi na ubishi na ugomvi juu ya sheria; haya hayana maana wala hayamsaidii mtu ye yote. 10 Mtu anayesababisha mafarakano, muonye mara ya kwanza na mara ya pili. Baada ya hapo, usijishughulishe naye tena. 11 Una jua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi ambaye amejihukumu mwenyewe.
Maagizo Ya Mwisho
12 Nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja Nika poli unione, maana nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya bar idi. 13 Wahimize Zena, yule mwanasheria, na Apolo waje upesi na uhakikishe kwamba hawapungukiwi na kitu cho chote. 14 Watu wetu hawana budi kujifunza kuona umuhimu wa kutenda mema, ili waweze kusaidia watu wenye mahitaji ya lazima na maisha yao yasikose kuwa na matunda.
1 Mimi Paulo, mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu, pamoja na ndugu yetu Timotheo. Tunakuandikia wewe Filemoni mfanyakazi mwenzetu mpendwa, na dada yetu Afia na askari mwenzetu Arkipo, 2 pamoja na kanisa linalokutana nyumbani kwako 3 Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu
Upendo Na Imani Ya Filemoni
4 Ninamshukuru Mungu wangu kila ninapokuombea 5 kwa sababu ninasikia habari za upendo wako na imani uliyonayo kwa Bwana wetu Yesu na kwa watakatifu wote. 6 Ninakuombea kwamba unaposhirikiana na wengine juu ya imani yako upate kuelewa kikamilifu kila jambo jema ambalo tunapata ndani ya Kristo. 7 Ndugu yangu, upendo wako umenipa furaha kubwa na faraja, kwa maana wewe umechangamsha mioyo ya watakatifu.
Ombi Kuhusu Onesmo
8 Kwa sababu hii, ingawa nina ujasiri ndani ya Kristo kuku amuru ufanye linalotakiwa, 9 lakini kwa ajili ya upendo, ninaona ni bora zaidi nikuletee ombi. Mimi Paulo, balozi ambaye sasa ni mfungwa kwa ajili ya Yesu Kristo, 10 ninalo ombi kwako kuhusu mwanangu Onesmo; ambaye nimekuwa baba yake wa kiroho nikiwa gere zani. 11 Hapo awali huyu Onesmo alikuwa hakufai, lakini sasa amekuwa wa manufaa kwako na kwangu pia.
12 Ninamrudisha kwako, yeye ambaye ni kama moyo wangu mwe nyewe. 13 Ningelipenda akae nami hapa anisaidie badala yako wakati huu ambapo niko gerezani kwa ajili ya Injili. 14 Lakini sikupenda kufanya lo lote pasipo wewe kuniruhusu maana sipendi unisaidie kwa kulazimishwa, bali kwa hiari yako mwenyewe.
15 Pengine Onesmo aliondoka kwako kwa muda mfupi kusudi uta kapompata tena uweze kuwa naye daima; 16 na asiwe tena kama mtumwa tu, bali kama ndugu mpendwa. Yeye ni wa thamani sana kwangu lakini hasa zaidi kwako, maana pamoja na kuwa mtumwa wako, sasa ni ndugu yako katika Bwana.
17 Kwa hiyo ikiwa unanihesabu kama mshiriki mwenzako, basi mpokee kama vile ambavyo ungenipokea mimi. 18 Kama amekukosea jambo lo lote au ana deni lako, basi unidai mimi. 19 Mimi Paulo ninaandika jambo hili kwa mkono wangu mwenyewe, nitalipa. Wala sidhani nina haja ya kukukumbusha kwamba wewe mwenyewe ni mdeni wangu kwa ajili ya nafsi yako. 20 Kwa hiyo ndugu yangu, ninaamini utafanya jambo hili kwa ajili ya Bwana. Burudisha moyo wangu katika Kristo.
21 Naandika nikiwa na hakika ya kuwa utatii ninalokuambia na kwamba utafanya hata zaidi ya haya. 22 Tena nakuomba unitayar ishie chumba cha kukaa, kwa maana natarajia kurudi kwenu kama jibu la Mungu kwa maombi yenu.
23 Salamu zenu kutoka kwa Epafra, mfungwa mwenzangu kwa ajili ya Kristo Yesu; 24 na kutoka kwa Marko, Aristarko, Dema na
Copyright © 1989 by Biblica