Beginning
Kuhusu Melkizedeki, Kuhani Mkuu
7 Huyu Melkizedeki alikuwa ni mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu aliye juu. Abrahamu alipokuwa akirudi kutoka vitani ambako aliua wafalme wengi, Melkizedeki alikutana naye, akambariki. 2 Abrahamu akampatia Melkizedeki sehemu ya kumi ya vitu vyote. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “Mfalme wa haki” na pia yeye ni “Mfalme wa Salemu,” maana yake, “Mfalme wa amani.”
3 Yeye hana baba wala mama wala ukoo; hana mwanzo wala hana mwisho, bali kama alivyo Mwana wa Mungu, yeye adumu kuwa kuhani milele.
4 Angalieni jinsi alivyo mkuu! Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 5 Hata wana wa Lawi ambao ni makuhani, wameamriwa na sheria ya Mose kuwatoza Waisraeli ndugu zao, ambao ni wazao wa Abrahamu, sehemu ya kumi ya mapato yao. 6 Ingawa huyu Melkizedeki si wa ukoo wa Lawi, alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu , na akambariki huyu ambaye alikwisha pokea ahadi za Mungu. 7 Wala hakuna ubishi kuwa mtu mdogo hubarikiwa na mtu aliye mkuu kuliko yeye. 8 Kwa upande wa makuhani wa ukoo wa Lawi, sehemu ya kumi inapokelewa na binadamu ambao hufa; lakini kwa upande huu wa Melkizedeki, sehemu ya kumi inapokelewa na mtu ambaye tunahakikishiwa kuwa anaishi. 9 Mtu anaweza kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, 10 kwa maana Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado hajazaliwa. Mbegu yake ilikuwa bado iko mwilini mwa Abrahamu babu yake.
Yesu Na Melkizedeki
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”
Melkizedeki.”
18 Sheria ya mwanzo imewekwa kando kwa kuwa ilikuwa dhaifu na tena haikufaa. 19 Kwa maana sheria haikufanya kitu cho chote kuwa kikamilifu, na sasa tumeletewa tumaini bora zaidi ambalo linatuwezesha kumkaribia Mungu.
20 Na tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wale waliofa nywa makuhani huko nyuma hapakuwepo kiapo. 21 Bali Yesu alipofa nywa kuhani aliwekewa kiapo wakati Mungu alipomwambia: “Bwana ameapa wala hatabadili nia yake, ‘Wewe ni kuhani milele.”’
22 Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
23 Makuhani wa zamani walikuwa wengi kwa sababu kifo kiliwa zuia kuendelea daima na huduma yao. 24 Lakini yeye anaendelea na ukuhani wake daima kwa maana anaishi milele. 25 Kwa hiyo anaweza kwa wakati wote kuwaokoa wale wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye anaishi daima ili kuwaombea.
26 Huyu ndiye kuhani mkuu tunayemhitaji: yeye ni mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetenganishwa na wenye dhambi na aliyeinuliwa juu ya mbingu. 27 Yeye hahitaji kutoa dhabihu kila siku kwa ajili ya dhambi zake kwanza kisha dhambi za watu, kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu mara moja kwa wakati wote, alipojitoa mwenyewe. 28 Kwa maana sheria ya Mose huchagua watu wenye udhaifu kuwa makuhani wakuu. Lakini neno la Mungu la kile kiapo ambalo lilikuja baada ya sheria, lil imteua Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.
Kuhani Mkuu Wa Agano Jipya
8 Basi, katika hayo yote, tunalosema ni hili: tunaye huyo kuhani mkuu, ambaye ameketi upande wa kuume wa kiti cha Mwenyezi mbinguni. 2 Yeye ni mhudumu wa patakatifu katika ile hema ya kweli iliyowekwa na Bwana, na wala si na wanadamu.
3 Kila kuhani huteuliwa ili atoe sadaka na dhabihu, kwa hiyo ilikuwa muhimu kwamba huyu kuhani naye awe na kitu cha kutoa. 4 Kama angalikuwa duniani asingalikuwa kuhani kwa sababu wapo makuhani wanaotoa sadaka kwa mujibu wa sheria ya Mose. 5 Wanahu dumu katika patakatifu iliyo mfano na kivuli cha ile iliyoko mbinguni. Ndio maana Mose alipokaribia kujenga ile hema takatifu aliamriwa na Mungu, akisema, “Hakikisha kuwa unafanya kila kitu kulingana na mfano ulioonyeshwa mlimani.” 6 Lakini Yesu amepewa huduma iliyo bora zaidi kuliko yao, kama vile lile agano ambalo yeye ni mpatanishi wake, lilivyo bora zaidi kuliko lile la zamani. Agano hili jipya limejengwa juu ya ahadi bora zaidi.
7 Kama lile agano la kwanza lisingekuwa na upungufu, kusinge kuwapo na haja ya kuwa na agano jingine. 8 Lakini Mungu hakurid hika na watu wake, akasema, “Siku zinakuja, asema Bwana, nitaka pofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. 9 Agano hili halitakuwa kama lile nililofanya na baba zao siku ile nilipowashika mkono niwaongoze kutoka nchi ya Misri; kwa kuwa hawakuwa waaminifu kwa agano langu, nami nikawaacha, asema Bwana. 10 Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli siku zile zitakapowadia, asema Bwana: nitaweka sheria zangu akilini mwao, na kuziandika mioyoni mwao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 11 Haitakuwapo haja tena kwao kumfundisha kila mtu mwenzake, au kila mtu ndugu yake, na kusema, ‘Mfahamu Bwana,’ kwa maana wote watanifahamu, tangu aliye mdogo kabisa hadi mkubwa kuliko wote. 12 Nitawasamehe maovu yao, na dhambi zao sitazikum buka tena”.
13 Anapozungumza juu ya agano jipya Mungu anahesabu lile agano la kwanza kuwa limechakaa, na kitu kilichochakaa na kuzeeka kitatoweka baada ya muda mfupi.
Agano La Kwanza Na Agano Jipya
9 Basi hata lile agano la kwanza lilikuwa na kanuni zake za ibada pamoja na mahali pa kuabudia hapa duniani. 2 Hema la kuabu dia liliandaliwa likiwa na chumba cha kwanza ambamo mlikuwa na chombo cha kuwekea taa, na meza na mikate iliyowekwa wakfu. Chumba hiki kiliitwa Patakatifu. 3 Nyuma ya pazia la pili, pali kuwa na chumba kiitwacho Patakatifu pa Patakatifu. 4 Chumba hiki kilikuwa na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba na sanduku la agano ambalo lilifunikwa kwa dhahabu pande zote. Sanduku hili lilikuwa na chombo cha dhahabu chenye ile mana na ile fimbo ya Aroni iliyochipuka, na yale mawe ya agano. 5 Juu ya sanduku kulikuwa na makerubi wa utukufu ambao kivuli chao kilifunika kiti cha rehema. Lakini mambo haya sasa hatuwezi kuyaeleza kwa undani.
6 Vitu vyote vilipokwisha kupangwa namna hii, makuhani wal iingia mara kwa mara katika kile chumba cha kwanza kutoa huduma yao ya ibada. 7 Lakini ni kuhani mkuu peke yake ambaye aliruhu siwa kuingia katika chumba cha ndani mara moja tu kwa mwaka. Tena ilibidi aingie huko na damu ambayo aliitoa kwa ajili yake mwe nyewe na kwa ajili ya dhambi za watu walizotenda pasipo kujua. 8 Kwa njia hii, Roho Mtakatifu alikuwa akionyesha kwamba maadamu hema ya kwanza ilikuwa bado imesimama, njia ya kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu ilikuwa bado haijafunguliwa. 9 Hii ili kuwa ni kielelezo kwa wakati wa sasa, kuonyesha kwamba sadaka na dhabihu zilizotolewa zilikuwa haziwezi kutakasa dhamiri ya mtu anayeabudu. 10 Hizi zilikuwa ni sheria zinazohusu chakula na vinywaji na taratibu mbalimbali za utakaso wa nje, kanuni ambazo zingetumika mpaka wakati wa matayarisho ya utaratibu mpya.
Damu Ya Kristo Husafisha Dhamiri
11 Kristo alipokuja kama kuhani mkuu wa mambo mema ambayo tayari yamekwisha wasili, alipitia kwenye hema ya kuabudia ambayo ni kuu zaidi na bora zaidi na ambayo haikujengwa na binadamu, yaani ambayo si sehemu ya ulimwengu huu ulioumbwa. 12 Yeye aliingia patakatifu pa patakatifu mara moja tu kwa wakati wote, akichukua, si damu ya mbuzi na ndama, bali damu yake mwenyewe, na hivyo kutupatia ukombozi wa milele.
13 Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama hunyunyizwa juu ya watu wachafu kidini ikawatakasa kwa kuwaondolea uchafu wao wa nje, 14 damu ya Kristo ambaye kwa njia ya Roho wa milele alijitoa mwenyewe kwa Mungu kama sadaka isiyokuwa na doa, itazisafisha dhamiri zetu zaidi sana kutokana na matendo yaletayo kifo, na kutuwezesha kumtumikia Mungu aliye hai.
15 Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa agano jipya ili wale walioitwa wapokee urithi wa milele ulioahidiwa na Mungu; kwa kuwa alikufa awe fidia itakayowaweka huru na dhambi walizotenda chini ya agano la kwanza.
16 Ili hati ya urithi itambuliwe ni lazima pawepo na uthi bitisho kwamba huyo aliyeiandika amekwisha kufa. 17 Kwa maana hati ya urithi huwa na uzito tu wakati mtu amekwisha kufa; haiwezi kutumika wakati yule aliyeiandika angali hai. 18 Hii ndio maana hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu kumwagika. 19 Wakati Musa alipowatangazia watu amri zote za sheria, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo akanyunyizia kitabu cha sheria na watu wote, 20 akasema, “Hii ndio damu ya agano ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 21 Vivyo hivyo akanyunyizia damu hiyo kwe nye lile hema na vifaa vyote vilivyotumika kwa ibada. 22 Hakika katika sheria, karibu kila kitu hutakaswa kwa damu; na pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.
23 Kwa hiyo ilikuwa muhimu vitu hivi ambavyo ni mfano wa vile vya mbinguni vitakaswe kwa njia hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. 24 Kwa maana Kristo hakuingia kwenye hema ya kuabudia iliyotengenezwa na bina damu kama mfano wa hema halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ambapo sasa anatuwakilisha mbele za Mungu. 25 Wala hakuingia mbinguni kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama kuhani mkuu ain giavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka na damu ambayo si yake. 26 Ingekuwa hivyo, ingalimpasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini ilivyo ni kwamba ametokea mara moja tu kwa wakati wote, katika siku hizi za mwisho, ili atokomeze dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 27 Na kama ambavyo mwanadamu ameandikiwa kufa mara moja tu, na baada ya hapo kukabili hukumu; 28 hali kadhalika Kristo alitolewa kama dhabihu mara moja tu ili azichukue dhambi za watu wengi; naye atakuja mara ya pili, si kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngojea kwa hamu.
Dhabihu Ya Kristo Ilikuwa Ya Mwisho
10 Basi kwa kuwa sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo na wala si mambo yenyewe, haiwezi kamwe, kwa njia ya dhabihu zito lewazo mwaka hadi mwaka, kuwakamilisha wale wanaoabudu. 2 Kama isingekuwa hivyo, dhabihu hizo zingekuwa hazitolewi tena. Maana hao waabuduo wasingalijiona tena kuwa wana hatia kwa ajili ya dhambi zao baada ya kutakaswa mara moja. 3 Badala yake, dhabihu hizo zilikuwa ni ukumbusho wa dhambi mwaka hadi mwaka. 4 Kwa maana damu ya mafahali na mbuzi, haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
5 Kwa sababu hii, Yesu alipokuja duniani alisema: “Hukutaka dhabihu na sadaka bali umeniandalia mwili. 6 Hukupendezwa na sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi. 7 Ndipo nikasema, ‘Nipo hapa, kama ilivyoandikwa katika gombo la sheria kunihusu; nimekuja kutimiza mapenzi yako wewe Mungu.’ ”
8 Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa wala sadaka zitolewazo kwa ajili ya dhambi hukutaka, wala huku pendezwa nazo,” ingawa hizi zilitolewa kwa mujibu wa sheria. 9 Kisha akasema, “Niko hapa, nimekuja kutimiza mapenzi yako.” Anaweka kando ule utaratibu wa kwanza na kuanzisha utaratibu wa pili. 10 Na kwa mapenzi hayo, sisi tumetakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu, kwa wakati wote.
11 Kila kuhani husimama siku hadi siku akifanya huduma yake ya ibada na akitoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kuondoa dhambi. 12 Lakini Kristo alipokwisha kutoa dhabihu yake kwa ajili ya dhambi mara moja tu kwa wakati wote, aliketi upande wa kulia wa Mungu. 13 Tangu wakati huo anangoja mpaka Mungu atakapowafanya maadui zake kuwa kiti cha miguu yake. 14 Maana kwa dhabihu moja tu amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.
15 Roho Mtakatifu pia anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema: 16 “Hili ndilo agano nitakalofanya nao baada ya siku hizo, asema Bwana. Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao na kuziandika akilini mwao.” 17 Kisha anasema: “Dhambi zao na makosa yao sitayakumbuka tena kamwe.”
18 Basi, haya yakishasamehewa, hakuna tena dhabihu inayoto lewa kwa ajili ya dhambi.
Haja Ya Kuwa Imara
19 Kwa hiyo ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, 20 kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kupitia lile pazia, yaani kwa njia ya mwili wake, 21 na kwa kuwa tunaye kuhani mkuu anayemiliki nyumba ya Mungu; 22 basi tumkaribie Mungu kwa moyo wa kweli na imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya na miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. 23 Tushikilie kwa makini tumaini tunalokiri kwa maana yeye ali yeahidi ni mwaminifu. 24 Na tujishughulishe kutafuta jinsi ya kuhimizana katika kuonyeshana upendo na kutenda mema. 25 Tusiache kukutana pamoja, kama wengine wanavyofanya, bali tutiane moyo, hasa zaidi tunapoona siku ile ikikaribia.
Hatari Ya Kukufuru
26 Kama tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kupokea na kufahamu ile kweli, hakuna tena dhabihu iliyobaki inayoweza kutolewa kwa ajili ya dhambi. 27 Kinachobakia ni kungojea kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza maadui zake. 28 Mtu aliyevunja sheria ya Mose aliuawa pasipo huruma kwa usha hidi wa watu wawili au watatu. 29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani zaidi anastahili kupewa mtu ambaye anamdharau na kum kataa Mwana wa Mungu, na ambaye anaona kuwa damu ya agano iliyom takasa si kitu, na ambaye amemtukana Roho wa neema? 30 Kwa maana tunamjua yeye aliyesema, “Kulipiza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipiza.” Pia alisema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 31 Kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai ni jambo la kutisha.
32 Kumbuka siku zile za mwanzo baada ya kupokea mwanga, jinsi mlivyovumilia mapambano makali na mateso. 33 Wakati mwin gine mlitukanwa na kuteswa hadharani; wakati mwingine mlikuwa radhi kuungana na wale walioteswa hivyo. 34 Mliwaonea huruma waliokuwa kifungoni, na mkakubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu kwa maana mlifahamu kwamba mlikuwa na mali bora zaidi inay odumu.
35 Kwa hiyo msitupe tumaini lenu, ambalo litapewa tuzo kubwa. 36 Mnahitaji kuvumilia ili mkisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi. 37 “Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu yeye anayekuja atakuja , wala hatakawia; 38 lakini mtu wangu mwenye haki ataishi kwa imani, na akirudi nyuma sitapendezwa naye.”
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaorudi nyuma wakaangamizwa, bali sisi ni miongoni mwa wanaoamini wakaokolewa.
Copyright © 1989 by Biblica