Beginning
1 Kutoka kwa Simoni Petro mtumishi na mtume wa Yesu Kristo. Kwa wote ambao wamepokea imani yenye thamani kama yetu kutokana na haki ya Mungu wetu na Mwokozi Yesu Kristo.
2 Nawatakieni neema na amani tele katika kumjua Mungu na Yesu
Wito Wa Kuishi Maisha Ya Kikristo
3 Uweza wake wa kimungu umetupatia mambo yote yanayohusiana na uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake. 4 Kwa njia hiyo ametupatia ahadi zake kuu na za tha mani. Mkishika ahadi hizo mtashiriki asili yake ya kimungu na kuepuka uovu ambao uko duniani kwa sababu ya tamaa mbaya.
5 Kwa sababu hii, jitahidini sana kuongeza wema katika imani yenu; na katika wema ongezeni maarifa; 6 na katika maarifa ongezeni kiasi; na katika kiasi ongezeni ustahimilivu; na katika ustahimilivu ongezeni kumcha Mungu; 7 na katika kumcha Mungu ongezeni upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu ongezeni upendo. 8 Maana mkiwa na sifa hizi kwa wingi zitawawe zesha kuwa wenye bidii na wenye kuzaa matunda katika kumfahamu Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Lakini mtu asiyekuwa na sifa hizi ni kipofu, haoni mbali, na amesahau kuwa ametakaswa dhambi zake za zamani.
10 Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuuhakikisha wito wenu na uteule wenu, kwa maana mkifanya hivyo, hamtaanguka kamwe; 11 na mtakaribishwa kwa fahari kubwa katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Unabii Wa Maandiko
12 Kwa hiyo ninakusudia kuwakumbusha hayo siku zote, ingawa mnayafahamu na mmekuwa imara katika kweli mliyo nayo. 13 Nadhani ni vema niwahimize kwa kuwakumbusha mambo haya, wakati wote nina poishi katika mwili huu. 14 Kwa maana najua kwamba karibu nitauweka kando mwili wangu, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyon ionyesha wazi. 15 Na nitahakikisha kwamba baada ya kuondoka kwangu mtaendelea kukumbuka mambo haya kila wakati.
16 Tulipowafundisha juu ya uweza na kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo, hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, bali tulish uhudia kwa macho yetu utukufu wake. 17 Maana alipopewa heshima na utukufu kutoka kwa Mungu Baba, na sauti ikamjia katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye’ 18 tuliisikia sauti hii iliyotoka mbinguni, maana tulikuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.
19 Kwa hiyo tuna uhakika zaidi juu ya ujumbe wa manabii. Hivyo itakuwa vema mkizingatia ujumbe huo, kama vile watu wanavy oitegemea taa ing’aayo mahali penye giza, mpaka Siku ile itakapo fika na nyota ya asubuhi itakapoangaza mioyoni mwenu. 20 Kwanza kabisa ni lazima muelewe kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliotokana na tafsiri ya nabii mwenyewe. 21 Kwa sababu hakuna unabii uliokuja kwa matakwa ya binadamu, bali watu walinena ujumbe kutoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Walimu Wa Uongo
2 Lakini pia walikuwepo manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyotokea walimu wa uongo kati yenu. Kwa siri, watain giza mafundisho ya upotovu hata kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watajiletea maangamizi ya haraka. 2 Na wengi wata fuata tamaa zao potovu, na kwa ajili ya matendo yao njia ya kweli itadharauliwa. 3 Nao katika tamaa yao watajaribu kuwanunua kwa kuwaambia hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu yao imekuwa tayari tangu zamani, wala mwangamizi wao hajalala usingizi.
4 Maana kama Mungu hakuwahurumia malaika walipotenda dhambi bali aliwatupa kuzimu, katika vifungo vya giza wakae huko mpaka siku ya hukumu; 5 kama hakuuhurumia ulimwengu wa kale alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa watu wasiomcha Mungu, akamlinda Noe mjumbe wa haki, pamoja na watu saba wengine; 6 kama aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kwa kuiteketeza ikawa majivu, akaifanya kuwa mfano kwa wote ambao hawatamcha Mungu; 7 na kama alimwokoa Loti, mtu mwenye haki ambaye alihuzunishwa na maisha ya uchafu ya watu wahalifu - 8 kwa sababu yale maasi aliyoona na kusikia huyo mtu wa Mungu alipoishi kati yao yalimhuzunisha usiku na mchana - 9 basi ikiwa ni hivyo, Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wa Mungu kutoka katika majaribu na kuwaweka waasi katika hali ya adhabu mpaka siku ya hukumu. 10 Hii ni hakika hasa kwa wale wanaofuata tamaa chafu za mwili na kudharau mamlaka. Watu hawa ni shupavu na katika kiburi chao, hawaogopi kuwatu kana viumbe vitukufu wa mbinguni;
11 ingawa hata malaika, ambao wana nguvu na uwezo zaidi, hawawashtaki au kuwatukana viumbe hao mbele za Bwana. 12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiy oyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawal iwa na hisia za mwili, ambao wamezaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa, na kama wanyama, wao pia wataangamizwa.
13 Watalipizwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Furaha yao ni kufanya karamu za ufisadi mchana, wazi wazi. Wao huleta aibu na fedheha wanaposhiriki katika karamu zenu kwa kuwa wakati wote huo, wanajifurahisha katika upotevu wao. 14 Macho yao yamejaa uzinzi, nao hutenda dhambi bila kikomo. Huwahadaa watu dhaifu. Mioyo yao imezoea kutamani. Hawa ni wana wa laana! 15 Wameiacha njia iliyonyooka, wakapotoka na kuifuata njia ya Balaamu mwana wa Beori aliyependa kupata fedha kwa kufa nya maovu. 16 Balaamu alikaripiwa kwa ajili ya uovu wake. Punda ambaye hasemi alinena kwa sauti ya binadamu akamzuia huyo nabii asiendelee na kichaa chake.
17 Watu hawa ni kama chemchemi zilizokauka na ukungu upeper ushwao na tufani, na lile giza jeusi limewekwa tayari kwa ajili yao. 18 Wao hutamka maneno matupu ya majivuno na kutumia tamaa mbaya za mwili kuwanasa tena wale ambao ndio kwanza wameepukana na watu wanaoishi maisha ya uovu. 19 Huwaahidi hao waliowanasa kuwa watakuwa huru kabisa, lakini wao wenyewe ni watumwa wa upo tovu. Kwa maana mtu huwa mtumwa wa kitu kile kinachomshinda nguvu. 20 Kwa maana wale waliokwisha kuponyoka kutoka katika uchafu wa dunia hii kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo , kisha wakanaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho ni mbaya zaidi kuliko ile ya kwanza. 21 Ingekuwa heri kwao kama hawa kuijua kamwe njia ya haki, kuliko kuifahamu kisha wakaiacha ile amri takatifu waliyopewa. 22 Kama methali moja isemavyo, “Mbwa huyarudia matapishi yake mwenyewe,” na nyingine, “Nguruwe huoshwa na kurudi kugaa-gaa matopeni.”
Siku Ya Bwana
3 Rafiki wapendwa, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua zote mbili nimejaribu kuziamsha nia zenu safi kwa kuwakumbusha mambo haya. 2 Napenda mkumbuke maneno yaliyosemwa zamani na manabii watakatifu na ile amri ya Bwana na Mwokozi mli yopewa na mitume wenu. 3 Kwanza kabisa ni lazima muelewe hili: kwamba siku za mwisho watu wenye dhihaka watakuja kuwadhihaki wakiwa wametawaliwa na tamaa zao wenyewe. 4 Watawaambia, “Ali yeahidi atakuja yuko wapi? Tangu baba zetu walipokufa mambo yam eendelea kuwa kama yalivyokuwa tangu kuumbwa kwa dunia.” 5 Wao wameamua kusahau kwamba ni kwa neno la Mungu mbingu zilikuwepo tangu zamani, na kwamba ulimwengu uliumbwa kutokana na maji kwa njia ya maji, 6 na kuwa kwa maji hayo hayo ulimwengu ule uliokuwepo uliangamizwa wakati ule wa gharika. 7 Lakini kwa neno hilo hilo mbingu na dunia, ambazo zipo hivi sasa, zimewekwa akiba kuchomwa moto, zimewekwa mpaka siku ile ya hukumu na ya kuangami zwa kwa watu wasiomcha Mungu.
8 Lakini wapendwa msisahau neno hili, kwamba kwa Bwana, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. 9 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kama watu wengine wanavyochukulia kukawia, bali yeye anawavumilia, maana hapendi mtu ye yote aan gamie, bali wote waifikie toba.
10 Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwizi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; na vitu vya asili vitateketezwa kwa moto na dunia na vitu vyote vilivyomo humo vitateketezwa.
11 Kwa kuwa kila kitu kitateketezwa hivyo, ninyi je, mna paswa kuwa watu wa namna gani? Mnapaswa kuishi maisha ya utaka tifu na utauwa, 12 mkingojea na mkiharakisha kuja kwa siku ya Mungu, siku ambayo mbingu zitateketezwa kwa moto na kutoweka, na vitu vyote vilivyomo ndani yake vitayeyushwa kwa moto! 13 Lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunangojea mbingu mpya na dunia mpya ambamo haki huishi.
14 Kwa hiyo wapendwa, kwa kuwa mnatazamia mambo haya, jita hidini ili mkutwe hamna doa wala lawama, mkiwa na amani naye. 15 Hesabuni uvumilivu wa Bwana kuwa ni wokovu, kama ndugu yetu mpendwa Paulo alivyokwisha kuwaandikieni kwa hekima aliyopewa na Mungu. 16 Ameandika hivyo hivyo katika barua zake zote akizun gumzia mambo haya. Barua zake zina mambo mengine ambayo ni magumu kuelewa, ambayo watu wajinga na wasio na msimamo huyapotosha, kama wanavyopotosha sehemu nyingine za Maandiko; na hivyo wana jiletea kuangamia.
17 Basi, ninyi wapendwa mkijua haya, jihadharini msije mka potoshwa na makosa ya hao waasi na kupoteza uthabiti wenu.
Copyright © 1989 by Biblica