Beginning
1 Kutoka kwa Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu. Kwa watu wa Mungu walio waaminifu kwa Kristo Yesu. 2 Nawa takieni neema ya Mungu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 3 Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametu bariki sisi kwa kila baraka za kiroho zitokazo mbinguni tukiwa ndani ya Kristo. 4 Mungu alituchagua sisi tuwe ndani ya Kristo hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na lawama mbele zake. 5 Kwa upendo wake, alipanga kabla ya mambo yote, kutufanya sisi kuwa watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo kwa mapenzi yake mwenyewe; 6 na hivyo apewe sifa kwa ajili ya neema yake tukufu ambayo tumepewa bure katika Mpendwa wake. 7 Kutoka kwake, tunapata ukombozi kwa ajili ya damu yake, yaani, kusamehewa dhambi zetu; kulingana na wingi wa neema yake 8 ambayo ametumiminia kwa wingi. 9 Kwa maana ametufahamisha kwa hekima yote na ufahamu, siri ya mapenzi yake, kulingana na mpango aliokusudia kuukamilisha kwa njia ya Kristo. 10 Mpango huo ambao ungetekelezwa wakati ukitimia, ni kwamba Mungu ataviunganisha vitu vyote po pote vilipo, mbinguni na duniani, viwe kwake chini ya Kristo. 11 Tukiwa ndani ya Kristo, tulichaguliwa kama alivy opanga Mungu kwa makusudio yake yeye ambaye hufanya mambo yote kulingana na mapenzi yake. 12 Kwa njia hiyo, sisi ambao tulikuwa wa kwanza kumtegemea Kristo, tupate kuishi maisha yatakayoleta sifa kwa utukufu wake. 13 Ninyi pia mliingia ndani ya Kristo mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Nanyi mmemwa mini, mkawekewa muhuri na Roho Mtakatifu ambaye mliahidiwa, 14 yeye ndiye dhamana ya urithi wetu mpaka hapo tutakapoupokea, kwa sifa ya utukufu wake. Shukrani Na Maombi
15 Hii ndio sababu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana wetu Yesu, na juu ya upendo mlio nao kwa watu wa Mungu, 16 sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu, na kuwakumbuka katika sala zangu. 17 Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awajalieni roho ya hekima na ya mafunuo mpate kumfahamu zaidi. 18 Ninaomba pia kwamba macho ya mioyo yenu yaangaziwe ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na mtambue utajiri wa urithi wa utukufu wake kwa watu wa Mungu; 19 na muu fahamu uweza wake usiopimika ambao ametupa sisi tunaoamini. Uweza huo ni sawa na ile nguvu kuu 20 ambayo aliitumia alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamweka akae mkono wake wa kulia katika enzi yake mbinguni. 21 Hapo alipo ni juu sana, kupita tawala na mamlaka zote na nguvu zote na milki, na kupita cheo cho chote kinachoweza kutolewa, si tu katika nyakati hizi, bali pia katika nyakati zijazo. 22 Na Mungu ameweka vitu vyote viwe chini ya mamlaka yake na akamteuwa awe mkuu wa vitu vyote kwa ajili ya kanisa, 23 ambalo ni mwili wake, nalo limejawa na yeye ambaye hujaza kila kitu kwa kila njia. Tumefanywa Kuwa Hai Ndani Ya Kristo
2 Nanyi aliwafanya muwe hai, mlipokuwa mmekufa kiroho kwa ajili ya makosa na dhambi zenu. 2 Hapo zamani mliishi maisha ya jinsi hiyo, mkimtii mfalme wa nguvu za anga, ambaye ndiye ile roho inayowatawala wote wanaomwasi Mungu. 3 Sisi sote pia tuliishi miongoni mwao hapo zamani, tukiridhisha na kutawaliwa na tamaa mbaya za mwili na mawazo. Kwa hiyo sisi pia tulikuwa kwa asili tunastahili ghadhabu ya Mungu kama binadamu wengine wote. 4 Lakini Mungu, ambaye ana huruma nyingi, kutokana na upendo wake mkuu ambao alitupenda nao, 5 japokuwa tulikuwa bado tumekufa kiroho kwa sababu ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu. Mmeokolewa kwa neema. 6 Mungu alitufufua pamoja na Kristo, akatufanya tukae pamoja naye katika makao ya mbinguni tukiwa ndani yake Kristo; 7 ili katika vizazi vijavyo aonyeshe wingi wa neema yake isiyo na mfano, ambayo imedhihirishwa kwa wema wake kwetu sisi tunaoishi ndani ya Kristo Yesu. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na si kwa sababu ya matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu mwenyewe. 9 Na kwa sababu hamkuifanyia kazi, mtu ye yote asije akajisifu juu ya wokovu wake. 10 Kwa maana sisi ni matokeo ya kazi ya Mungu tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tuwe na matendo mema ambayo Mungu alikwisha andaa, tuishi katika hayo. 11 Kwa hiyo kumbukeni kwamba ninyi ambao kwa asili ni watu wa mataifa mengine, mnaoitwa ‘wasiotahiriwa’ na wale ‘waliotahi riwa’ kwa kanuni za binadamu; 12 kumbukeni kwamba wakati ule ninyi mlikuwa mmetengwa na Kristo, mkiwa mmefarakana na jumuia ya Israeli na mkiwa wageni kuhusu yale maagano ya ahadi. Mlikuwa hamna matumaini wala Mungu duniani. 13 Lakini kwa kuwa mmeungana na Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali zamani, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. 14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu; yeye aliyetufanya tuwe jamii moja, akavunjavunja ule ukuta wa uadui uliotutenga 15 kwa kuifuta ile sheria na amri zake na kan uni zake alipoutoa mwili wake. Alifanya hivyo ili aumbe taifa jipya kutokana na jamii mbili: Wayahudi na watu wa mataifa, na hivyo alete amani. 16 Kwa kutoa mwili wake pale msalabani, ali patanisha jamii zote mbili na Mungu; na kwa njia hiyo akaua ule uadui uliokuwepo kati yao. 17 Alikuja akahubiri amani kwenu ninyi watu wa mataifa ambao mlikuwa mbali na Mungu, na pia kwa wale waliokuwa karibu na Mungu. 18 Kwa maana, kwa kupitia kwake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa, tunaweza kumkaribia Baba katika Roho mmoja. 19 Kwa hiyo, ninyi sasa siyo wageni tena wala wapita njia, bali mmekuwa raia halisi pamoja na watu wa Mungu na familia ya Mungu. 20 Ninyi mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ndiye jiwe kuu la pembeni. 21 Ndani yake yeye, jengo lote limeunganishwa pamoja na kusimam ishwa kuwa Hekalu takatifu la Mungu. 22 Katika yeye ninyi pia mnajengwa pamoja ili mpate kuwa makao ambamo Mungu anaishi kwa njia ya Roho wake. Paulo, Mhudumu Kwa Watu Wa Mataifa
3 Kwa sababu hii, mimi Paulo, nimekuwa mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi watu wa mataifa. 2 Ninaamini kwamba mmek wisha sikia kuwa Mungu amenipa neema yake niwe mhudumu kwa ajili yenu; 3 na kwamba Mungu alinifahamisha siri hii kwa njia ya mafu nuo, kama nilivyokwisha andika kwa kifupi. 4 Kwa hiyo mtakaposoma barua hii mtaweza kutambua ufahamu niliopewa kuhusu siri ya Kris to. 5 Siri hii haikufahamika kwa watu wa vizazi vilivyopita kama ilivyodhihirishwa sasa na Roho kwa mitume na manabii watakatifu wa Mungu. 6 Siri hii ni kwamba, kwa njia ya Injili, watu wa mataifa ni warithi pamoja na Waisraeli; na wote pamoja ni viungo vya mwili mmoja, na ni washiriki kwa pamoja wa ile ahadi aliyotoa Mungu katika Kristo Yesu. 7 Niliteuliwa kuwa mtumishi wa Injili hii kwa kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa uwezo wake uliokuwa ukifanya kazi ndani yangu. 8 Ingawa mimi ni mdogo kuliko hata aliye mdogo kabisa kati ya watu wote wa Mungu, nilipewa neema hii, niwahubirie watu wa mataifa kuhusu utajiri usiopimika ulio ndani ya Kristo. 9 Na nieleze wazi wazi ili watu wote waone jinsi siri hii itakavyotekelezwa. Siri hii ilikuwa imefichwa tangu awali kwa Mungu aliyeumba vitu vyote. 10 Yeye alikusudia kwamba sasa, kwa njia ya kanisa, hekima yote ya Mungu ipate kufa hamika kwa mamlaka na nguvu zote katika makao ya mbinguni. 11 Mpango huu ulikuwa sawasawa na mapenzi yake yaliyotimi zwa katika Kristo Yesu Bwana wetu, 12 ambaye tukiwa ndani yake, tuna ujasiri na uhakika wa kumkaribia Mungu kwa njia ya imani katika Kristo. 13 Kwa hiyo, nawasihi msikate tamaa kutokana na mateso ninayopata kwa ajili yenu; mateso haya ni utukufu wenu. Sala Ya Paulo Kwa Waefeso
14 Kwa sababu hii napiga magoti mbele ya Mungu Baba, 15 aliye baba wa familia ya waamini wote, mbinguni na duniani. 16 Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyoni mwenu kwa njia ya Roho wake kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake. 17 Na naomba kwamba, kwa imani, Kristo aendelee kuishi ndani ya mioyo yenu, ili mkiwa mmesimama imara na kujengwa katika upendo, 18 mpate uwezo wa kuelewa, pamoja na watu wote wa Mungu, upana na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo; 19 na mpate kufa hamu upendo huu, ingawa unapita upeo wa maarifa, na hivyo mpate kujazwa kabisa na ukamilifu wa Mungu mwenyewe. 20 Utukufu ni wake yeye, ambaye ana uwezo wa kutenda zaidi ya yale tunayoyaomba na kuyawazia, kwa kadiri ya nguvu yake inayofanya kazi ndani yetu. 21 Utukufu ni wake katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amina.
Copyright © 1989 by Biblica