Beginning
4 Basi, mimi niliye mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mu ishi maisha yanayostahili wito mlioitiwa. 2 Muwe wanyenyekevu, wapole, wenye subira, mkivumiliana ninyi kwa ninyi katika upend o. 3 Muwe wepesi wa kutaka kudumisha umoja wa Roho kwa sababu ya amani inayowafunga pamoja. 4 Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, k ama mlivyoitwa mpokee tumaini moja. 5 Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja; 6 na Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wot e, aliye juu ya wote, anayefanya kazi katika yote na aliye ndani ya yote. 7 Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo alichogawiwa na Kristo. 8 Kwa hiyo Maandiko yanasema: “Alipopaa juu, aliongoza mateka wengi, na akawapa watu zawadi.” 9 Maandiko yanaposema, “Alipaa juu’ 10 Yeye aliyeshuka ndiye aliyepaa juu sana, kupita mbingu zote, ili apate kujaza vitu vyote. 11 Yeye ndiye aliyewapa watu vipawa, wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu; 12 wapate kuwatayarisha watu wa Mungu kwa kazi za huduma, kwa ajili ya kujenga kanisa, ambalo ni mwili wa Kristo. 13 Kazi hiyo itaende lea mpaka sote tuufikie umoja katika imani na katika kumjua Mwana wa Mungu; tupate kuwa watu waliokomaa kiroho kwa kufikia kiwango cha ukamilifu wote ulio ndani ya Kristo. 14 Hapo ndipo tutaacha kuwa tena kama watoto wadogo, wanaorushwarushwa huku na huko na kupeperushwa na kila upepo wa mafundisho na hila za watu wadan ganyifu. 15 Badala yake, tukiambiana ukweli kwa upendo, tutakua kwa kila hali, tufanane na Kristo ambaye ndiye kichwa. 16 Kutoka kwake, mwili wote ukiwa umeunganishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo vyake, hukua na kujengeka katika up endo, kila sehemu ikifanya kazi yake. Maisha Mapya Ndani Ya Kristo
17 Kwa hiyo nawaambia na kusisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa mataifa wasiomjua Mungu, ambao wanaon gozwa na mawazo yao yasiyofaa. 18 Watu hao akili zao zimetiwa giza wasiweze kuelewa; nao wametengwa mbali na uhai wa Mungu kwa sababu ya ujinga walionao na ugumu wa mioyo yao. 19 Kwa kuwa hawajali kuhusu mema na mabaya, wamekuwa sugu na kutawaliwa na uasherati, wakiwa na tamaa ya kutenda kila aina ya uchafu. 20 Lakini ninyi hamkujifunza hivyo kutoka kwa Kristo, 21 kama kweli mlisikia habari zake na kufundishwa kumhusu, kufuatana na kweli itokayo kwa Yesu. 22 Vueni maisha yenu ya zamani muweke kando hali yenu ya asili ambayo huharibiwa na tamaa potovu. 23 Nia zenu zifanywe upya 24 na mvae utu upya ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu. 25 Kwa hiyo, kila mmoja wenu aache kusema uongo, na amwambie ndugu yake ukweli, kwa maana sisi sote ni viungo vya mwili mmoja. 26 Mkikasirika, msitende dhambi; msikubali kukaa na hasira kutwa nzima 27 na kumpa she tani nafasi. 28 Mwizi asiibe tena, bali afanye kazi halali kwa mikono yake ili aweze kuwa na kitu cha kuwapa wenye kuhitaji msaada. 29 Msiruhusu maneno machafu yatoke vinywani mwenu, bali mazungumzo yenu yawe ya msaada katika kuwajenga wengine kufuatana na mahitaji yao, ili wale wanaowasikiliza wapate kufaidika. 30 Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi. 31 Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. 32 Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo. Watoto Wa Nuru
5 Kwa hiyo mfuateni Mungu kama watoto wapendwa. 2 Muishi maisha ya upendo kama Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu. 3 Lakini uasherati, uchafu wa aina zote na tamaa, wala yasitajwe miongoni mwenu, kwa maana mambo haya hayawastahili watakatifu wa Mungu. 4 Kusiwepo na mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuuzi au mzaha; mazungumzo ya namna hii hayafai. Badala yake mshukuruni Mungu. 5 Mjue hakika kwamba hakuna mwasherati wala mtu mwenye mawazo machafu, wala mwenye tamaa, yaani mwabudu sanamu, ambaye ataurithi Ufalme wa Kristo na wa Mungu. 6 Msikubali kudan ganywa na mtu ye yote kwa maneno matupu, kwa kuwa hasira ya Mungu huwaka kwa sababu ya mambo kama haya juu ya watu wote wasiomtii. 7 Kwa hiyo, msishirikiane nao. 8 Zamani ninyi pia mlikuwa gizani, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana; basi muishi kama watoto wa nuru. 9 Kwa maana tunda la nuru hupatikana katika kila lililo jema, lililo la haki na la kweli. 10 Jifunzeni mambo yanayom pendeza Bwana. 11 Msishiriki matendo ya giza yasiyofa a, bali yafichueni. 12 Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo wanayofanya kwa siri. 13 Lakini ikiwa jambo lo lote linawekwa katika nuru, huonekana, kwa maana ni nuru inayofanya vitu vionekane. 14 Ndio sababu husemwa, “Amka wewe uliyelala, ufufuke kutoka kwa wafu, na Kristo atakuangazia.” 15 Kwa hiyo muwe waangalifu jinsi mnavyoishi; msiishi kama watu wasio na hekima, bali kama watu wenye hekima, 16 mkitumia vizuri muda mlio nao, kwa maana hizi ni nyakati za uovu. 17 Kwa hiyo msiwe wajinga, bali muelewe yaliyo mapenzi ya Mungu. 18 Pia msilewe divai, kwa sababu huo ni upotovu, bali mjazwe Roho. 19 Zungumzeni ninyi kwa ninyi kwa zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia Mungu mioyoni mwenu kwa sauti tamu. 20 Wakati wote na kwa kila kitu mshukuruni Mungu Baba katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo. 21 Kila mmoja wenu ajinyenyekeze kwa mwenzake kwa sababu ya upendo mlio nao kwa Kristo. 22 Wake, watiini waume zenu kama mnavyomtii Bwana. 23 Kwa maana mume ni kichwa cha mke kama vile Kristo alivyo kichwa cha kanisa, ambalo ni mwili wake, naye mwe nyewe ni Mwokozi wa kanisa. 24 Basi, kama vile Kanisa linavyom tii Kristo, vivyo hivyo na wake pia wanapaswa kuwatii waume zao kwa kila jambo. 25 Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili 26 alitakase. Alifanya hivyo kwa kuliosha kwa maji na kwa neno lake 27 ili ajipatie kanisa linalong’aa, lisilo na doa wala kunjamano wala kitu kingine cho chote kama hicho; liwe takatifu na bila kasoro. 28 Vivyo hivyo waume wawapende wake zao kama miili yao. Anayempenda mkewe anajipenda mwenyewe. 29 Hakuna mtu anayeuchukia mwili wake mwenyewe, bali huulisha na kuutunza vizuri, kama Kristo anavyolitunza kanisa lake. 30 Sisi tu viungo vya mwili wake. 31 “Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataungana na mkewe, na hawa wawili wata kuwa mwili mmoja.” 32 Hili ni fumbo gumu kueleweka, nami nasema kuwa ni kielelezo kuhusu Kristo na kanisa. 33 Hata hivyo kila mmoja wenu ampende mkewe kama anavyoipenda nafsi yake; na mke naye ahakikishe anamheshimu mumewe. Watoto Na Wazazi
6 Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana kufanya hivyo ni vizuri. 2 “Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, 3 “upate baraka na uishi siku nyingi duniani.” 4 Akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana. Watumwa Na Mabwana
5 Watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani, kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnamtii Kristo. 6 Watiini, sio tu wakati wakiwaona ili mpate sifa, bali mtumike kama watumishi wa Kristo, mkifanya mapenzi ya Mungu kwa moyo. 7 Toeni huduma yenu kwa moyo wote, kama vile mnamtumikia Bwana na sio watu. 8 Mkumbuke kuwa Bwana atampa kila mmoja tuzo kutegemeana na wema aliotenda, kama yeye ni mtumwa au ni mtu huru. 9 Nanyi mabwana watendeeni watumwa wenu kwa jinsi hiyo hiyo. Msiwatishe, kwa kuwa mnajua ya kwamba yeye aliye Bwana wenu na wao yuko mbinguni, naye hana upendeleo.
10 Hatimaye, muwe imara katika Bwana na katika nguvu zake kuu. 11 Vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama na kupin gana na hila zote za shetani. 12 Kwa maana hatupambani na bina damu, bali tunapambana na tawala na mamlaka na nguvu za ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 13 Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu ili mpate kusimama imara siku ya uovu itakapokuja; na mkishafanya yote, mtakuwa bado mme simama. 14 Kwa hiyo simameni imara mkisha jifunga na kweli kama mkanda kiunoni na haki kama kinga ya kifuani; 15 na kuvaa Injili ya amani kama viatu miguuni, ili muweze kusimama barabara. 16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. 17 Vaeni wokovu kama kofia ya vita vichwani na chukueni upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu. 18 Ombeni wakati wote katika Roho, katika sala zote na maombi. Kwa hiyo muwe macho na siku zote endeleeni kuwaombea watu wote wa Mungu. 19 Niombeeni mimi pia, ili kila ninapozungumza, nipewe maneno ya kusema, niweze kutangaza siri ya Injili pasipo woga. 20 Mimi ni balozi kifun goni kwa ajili ya Injili hii. Kwa hiyo niombeeni niihubiri Injili kwa ujasiri kama inipasavyo. 21 Ndugu mpendwa Tikiko, ambaye ni mtumishi mwaminifu wa Bwana, atawaelezeni kila kitu ili mjue habari zangu na mfahamu ninachofanya. 22 Ninamtuma kwenu kwa kusudi hili, mpate habari zetu naye awafariji. 23 Nawatakia ndugu wote amani na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo.
Copyright © 1989 by Biblica