Beginning
1 Kutoka kwa Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wathes alonike mlio wa Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. 2 Tuna watakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.
Sala Na Shukrani
3 Hatuna budi kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu wapendwa; na ndivyo inavyostahili kwa sababu imani yenu inaongezeka zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu kwa mwen zake unazidi kuongezeka. 4 Ndio maana sisi tunajivuna kwa ajili yenu miongoni mwa makanisa ya Mungu. Tunajivuna juu ya uvumilivu wenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazopata.
5 Haya yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki na kwa sababu hiyo ninyi mtastahili kupata Ufalme wa Mungu ambao mnateswa kwa ajili yake. 6 Mungu ni wa haki: atawalipa kwa mateso wale wanaowatesa ninyi 7 na kuwapeni ninyi mnaoteseka nafuu pamoja na sisi pia. Haya yatatokea wakati Bwana Yesu atakapodhi hirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. 8 Atawahukumu wale wasiomjua Mungu, wasioitii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. 9 Wataadhibiwa kwa kuangamizwa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake, 10 siku ile atakapokuja kutukuzwa kwa ajili ya watakatifu wake na kustaajabiwa na watu wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa mion goni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.
11 Kwa sababu hii tunawaombeeni bila kukoma, kwamba Mungu awahesabu kuwa mnastahili maisha aliyowaitia na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila nia njema mliyo nayo na kila tendo linalotokana na imani yenu. 12 Tunaomba hivi ili jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe kwa ajili yenu nanyi mtukuzwe kwa ajili yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo.
Kuja Kwa Bwana Na Kudhihirishwa Kwa Mwovu
2 Basi, kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu mbele zake, tunawasihi, ndugu wapendwa, 2 msifadhaike au kuwa na wasiwasi kutokana na utabiri fulani, au taarifa au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, kusema eti kwamba siku ya Bwana imekwisha kuja. 3 Mtu asiwadanganye kwa namna yo yote maana siku hiyo haitakuja kabla ya uasi kutokea kwanza na yule mwasi adhi hirishwe, yule ambaye mwisho wake ni kuangamizwa kabisa. 4 Yeye anapinga kila ambacho watu hukiita mungu au cho chote kinachoabu diwa; naye hujiweka hata katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
5 Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambieni mambo haya? 6 Na mnajua kinachomzuia sasa, ili adhihirishwe wakati ufaao. 7 Maana ile nguvu ya siri ya uasi imekwisha anza kufanya kazi; lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa. 8 Hapo ndipo yule mwovu ataonekana, na Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa ufahari wa kuja kwake. 9 Kuja kwa yule mwovu kutafuata kazi ya shetani ambayo itaonyeshwa katika aina zote za ishara bandia na maajabu ya uongo; 10 na katika kila aina ya uovu unaotumiwa kuwadanganya wale wanaoangamia. Wanaangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. 11 Ndio maana Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu ili waendelee kuu amini uongo; 12 na ili wote wasioamini kweli bali hufurahia uovu, wahukumiwe.
Simameni Imara
13 Lakini tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu, ndugu mpendwao na Bwana, maana Mungu aliwachagueni tangu mwanzo ili mwokolewe kwa kutakaswa na Roho na kwa kuiamini kweli. 14 Mungu amewaitieni jambo hili kwa njia ya mahubiri yetu ya Habari Njema, ili muweze kushiriki katika utukufu wa Bwana Yesu Kristo. 15 Kwa hiyo ndugu wapendwa, simameni imara na mshike sana yale mafundisho tuliyowapeni katika mahubiri yetu na kwa barua zetu.
16 Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, ali yetupenda akatupatia faraja ya milele na tumaini jema kwa neema, 17 na awafariji mioyoni mwenu na kuwaimarisheni katika kila jambo jema mnalosema au kutenda.
Ombi Kuhusu Maombezi
3 Hatimaye, ndugu wapendwa, tuombeeni ili neno la Mungu lienee upesi na kukubaliwa kama ilivyokuwa kwenu. 2 Ombeni pia kwamba tuokolewe kutokana na watu waovu na wasio na haki, kwa maana si watu wote wanaamini. 3 Lakini Bwana ni mwaminifu. Ata waimarisheni na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4 Nasi tuna tumaini kubwa kwa Bwana juu yenu, kwamba mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5 Bwana aielekeze mioyo yenu kwenye upendo wa Mungu na katika ustahimilivu wa Kristo.
Onyo Kuhusu Uvivu
6 Ndugu wapendwa, katika jina la Bwana Yesu Kristo, tuna waagiza mjitenge na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapeni. 7 Maana ninyi wenyewe mnafa hamu jinsi mnavyopaswa kuiga mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa nanyi 8 wala hatukula chakula cha mtu ye yote pasipo kulipa. Bali tulifanya kazi kwa juhudi usiku na mchana ili tusimlemee mtu ye yote kati yenu. 9 Hatukufanya hivi kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada wenu, bali tulitaka tuwape mfano wa kuiga. 10 Maana tulipokuwa pamoja nanyi tuliwapa amri hii: “Ikiwa mtu hatafanya kazi, basi asile.”
11 Tumesikia kwamba baadhi yenu ni wavivu, hawana shughuli maalumu isipokuwa kusengenya wenzao. 12 Sasa tunawaagiza na kuwaonya watu hao katika jina la Bwana Yesu Kristo, wafanye kazi ili wajipatie chakula wanachokula. 13 Ndugu wapendwa, ninyi msi choke kutenda mema.
14 Ikiwa mtu atakataa kutii maagizo tunayotoa katika barua hii, mwangalieni vema mtu huyo, mjitenge naye, ili apate kuona aibu. 15 Lakini msimhesabu kama adui bali mkanyeni kama ndugu.
Salamu Za Mwisho
16 Sasa, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa njia zote. Bwana na awe nanyi nyote.
17 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwe nyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote.
Copyright © 1989 by Biblica