Old/New Testament
27 Siku ya kumi na nne, mnamo saa sita za usiku, tulipokuwa bado tunasukumwa na upepo katika bahari ya Adria, mabaharia wali hisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. 28 Kwa hiyo wakapima kina cha bahari wakakuta kilikuwa mita thelathini na tano hivi, na baada ya kitambo kidogo wakapima tena wakapata kina cha mita ishirini na sita hivi. 29 Wakaogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, kwa hiyo wakashusha nanga nne nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. 30 Mabaharia walikuwa wanataka kutoroka kutoka mle melini, wakashusha mashua baharini wakidanga nya kuwa walikuwa wanakwenda kuweka nanga upande wa mbele ya meli. Ndipo 31 Paulo akawaambia wale maaskari na maofisa wao, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokolewa.” 32 Basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua kwenye meli wakaiacha mashua ichukuliwe baharini. 33 Mapambazuko yalipokaribia, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi bila kula cho chote. 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula kwa maana mnakihi taji ili muweze kuishi. Hakuna mmoja wenu atakayepoteza hata unywele mmoja kichwani mwake.” 35 Baada ya maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. 36 Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chak ula. 37 Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu mia mbili na sabini na sita. 38 Baada ya wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.
39 Kulipokucha, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga ambako walitaka waielekeze meli kama ingewezekana, ili wafike pwani. 40 Kwa hiyo wakatupa nanga zote baharini, wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli, na kutweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani. 41 Lakini ile meli ikagonga mwamba ikakwama kwenye mchanga na upande wa mbele wa meli uka banwa kwenye mwamba wala usingeweza kuondolewa tena. Na upande wa nyuma ulivunjika vipande kwa nguvu ya yale mawimbi. 42 Wale askari walikuwa wamepanga kuwaua wafungwa wote ili wasije wakaogelea hadi pwani na kutoroka. 43 Lakini yule Ofisa wa maas kari alitaka kumwokoa Paulo, kwa hiyo akawazuia wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, na waogelee kuelekea pwani; 44 na wengine wajishikize kwenye vipande vya meli waelee navyo. Kwa jinsi hii, watu wote waliokolewa wakafika nchi kavu.
Copyright © 1989 by Biblica