Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 20:17-38

Paulo Anawaaga Wazee Wa Kanisa La Efeso

17 Paulo akiwa Mileto, alituma ujumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa wakutane naye. 18 Walipofika aliwaambia, “Ninyi mnajua jinsi nilivyoishi nanyi tangu siku ya kwanza nilipofika Asia. 19 Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu na machozi na kwa mateso yaliyotokana na njama za Wayahudi. 20 Mnajua jinsi ambavyo sikusita kuwaambia cho chote ambacho kingekuwa cha faida kwenu, na jinsi nilivyofundisha hadharani na nyumba kwa nyumba 21 nikiwashuhudia Wayahudi na Wagiriki juu ya kutubu dhambi kwa Mungu na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. 22 Na sasa nimevutwa na Roho niende Yerusalemu na sijui mambo yatakayonipata huko. 23 Ila katika kila mji niliopitia, Roho Mtakatifu amenifunulia kwamba mbele yangu kifungo na mateso vinaningoja. 24 Lakini nay ahesabu maisha yangu kuwa si kitu cha thamani kwangu, ili mradi niweze kukamilisha wito na kazi niliyopewa na Bwana Yesu; kazi ya kuwashuhudia watu kuhusu Habari Njema ya neema ya Mungu. 25 Na sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja wenu, ninyi ambao kati yenu nimekuwa nikihubiri juu ya Ufalme wa Mungu, atakayeniona tena. 26 Kwa hiyo nawashuhudia wazi leo hii kwamba sina lawama juu ya mtu ye yote kati yenu, 27 kwa sababu sikuacha kuwatangazia mpango kamili wa Mungu. 28 Jilindeni nafsi zenu, na mlinde kundi lote la kondoo ambalo Roho Mtakatifu ameliweka chini ya uongozi wenu; mtunze kanisa la Mungu ambalo amelinunua kwa damu ya Mwa nae. 29 Najua kwamba nikishaondoka, mbwa mwitu wakali watakuja kati yenu nao hawatakuwa na huruma yo yote juu ya kundi lenu. 30 Na hata kati yenu ninyi patatokea watu watakaosema maneno ya kupotosha ili wawavute baadhi ya wanafunzi wawafuate. 31 Kwa hiyo muwe macho; mkumbuke jinsi nilivyomwonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu. 32 Na sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake ambalo linaweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi pamoja na wote ambao wameta kaswa. 33 Sikutamani fedha au dhahabu au nguo za mtu ye yote. 34 Ninyi wenyewe mnajua kwamba kwa mikono yangu nimefanya kazi nikapata mahitaji yangu na ya wenzangu. 35 Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa kufanya kazi kwa bidii mtaweza kuwa saidia walio dhaifu, mkikumbuka maneno aliyosema Bwana Yesu kwamba, ‘Kuna baraka kubwa zaidi katika kutoa kuliko kupokea.”’

36 Paulo alipomaliza kusema haya alipiga magoti akaomba pamoja nao wote. 37 Na wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kum busu, 38 wakihuzunika kwa sababu ya maneno aliyowaambia kwamba hawatamwona tena. Wakamsindikiza wakamfikisha kwenye meli.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica