Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 13:1-25

Barnaba Na Sauli Wachaguliwa Kwa Kazi Maalumu

13 Katika Kanisa la Antiokia Walikuwako manabii na waalimu wafuatao: Barnaba, Simeoni aitwaye mtu mweusi, Lukio kutoka Kirene, Manaeni aliyekuwa nduguye mfalme Herode, na Sauli. Wal ipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi maalumu niliyowaitia.” Kwa hiyo baada ya kufunga na kuomba, waliwawekea mikono Sauli na Barnaba wakawaaga.

Barnaba Na Sauli Waenda Kipro

Barnaba na Sauli wakaongozwa na Roho Mtakatifu wakaenda mpaka Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro . Nao walipowasili katika mji wa Salami, walihubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Walikuwa wameongozana na Yohana Marko kama msaidizi wao.

Bar-Yesu Alaaniwa Na Mitume

Baada ya kuhubiri sehemu zote za kisiwa cha Kipro walifika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, aitwaye Bar-Yesu. Bar-Yesu alikuwa rafiki wa liwali ait waye Sergio Paulo, mtu mwenye hekima. Liwali huyu alituma Sauli na Barnaba waletwe kwake kwa sababu alitaka kusikia Neno la Mungu. Lakini yule mchawi ambaye jina lake kwa Kigiriki ni Elima, alijaribu kuwapinga Barnaba na Sauli na kumshawishi yule liwali asiwasikilize. Ndipo Sauli ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule mchawi, 10 akamwambia, “Wewe mwana wa Shetani! Wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa hila, na uovu. Je, utaacha lini kujaribu kugeuza kweli ya Bwana kuwa uongo? 11 Na sasa tazama mkono wa Bwana uko juu yako kukuadhibu, nawe utakuwa kipofu; hutaona kwa muda.” Na mara ukungu na giza likafunika macho ya Elima akaanza kutanga-tanga akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. 12 Yule liwali alipoona mambo haya, akaamini, kwa maana alistaajabishwa na mafundisho ya Bwana.

13 Basi Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo mpaka Perge huko Pamfilia. Yohana Marko akawaacha huko akarejea Yerusalemu. 14 Lakini Barnaba na Paulo wakaendelea hadi Antiokia, mji ulioko katika jimbo la Pisidia. Na siku ya sabato waliingia ndani ya sinagogi wakaketi . 15 Baada ya kusoma kutoka katika vitabu vya sheria za Musa na Maandiko ya manabii, viongozi wa lile sinagogi waliwatumia ujumbe pale walipokaa wakisema, “Ndugu, kama mna neno la mafundisho kwetu, njooni mkaliseme watu walisikie. 16 Paulo akasimama akawapungia mkono akasema, “Watu wa Israeli, na ninyi wote mnaomcha Mungu, sikilizeni. 17 Mungu wa taifa la Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kuwa taifa kubwa wakati walipoishi katika nchi ya Misri na akawatoa katika utumwa wa Misri kwa nguvu za ajabu. 18 Kwa muda wa miaka arobaini aliwavu milia walipokuwa jangwani. 19 Na baada ya kuwaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao kwa muda wa miaka mia nne na hamsini. 20 Kisha akawapa Waamuzi wakatawala mpaka wakati wa nabii Samweli. 21 Hatimaye wakataka wawe na mfalme. Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, wa kabila la Benjamini, akawatawala kwa miaka arobaini. 22 Mungu akamwondoa Sauli katika ufalme, akamta waza Daudi mwana wa Yese, akamshuhudia akisema, ‘Nimempata Daudi mwana wa Yese, ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Yeye atafanya mapenzi yangu .’ 23 Katika uzao wa Daudi, Mungu amewaletea Wais raeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi. 24 Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli. 25 Kabla Yohana Mbatizaji hajamaliza kazi yake, alisema, ‘Mna nidhania mimi ni nani? Mimi siye yule mnayemtazamia. Lakini anayekuja baada yangu mimi sistahili hata kufungua viatu vyake.’

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica