Old/New Testament
Petro Nyumbani Kwa Kornelio
24 Kesho yake wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwan goja pamoja na ndugu zake na marafiki wa karibu ambao alikuwa amewaalika. 25 Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akapiga magoti. 26 Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama! Mimi ni mwanadamu tu.” 27 Petro alipokuwa akizungumza naye aliingia ndani ambapo alikuta watu wengi wamekusanyika. 28 Petro akawaambia, “Mnajua kwamba sheria ya Wayahudi hairu husu Myahudi kuwatembelea au kuchangamana na watu wa mataifa men gine kama hivi nifanyavyo. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwone mtu ye yote kuwa mchafu au asiyefaa. 29 Ndiyo sababu ulipotuma nije sikusita. Kwa hiyo naomba unieleze kwa nini ume niita.” 30 Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa mchana. Mara akatokea mtu aliyevaa nguo za kung’ara akasimama mbele yangu. 31 Akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na Mungu, naye amekumbuka msaada wako kwa maskini. 32 Basi tuma watu waende Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. Yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko sehemu za pwani.’ 33 Ndio sababu nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vizuri kuja. Basi sasa tuko hapa wote mbele ya Mungu kuyasikiliza yote ambayo Mungu amekuamuru kutuambia.”
Hotuba Ya Petro
34 “Ndipo Petro alianza kwa kusema, “Sasa naamini ya kuwa Mungu hana upendeleo. 35 Yeye huwakubali watu wa kila taifa wam chao na kutenda haki. 36 Huu ndio ujumbe ambao Mungu aliwapele kea watu wa Israeli, kuhusu Habari Njema za amani kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wa wote. 37 Ninyi bila shaka mnafa hamu mambo yaliyotokea sehemu zote za Yudea, kuanzia Galilaya tangu wakati wa mahubiri ya Yohana Mbatizaji. 38 Mnafahamu jinsi Mungu alivyompa Yesu wa Nazareti Roho Mtakatifu na uwezo, na jinsi alivyozunguka kila mahali akifanya mema na kuponya wote waliokuwa wakiteswa na nguvu za shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyofanya katika nchi ya Wayahudi na Yerusalemu. Walimwua kwa kumtundika msalabani. 40 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu. 41 Hakuonekana kwa watu wote, lakini alionekana kwa mashahidi ambao Mungu aliwachagua, yaani sisi ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake. 42 Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote, na kushuhudia kwamba yeye ndiye aliyechaguliwa na Mungu kuwahukumu walio hai na wafu. 43 Manabii wote walishuhudia juu yake, kwamba kila mtu amwami niye atasamehewa dhambi katika jina lake.”
Mataifa Wapokea Roho Mtakatifu
44 Petro alipokuwa akisema maneno hayo, Roho Mtakatifu ali washukia wote waliokuwa wakisikiliza. 45 Wale Wayahudi waamini waliokuwa wamekuja na Petro walishangaa sana kuona kuwa Mungu aliwapa watu wa mataifa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46 Kwa kuwa waliwasikia wakisema kwa lugha mpya na kumtukuza Mungu kwa ukuu wake. Ndipo Petro akasema, 47 “Je, kuna mtu anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.” 48 Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.
Copyright © 1989 by Biblica