Old/New Testament
Paulo Ahubiri Thesalonike
17 Walisafiri kupitia Amfipoli na Apolonia wakafika Thesalo nike, ambako kulikuwa na sinagogi la Wayahudi. 2 Paulo aliingia ndani ya sinagogi kama ilivyokuwa kawaida yake, na kwa muda wa majuma matatu akawa akihojiana na Wayahudi akitumia Maandiko 3 kuwaonyesha wazi kwamba ilikuwa ni lazima Kristo ateswe na afu fuke kutoka kwa wafu, akamalizia kwa kusema, “Huyu Yesu ambaye nawaambia habari zake, ndiye Kristo.” 4 Baadhi yao wakakubaliana nao, wakajiunga na Paulo na Sila. Pia umati mkubwa wa Wagiriki waliomcha Mungu, na baadhi ya wanawake viongozi wakaungana nao. 5 Lakini Wayahudi wengi waliwaonea Paulo na Sila wivu, waka chochea baadhi ya wazururaji waovu waanzishe fujo mji mzima; kisha wakashambulia nyumba ya Yasoni ambamo Paulo na Sila wali kuwa wakikaa, ili wawatoe nje. 6 Walipokuta hawako huko, wakawa kamata Yasoni na baadhi ya ndugu waamini wakawaleta mbele ya viongozi wa mji wakipiga kelele: “Hawa watu ambao wamepindua dunia nzima wamefika huku 7 na huyu Yasoni amewakaribisha. Wao wanavunja sheria ya Kaisari kwa kusema eti kuna mfalme mwingine aitwaye Yesu.” 8 Mashtaka haya ya Wayahudi yaliwafadhaisha watu wote pamoja na wale viongozi wa mji. 9 Kwa hiyo wakataka dhamana kutoka kwa Yasoni na waamini wenzake kabla ya kuwaachilia waende zao.
10 Giza lilipoingia, wale ndugu waamini waliwatoa Paulo na Sila wakaondoka kwenda Beroya, na walipowasili wakaingia katika Sinagogi la Wayahudi. 11 Watu wa Beroya walikuwa waungwana zaidi kuliko watu wa Thesalonike. Walisikiliza neno la Mungu kwa hamu wakachambua Maandiko kila siku ili waone kama waliyokuwa wakiam biwa na Paulo ni kweli. 12 Wengi wao waliamini, ikiwa ni pamoja na wanawake maarufu wa Kigiriki na wanaume wengi. 13 Lakini wale Wayahudi wa Thesalonike waliposikia kuwa Paulo anahubiri neno la Mungu huko Beroya, walikuja wakaanza kuwashawishi watu na kuwa chochea waanzishe vurugu. 14 Na ndugu wa Beroya wakafanya haraka wakamsafirisha Paulo kuelekea bandarini , lakini Sila na Timotheo walibaki Beroya. 15 Wale waliomsindikiza Paulo walienda naye mpaka Athene. Ndipo wakarudi Beroya wakiwa na maagizo kutoka kwa Paulo kwamba, Sila na Timotheo wamfuate upesi iwezekanavyo.
Copyright © 1989 by Biblica