Old/New Testament
16 Basi kumbe binamu yake Paulo alisikia kuhusu mpango huu. Akaenda katika ngome ya jeshi akamweleza Paulo mambo haya. 17 Paulo akamwita mmoja wa wale maaskari akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwa jemadari, ana neno la kumwambia.” 18 Yule askari akamchukua yule kijana mpaka kwa jemadari akamwambia, “Yule mfungwa Paulo aliniita akaniambia nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukuambia.” 19 Yule jemadari akamchukua yule kijana kando akamwuliza, “Unataka kuniambia nini?” 20 Naye akasema, “Wayahudi wameku baliana wakuombe kesho umpeleke Paulo kwenye Baraza lao kwa kisingizio kwamba wanataka kuchunguza kesi yake kwa uangalifu zaidi. 21 Lakini usikubali ombi lao kwa maana zaidi ya watu aro baini wamekula njama kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamwue Paulo nao wamejiweka tayari kumvizia ukishakubali ombi lao.” 22 Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende, akamwonya akisema, “Usimwambie mtu ye yote kwamba umenieleza habari hizi.”
Paulo Apelekwa Kaisaria Kwa Gavana Feliksi
23 Yule jemadari akawaita maaskari wawili akawaambia, “Tay arisheni askari mia mbili watakaokwenda Kaisaria pamoja na askari wa farasi sabini, na askari wa mikuki mia mbili; nanyi muwe tay ari kuondoka leo saa tatu za usiku. 24 Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mumpeleke salama mpaka kwa gavana Feliksi.” 25 Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo: 26 “Mimi Klaudio Lisia, nakuandikia wewe gavana mtukufu Feliksi. Salamu. 27 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakawa kar ibu kumwua, ndipo mimi nilipofika na askari wangu nikamwokoa kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raia wa Kirumi. 28 Nami nikampeleka mbele ya baraza lao ili nipate kujua kosa alilofanya. 29 Ndipo nikagundua ya kuwa alikuwa anashtakiwa kuhusu sheria yao, lakini hakuwa na kosa la kustahili kifo au kifungo. 30 Lakini nilipata habari kwamba kuna mpango wa kumwua nikaamua nimpeleke kwako mara moja, nikawaamuru washitaki wake walete mashtaka yao kwako.” 31 Basi wale askari wakamchukua Paulo usiku wakampeleka mpaka Antipatri kama walivyoamriwa. 32 Kesho yake wakarudi kituoni wakawaacha wale askari wa mikuki waendelee na safari pamoja na Paulo. 33 Walipofika Kaisaria walimpa Liwali ile barua na pia wakamkabidhi Paulo kwake. 34 Alipokwisha soma ile barua, alimwuliza Paulo ametoka jimbo gani. Alipofahamishwa kuwa anatoka Kilikia 35 alisema, “Nitasikiliza kesi yako mara tu washtaki wako watakapofika.” Akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi katika ikulu ya Herode.
Copyright © 1989 by Biblica