Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Job for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 16:1-21

Paulo Amchagua Timotheo

16 Paulo alisafiri mpaka Derbe na Listra ambako mwanafunzi mmoja aitwaye Timotheo aliishi. Mama yake Timotheo alikuwa Myahudi naye alikuwa mwamini; baba yake alikuwa Mgiriki. Timotheo alikuwa mtu mwenye sifa nzuri kwa ndugu wote wa huko Listra na Ikonio. Paulo alitaka amchukue Timotheo awe akisafiri naye, kwa hiyo akamtahiri ili asiwe kikwazo kwa Wayahudi wa eneo hilo ambao walijua ya kuwa baba yake Timotheo alikuwa Mgiriki. Walipokuwa wakipita katika miji mbali mbali waliwasilisha maamuzi ya baraza la mitume na wazee wa kanisa huko Yerusalemu ili wayazingatie. Kwa hiyo makanisa yakazidi kuimarika katika imani na idadi ya waamini ikawa inaongezeka kila siku.

Paulo Anaongozwa Kwenda Makedonia

Walisafiri kupitia wilaya ya Firigia na Galatia, kwa sababu Roho Mtakatifu aliwazuia wasihubiri neno sehemu za Asia. Wali pofika kwenye mpaka wa Misia walijaribu kuingia wilaya ya Bithi nia lakini Roho wa Yesu hakuwaruhusu. Kwa hiyo wakaendelea na safari kupitia Misia, wakafika Troa. Usiku huo Paulo akaona katika ndoto, mtu wa Makedonia amesimama akimsihi, “Njoo Makedo nia ukatusaidie.” 10 Mara baada ya Paulo kuona maono haya, tulijiandaa kuondoka kwenda Makedonia kwa sababu tuliona kuwa Mungu ametuita kuhubiri Habari Njema kwa watu wa huko. 11 Tuliondoka Troa kwa meli tukaenda moja kwa moja mpaka Samo trake, na kesho yake tukafika Neapoli. 12 Kutoka huko tukaende lea na safari hadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia ambao ni koloni la Kirumi. 13 Tulikaa Filipi kwa siku chache na siku ya sabato tukaenda nje ya mji kando ya mto, mahali ambapo tulidhani pange faa kwa maombi. Tukakaa chini tukaongea na baadhi ya wanawake waliokuja pale mtoni. 14 Mmoja wa wanawake waliotusikiliza aliitwa Lidia, mwenyeji wa mji wa Thiatira na mfanya biashara wa nguo za zambarau. Yeye alimpenda Mungu na Bwana akaufungua moyo wake akapokea mahubiri ya Paulo. 15 Basi alipokwisha kubatizwa yeye na jamaa yake, alitusihi akisema, “Kama mmenipokea kweli kama mwamini, tafadhali njooni mkae nyumbani kwangu.” Akatushaw ishi twende naye.

Paulo Na Sila Wafungwa Gerezani

16 Siku moja tulipokuwa tukienda mahali pa sala tulikutana na msichana mmoja mtumwa aliyekuwa na pepo wa kutabiri mambo yaj ayo. Alikuwa amewapatia mabwana wake faida kubwa kwa kutumia uwezo wa kutabiria watu mambo yajayo. 17 Basi alimfuata Paulo na sisi akipiga kelele, “Watu hawa ni watumishi wa Mungu aliye Juu kuliko wote. Wao wanatangaza kwenu njia ya wokovu.” 18 Na aliendelea kusema maneno haya kwa siku nyingi. Lakini Paulo aliudhika, akageuka na kumwambia yule pepo, “Ninakuamuru katika jina la Yesu Kristo, umtoke!” Yule pepo akamtoka wakati ule ule. 19 Basi mabwana wa yule msichana mtumwa walipoona kuwa matumaini yao ya kuendelea kujipatia fedha yametoweka, wakawakamata Paulo na Sila wakawapeleka sokoni mbele ya viongozi wa mji. 20 Waka washtaki kwa mahakimu wakisema, “ Hawa watu ni Wayahudi nao wan aleta fujo mjini kwetu. 21 Wanafundisha desturi ambazo si halali kwetu kama raia wa Kirumi kuzikubali au kuzitimiza.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica