Old/New Testament
Paulo Ahubiri Huko Athene
16 Paulo alipokuwa akiwangojea wenzake huko Athene alisikit ishwa sana kuona jinsi mji ulivyojaa miungu ya sanamu. 17 Kwa hiyo akawa akienda katika sinagogi kujadiliana na Wayahudi na Wagiriki waliomcha Mungu na katika mahali pa soko ambako aliongea na watu aliokutana nao. 18 Huko sokoni alikutana na vikundi viwili vya wanafalsafa waitwao Waepikureo na Wastoiko. Baadhi yao wakamdhihaki wakisema, “Huyu mpayukaji asiyejua kitu anajaribu kusema nini?” Wengine wakasema, “Anaelekea kuwa mhubiri wa miungu wageni.” Walisema hivi kwa sababu Paulo alikuwa akihubiri juu ya Yesu na ufufuo. 19 Wakamkamata wakampeleka kwenye baraza la Areopago wakamwambia, “Tungependa kufahamu haya mafundisho mapya unayotangaza. 20 Mambo tunayosikia kuwa unafundisha ni mageni kwetu nasi tungependa kuelewa maana yake.” 21 Waathene na hata wageni walikuwa na tabia ya kutumia wakati wao wote katika mazungumzo ya mambo yo yote ambayo yanaonekana kuwa mageni au mapya.
Hotuba Ya Paulo Kwenye Areopago
22 Kwa hiyo Paulo alisimama kati kati ya Areopago akasema, “Ndugu wa Athene! Nimeona katika kila jambo kuwa ninyi ni watu wa dini hasa. 23 Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini niliona sehemu nyingi za kuabudia. Niliona pia madhabahu moja iliyoan dikwa, ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Huyo Mungu mnayemwabudu bila kumfahamu, ndiye ninayemtangaza kwenu. 24 Mungu aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo, ambaye pia ni Bwana wa mbingu na nchi, haishi katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu. 25 Wala hahu dumiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji cho chote; kwa sababu yeye ndiye anayewapa watu wote uhai na pumzi na kila kitu. 26 Yeye aliumba mataifa yote ya wanadamu waishi juu ya nchi kutokana na mtu mmoja. Pia amepanga muda wa maisha ya watu wote, akaweka na mipaka ya mahali watakapoishi 27 ili wamtafute Mungu na wamfahamu. Lakini Yeye hayuko mbali nasi kwa maana 28 ‘Tunaishi na kuenenda na kuwa na uhai ndani yake,’ na kama mtunga mashairi wenu alivyosema, ‘Sisi ni uzao wa Mungu.’ 29 Kwa kuwa sisi ni wa uzao wa Mungu hatupaswi kudhani kuwa yeye ni kama sanamu ya dhahabu au fedha au jiwe iliyotengenezwa kwa akili na ufundi wa mwanadamu. 30 Mungu alisamehe ujinga huo wa zamani, lakini sasa anaamuru watu wote watubu, waachane na miungu ya sanamu. 31 Kwa kuwa amepanga siku ambayo atahukumu ulimwengu kwa haki akimtumia mtu aliyemchagua, ambaye amemhakikisha kwa watu wote kwa kumfufua kutoka kwa wafu.” 32 Waathene waliposikia juu ya ufufuo wa wafu, baadhi yao wakamdhihaki; lakini wengine wal isema, “Tutataka kusikia tena juu ya habari hii.” 33 Kwa hiyo Paulo akaondoka. 34 Lakini baadhi ya watu walimfuata Paulo wakaamini. Kati yao alikuwepo Dionisio, Mwareopago, na mwanamke mmoja aliyeitwa Damari na wengine.
Copyright © 1989 by Biblica