Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 21:1-17

Paulo Aenda Yerusalemu

21 Tulipokwisha agana nao tuliondoka tukasafiri moja kwa moja, mpaka Kosi, na siku ya pili yake tukafika Rodo, na kutoka huko tukaenda Patara. Hapo tukapata meli iliyokuwa ikielekea Foinike tukaingia ndani tukasafiri nayo. Tulipokaribia kisiwa cha Kipro, tulikizunguka upande wa kushoto, tukasafiri mpaka Siria, tukatia nanga katika bandari ya Tiro ambapo meli yetu ili kuwa ipakue shehena yake. Tukawatafuta waamini wa huko, tukakaa nao kwa siku saba. Wale waamini wakiwa wameongozwa na Roho walim wambia Paulo asiende Yerusalemu. Muda wa kukaa nao ulipokwisha, tuliendelea na safari yetu na wale ndugu waamini pamoja na wake zao na watoto wao walitusindikiza hadi nje ya mji. Wote tulipiga magoti pale pwani tukaomba, kisha tukaagana.

Ndipo tukaingia ndani ya meli na wale ndugu wakarudi mak wao. Tuliendelea na safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawasalimu waamini wa huko na tukakaa nao kwa siku moja. Kesho yake tuliondoka tukafika Kaisaria. Huko tukaenda nyumbani kwa mwinjilisti mmoja jina lake Filipo ambaye alikuwa kati ya wale watu saba waliochaguliwa kule Yerusalemu, tukakaa kwake. Filipo alikuwa na binti wanne ambao walikuwa bado hawajaolewa nao walikuwa na karama ya unabii. 10 Wakati tulipokuwa huko kwa siku kadhaa, alifika nabii mmoja aitwaye Agabo kutoka Yudea. 11 Alikuja kutuona akachukua mshipi wa Paulo, akautumia kufunga mikono yake mwenyewe na miguu yake akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mwe nye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa mataifa .”’ 12 Tulipo sikia maneno haya sisi na ndugu wengine tulimwomba Paulo asiende Yerusalemu. 13 Lakini Paulo alijibu, “Kwa nini mnanivunja moyo kwa machozi yenu? Mimi niko tayari kufungwa na hata kufa huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.” 14 Na kwa kuwa hatukuweza kumshawishi asiende, tuliacha kumsihi tukamwambia, “Mapenzi ya Bwana na yatendeke.”

15 Baadaye tulijiandaa tukaondoka kwenda Yerusalemu. 16 Baadhi ya waamini kutoka Kaisaria waliongozana nasi, wakat upeleka nyumbani kwa Mnasoni, mtu wa Kipro, mmoja wa waamini wa zamani, tukae kwake.

Taarifa Ya Paulo Kwa Kanisa La Yerusalemu

17 Tulipofika Yerusalemu ndugu wa huko walitukaribisha kwa furaha.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica