Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 2Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 12:27-50

27 “Moyo wangu unafadhaika sana. Niombeje? ‘Baba uniepushe na mambo yatakayotokea’? La, nilikuja ulimwenguni kwa sababu hii. 28 Baba, dhihirisha utukufu wa jina lako!” Kisha ikasikika sauti kutoka mbinguni, “Nimedhihirisha utukufu wa jina langu, na nitafanya hivyo tena.” 29 Umati wa watu uliposikia sauti hii, baadhi walidhani ilikuwa ni sauti ya radi, na wengine wakasema, “Malaika alikuwa anaongea naye.” 30 Yesu akawaambia, “Sauti hii imesikika, si kwa faida yangu, bali ni kwa faida yenu. 31 Wakati wa Mungu kutamka hukumu juu ya ulimwengu umetimia, huu ni wakati ambao shetani, mtawala wa dunia hii, atapinduliwa. 32 Nami nitakapoinuliwa kutoka ardhini, nitawavuta watu wote waje kwangu.” 33 Alisema haya ili kuonyesha jinsi atakavyokufa. 34 Wakamwambia, “Tumesoma katika Maandiko ya sheria kuwa Kristo anaishi milele na hatakufa. Mbona unasema lazima Mwana wa Adamu ainuliwe? Huyo Mwana wa Adamu ni nani? 35 Yesu akawajibu, “Nuru yangu itawaangazia kwa muda mfupi. Tembeeni wakati nuru bado ipo nanyi msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui ana kokwenda. 36 Wakati mkiwa na nuru, muitegemee hiyo nuru ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Yesu aliondoka akajificha.

Kutokuamini Kwa Wayahudi

37 Hata baada ya miujiza yote Yesu aliyofanya mbele yao hawakumwamini. 38 Ikawa kama alivyotabiri nabii Isaya aliposema, “Bwana, ni nani ameamini tuliyowaambia? Na ni nani ambaye ameona nguvu za Bwana?” 39 Kwa hiyo hawakuamini, kwa sababu kama Isaya alivyosema tena, 40 “Mungu amewafanya vipofu wasione na mioyo yao ameifanya migumu, ili wasije wakaona kwa macho yao na kuamini kwa mioyo yao, na kumgeukia Mungu awaponye.” 41 Isaya alisema haya kwa kuwa aliona katika maono utukufu wa Yesu na akatabiri juu yake. 42 Hata hivyo wapo wengi, pamoja na viongozi wa Way ahudi, ambao walimwamini, lakini hawakukiri wazi wazi kwa sababu waliwaogopa Mafarisayo, wasije wakafukuzwa kutoka katika masina gogi yao. 43 Wao walithamini zaidi sifa za watu kuliko sifa kutoka kwa Mungu.

Amwaminiye Yesu Hatabaki Gizani

44 Yesu akasema kwa sauti kuu, “Mtu anayeniamini mimi, anamwamini Mungu aliyenituma. 45 Na mtu anayeniona mimi, anam wona yeye ali yenituma. 46 Nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu anayeniamini asibaki gizani. 47 Mtu anayesikia maneno yangu asiyatii, simhukumu; kwa maana sikuja ulimwenguni kuhukumu bali kuokoa. 48 Mtu anayenikataa na kuyapuuza maneno yangu anaye hakimu; neno nililotamka litamhukumu siku ya mwisho. 49 Sikusema mambo haya kwa mamlaka yangu mwenyewe. Bali Baba yangu aliyeni tuma amenipa amri kuhusu mambo ninayosema na kutamka. 50 Ninafa hamu ya kuwa sheria yake ni uzima wa milele. Kwa hiyo ninayosema ni yale ambayo Baba yangu ameniagiza niyaseme.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica