Old/New Testament
Mariamu Ampaka Yesu Mafuta
12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alikwenda mpaka Bethania ambako Lazaro aliyemfufua alikuwa anaishi. 2 Wakamwan dalia karamu; na Martha akawahudumia. Lazaro alikuwa miongoni mwa wageni waliokaa mezani pamoja na Yesu. 3 Kisha Mariamu akachukua chupa yenye manukato ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu ya manukato. 4 Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi, ambaye baadaye alimsaliti Yesu, akasema, 5 “Kwa nini manukato haya hay akuuzwa zikapatikana fedha nyingi wapewe maskini?” 6 Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. 7 Yesu akajibu, “Msimsumbue! Mwacheni ayaweke manukato hayo kwa ajili ya siku ya kifo changu. 8 Maskini wapo pamoja nanyi siku zote ila hamtakuwa nami siku zote. ” 9 Umati mkubwa wa Wayahudi waliposikia kwamba Yesu ali kuwa Bethania, walikuja ili pia wamwone Lazaro ambaye alimfufua. 10 Kwa hiyo makuhani wakuu wakafanya mpango wa kumuua Lazaro pia, 11 kwa kuwa baada ya kufufuliwa kwake Wayahudi wengi wal iamua kuwakataa viongozi wao na kumwamini Yesu.
Yesu Aingia Yerusalemu Akishangiliwa
12 Kesho yake watu wengi waliokuja mjini kwa sikukuu waka pata habari kuwa Yesu angekuja Yerusalemu. 13 Basi wakachukua matawi ya mitende wakatoka kwenda kumpokea, huku wakiimba, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu ambar iki Mfalme wa Israeli!” 14 Yesu akampata mwanapunda akampanda, kama ilivyoandikwa katika Maandiko, 15 “Usiogope, wewe mwenyeji wa Sioni. Tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda!”
16 Wanafunzi wa Yesu hawakuelewa mambo haya wakati huo, lakini Yesu alipofufuka kwa utukufu walikumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yametajwa katika Maandiko; na kwamba waliyatekeleza kwa ajili yake. 17 Wale waliokuwepo wakati Yesu alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua, baadaye waliwasimulia wengine yaliy otokea. 18 Ndio sababu watu wengi walitoka kwenda kumpokea, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu. 19 Mafarisayo walipoona haya wakaambiana, “Mnaona? Hakuna tun aloweza kufanya; ulimwengu wote unamfuata!”
Yesu Anatabiri Kifo Chake
20 Kati ya watu waliokwenda Yerusalemu kuabudu wakati wa sikukuu walikuwepo Wagiriki kadhaa. 21 Hawa walimjia Filipo, ambaye alikuwa mwenyeji wa Bethsaida huko Galilaya, wakamwambia, “Tungependa kumwona Yesu.” 22 Filipo akaenda akamweleza Andrea, na wote wawili wakamwambia Yesu. 23 Yesu akawaambia, “Wakati umefika wa mimi Mwana wa Adamu kutukuzwa. 24 Ninawaha kikishia kuwa, mbegu ya ngano isipopandwa ardhini na kufa, huba kia peke yake. Lakini ikifa inazaa nafaka kwa wingi. 25 Mtu ye yote anayeishi kwa ajili ya nafsi yake tu, ataipoteza, lakini mtu anayeishi kwa ajili ya wengine, atasalimisha nafsi yake kwa maisha ya milele. 26 Mtu ye yote anayetaka kunitumikia lazima anifuate; ili mtumishi wangu awepo mahali nilipo; na mtu ye yote akinitumikia, Baba yangu atampa tuzo ya heshima.
Copyright © 1989 by Biblica