Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Old/New Testament

Each day includes a passage from both the Old Testament and New Testament.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Error: Book name not found: 1Chr for the version: Neno: Bibilia Takatifu
Yohana 8:1-27

Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini

Lakini Yesu akaenda kwenye Mlima wa Mizeituni. Alfajiri Yesu akaja tena Hekaluni, watu wengi wakakusanyika, akakaa akaanza kuwafundisha. Walimu wa sheria na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya watu wote. Wakamwambia Yesu, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini. Katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe wanawake waliokamatwa wakizini, mpaka wafe. Sasa wewe wasemaje?” Walim wuliza hivi kwa kumtega, kusudi wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Yesu akainama chini akaanza kuandika kwa kidole chake mavumbini. Walipoendelea kumwulizauliza akainuka, akawaambia, “Asiyekuwa na dhambi kati yenu awe wa kwanza kumtupia jiwe.” Akainama tena akaendelea kuandika chini. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, akianza mkubwa wao. Yesu akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama pale walipomwacha. 10 Yesu akasimama akamwuliza, “Mama, wale waliokuwa wanakush taki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?” 11 Yule mwa namke akajibu, “Hakuna Bwana.” Yesu akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Unaweza kwenda, lakini usitende dhambi tena.”]

Yesu Ni Nuru Ya Ulimwengu

12 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.” 13 Mafarisayo wakam wambia, “Ushuhuda wako haukubaliki kwa sababu unajishuhudia mwe nyewe.” 14 Yesu akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni wa kweli kwa sababu najua nilikotoka na nina kokwenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakokwenda. 15 Ninyi mnatoa hukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu. Mimi simhukumu mtu ye yote. 16 Lakini hata kama nikitoa hukumu, ita kuwa sahihi kabisa kwa sababu sitoi hukumu peke yangu; Baba ali yenituma yupo pamoja nami. 17 Imeandikwa katika Sheria zenu kwamba ushahidi wa watu wawili unatosha kuthibitisha ukweli. 18 Mimi najishuhudia mwenyewe; shahidi wangu mwingine ni Baba ambaye amenituma.” 19 Wakamwuliza, “Huyo baba yako yuko wapi?” Yesu akawajibu, “Ninyi hamfahamu mimi ni nani, wala ham fahamu Baba yangu ni nani. Kama mngefaham u mimi ni nani, mngem fahamu na Baba yangu.” 20 Yesu alisema haya alipokuwa akifund isha Hekaluni katika chumba ambamo vyombo vya sadaka viliwekwa. Wala hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa wakati wake ulikuwa hauja timia.

Yesu Asema, ‘Niendako Hamwezi Kufika’

21 Tena Yesu akawaambia, “Nitaondoka, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Mahali ninapokwenda ninyi hamwezi kufika.” 22 Wale Wayahudi wakaulizana, “Mbona anasema, ‘Mahali ninapokwenda hamwezi kufika’? Je, anataka kujiua?” 23 Akawaambia, ‘Tofauti kati yenu na Mimi ni kwamba ninyi ni wa hapa duniani, mimi natoka mbinguni. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu. 24 Kwa hiyo nimewaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Kwa maana msipoamini ya kwamba ‘Mimi Ndiye 25 Wakamwuliza, “Kwani wewe ni nani?” Yesu akawajibu, “Nimekuwa nikiwaambia mimi ni nani tangu mwanzo. 26 Kuna mambo mengi ambayo ningeweza kusema juu yenu na kuna mambo mengi ambayo ningeweza kuwahukumu. Lakini yeye ali yenituma ni wa kweli, na yale niliyosikia kutoka kwake nawaambia wa ulimwengu.” 27 Hawakuelewa kuwa alikuwa anasema juu ya Baba yake wa Mbinguni.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica