Old/New Testament
22 Umati wa watu waliokuwepo wakaunga mkono mashtaka haya, na wale maha kimu wakatoa amri Paulo na Sila wavuliwe nguo wachapwe viboko. 23 Baada ya kuchapwa sana wakatupwa gerezani, na askari jela akaamriwa aweke ulinzi mkali. 24 Yule askari jela alipopokea amri hiyo akawaweka katika chumba cha ndani mle gerezani na kisha akafunga miguu yao kwa mkatale. 25 Ilipokaribia saa sita za usiku, Paulo na Sila walikuwa wakiomba na kuimba nyimbo za kum sifu Mungu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza. 26 Gha fla pakatokea tetemeko kubwa la nchi, hata msingi wa jengo la gereza ukatikisika. Mara milango ya gereza ikawa wazi na mikatale yao ikafunguka. 27 Askari wa gereza alipoona kuwa milango ya gereza ni wazi, alivuta upanga wake ili ajiue, akidhani ya kuwa wafungwa wote wametoroka. 28 Lakini Paulo akapiga kelele kum zuia, akasema, “Usijidhuru kwa maana hatujatoroka, wote tuko hapa.” 29 Askari akaitisha taa iletwe, akaingia ndani ya chumba cha gereza, akapiga magoti akitetemeka miguuni mwa Paulo na Sila. 30 Kisha akawatoa nje akasema, “Ndugu zangu, nifanye nini ili nipate kuokoka?” 31 Wakamjibu, “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka, wewe pamoja na jamaa yako.” 32 Wakawaambia neno la Bwana yeye pamoja na wote waliokuwa wanaishi nyumbani kwake. 33 Yule askari akawachukua saa ile ile akaosha majeraha yao, naye akabatizwa pamoja na wote waliokuwa nyumbani kwake. 34 Aka wachukua, akawaandalia chakula nyumbani kwake, naye akafurahi pamoja na jamaa yake kwa kuwa alikuwa amemwamini Mungu.
35 Kulipopambazuka wale mahakimu wakamtuma polisi amwambie yule askari jela, “Waachie hao watu waende zao.” 36 Yule askari jela akampasha habari Paulo akisema, “Mahakimu wametuma niwaachilie huru; kwa hiyo tokeni mwende kwa amani.” 37 Lakini Paulo akawaambia, “Wametuchapa viboko hadharani bila kufanya kesi na kutoa hukumu, na sisi ni raia wa Kirumi. Je, sasa wana taka kututoa gerezani kisiri siri? Hii si haki! Waambieni wao waje watutoe humu gerezani wenyewe.” 38 Yule askari akarudi kwa wale mahakimu kuwaeleza maneno haya, nao wakaogopa sana walipofa hamu kuwa Paulo na Sila ni raia wa Kirumi. 39 Kwa hiyo wakaja wakawaomba msamaha. Kisha wakawatoa gerezani, wakawaomba waondoke mjini. 40 Paulo na Sila walipotoka gerezani walimtembelea Lidia, wakakutana na ndugu waamini wakawatia moyo; ndipo wakaondoka.
Copyright © 1989 by Biblica