Old/New Testament
26 “Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, na ninyi mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu ni kwa ajili yetu. 27 Watu wa Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua Yesu kuwa ni Mwokozi. Lakini kwa kum hukumu kifo walitimiza maneno ya manabii yaliyokuwa yaliyokuwa yakisomwa kila siku ya sabato. Hata hivyo wameyafanya maneno ya manabii kutimilika walipomshitaki Yesu. 28 Ijapo kuwa hawakupata sababu yo yote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato amtoe auawe. 29 Na baada ya kufanya kila kitu kilichotabiriwa katika Maandiko kumhusu, wakamshusha kutoka msalabani wakamweka kaburini. 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. 31 Na kwa siku nyingi akawatokea wale waliosafiri naye kutoka Galilaya kwenda Yerusalemu. Wao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wote.
32 “Nasi tunawaletea Habari Njema kwamba yale Mungu aliy oahidi baba zetu, 33 sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya Pili, ‘Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako.’ 34 Na kuhusu kufufuka kwake, na kwamba hataona tena uharibifu, Mungu alisema hivi, ‘Nitakupa wewe baraka takatifu za hakika ambazo nilimwahidi Daudi.’ 35 Na pia Maandiko yanasema katika sehemu nyingine, ‘Wewe hutaruhusu Mtakatifu wako aone uharibifu.’ 36 Kwa maana Daudi alipokwisha kamilisha mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alikufa akazikwa pamoja na baba zake, mwili wake ukaharibika. 37 Lakini yule ambaye Mungu alimwinua kutoka kwa wafu, mwili wake haukuharibika. 38 Kwa hiyo ndugu zangu, fahamuni kwamba katika huyu Yesu, msa mahawa dhambi unatangazwa kwenu. 39 Kwa ajili yake, kila mtu amwaminiye anawekwa huru na yale yote ambayo sheria ya Musa haikuweza kuwaweka huru. 40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliy osema manabii yasiwapate: 41 ‘Tazameni ninyi wenye kudharau, mkapate kushangaa na kuangamia kwa maana nitatenda jambo wakati wenu, ambalo hamtalisadiki, hata kama mtu akiwatangazia.’
42 Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi watu waliwasihi warudi tena sabato ifuatayo wawaambie zaidi kuhusu mambo haya. 43 Baada ya mkutano wa sinagogi kumalizika Wayahudi wengi na waongofu wa dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Bar naba, nao wakazungumza na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44 Sabato iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la Mungu. 45 Lakini Wayahudi walipoona lile kusanyiko kubwa la watu, waliona wivu, wakakanusha mafundisho ya Paulo na kumtukana. 46 Paulo na Barnaba wakazidi kufundisha kwa ujasiri, wakisema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu lihubiriwe kwanza kwenu Wayahudi. Lakini kwa kuwa mnalikataa, mnajihukumu wenyewe kuwa hamstahili kupata uzima wa milele. Tutawahubiria watu wa mataifa mengine. 47 Kwa maana Bwana ametuagiza akisema, ‘Nimewaweka ninyi kuwa nuru kwa watu wa mataifa, ili mpeleke wokovu hadi pembe zote za dunia.”’ 48 Watu wa mataifa mengine waliposikia maneno haya walifurahi, wakalitukuza neno la Mungu; na wote waliochaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Mungu likaenea sehemu zote katika jimbo lile. 50 Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake waheshimiwa wamchao Mungu pamoja na viongozi maarufu wa mji, wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba na kisha wakawafukuza kutoka wilaya ile. 51 Paulo na Barnaba wakakung’uta mavumbi miguuni mwao kuwapinga, wakaenda mji wa Ikonio. 52 Na Wanafunzi wakajazwa na furaha ya Roho Mtaka tifu.
Copyright © 1989 by Biblica