Old/New Testament
Barua Kwa Waamini Wa Mataifa Mengine
22 Mitume na wazee na kanisa zima wakakubaliana. Wakachagua watu waongozane na Paulo na Barnaba kwenda Antiokia. Walimchagua Yuda aitwaye Barsaba na Sila. Hawa wawili walikuwa viongozi wal ioheshimiwa miongoni mwa ndugu wote. 23 Wakatumwa na barua ifu atayo: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimu ninyi wa mataifa mlioamini huko Antiokia, Siria na Kilikia. 24 Kwa kuwa tumesikia kwamba kuna baadhi ya watu kati yetu waliokuja huko bila kibali chetu kutatanisha mawazo yenu kwa maneno yao, 25 tumeona ni vyema, kwa kauli moja, kuwachagua watu waje huko pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26 ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. 27 Tumewatuma hawa ndugu, Yuda na Sila, wawaeleze kwa mdomo mambo haya tunayow aandikia. 28 Kwa maana Roho Mtakatifu ameona vyema na sisi tume kubaliana tusiwatwike mzigo mkubwa zaidi ya mambo yafuatayo ambayo ni ya lazima: 29 kwamba msile cho chote kilichotolewa sadaka katika ibada za sanamu, kunywa damu, nyama ya wanyama wal ionyongwa; na muepukane na uasherati. Mkijitenga na mambo haya mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.”
30 Wale wajumbe walipokwisha kuagwa, wakaondoka wakaenda Antiokia, wakakusanya ushirika wote wa waamini, wakawapa ile barua. 31 Nao watu walipokwisha kuisoma, wakafurahishwa sana na ujumbe wake wa kutia moyo. 32 Yuda na Sila, ambao walikuwa mana bii wa kawapa ushauri mwingi wa kuwatia moyo na kuwajenga katika imani. 33 Wakakaa Antiokia kwa muda na kisha waamini wakawaaga. Wakarudi kwa amani kwa wale waliowatuma. [ 34 Lakini Sila aliona ni vema kukaa huko.] 35 Lakini Paulo na Barnaba walibaki Anti okia pamoja na wengine wengi wakifundisha na kuhubiri neno la
Paulo Na Barnaba Wanatengana
36 Baada ya siku chache Paulo alimwambia Barnaba, “Twende tukawatembelee ndugu katika miji yote ambamo tulihubiri neno la Bwana tuone jinsi waamini wanavyoendelea.” 37 Barnaba alitaka wamchukue Yohana Marko waende naye. 38 Lakini Paulo aliona si vizuri kumchukua kwa sababu aliwahi kuwakimbia walipokuwa huko Pamfilia, akakataa kuendelea kufanya kazi nao. 39 Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba juu ya jambo hili, wakaten gana. Barnaba akamchukua Yohana Marko akaenda naye Kipro. 40 Paulo akamchagua Sila akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana. 41 Naye akapitia Siria na Kilikia wakaimarisha makanisa ya huko.
Copyright © 1989 by Biblica