Old/New Testament
Ghasia Huko Efeso
21 Baada ya mambo haya kutokea, Paulo aliongozwa na Roho kupitia Makedonia na Akaya akiwa njiani kwenda Yerusalemu. Paulo alisema, “Nikishafika Yerusalemu, ni lazima niende Rumi pia.” 22 Akatuma wasaidizi wake wawili, Timotheo na Erasto, waende Makedonia, naye akakaa Asia kwa muda kidogo zaidi. 23 Wakati huo huo pakatokea ghasia kubwa kwa sababu ya Njia ya Bwana. 24 Mtu mmoja aitwaye Demetrio mhunzi wa vinyago vya fedha alikuwa akitengeneza vihekalu vya fedha vya Artemi na kuwa patia mafundi wake biashara kubwa. 25 Yeye aliwakutanisha watu hawa pamoja na watu wengine wanaofanya kazi za kutengeneza viny ago vya miungu kama wao akawaambia, “Jamani, mnajua ya kuwa uta jiri wetu unatokana na kazi zetu. 26 Lakini mmeona na kusikia jinsi ambavyo huko Efeso na karibu Asia yote huyu Paulo amewash awishi watu na kutuharibia biashara kwa kusema kuwa miungu iliy otengenezwa na watu si miungu ya kweli. 27 Kwa hiyo kuna hatari kuwa kazi yetu itaanza kudharauliwa. Na si hivyo tu, bali hata hekalu la mungu wetu Artemi, aliye mkuu na anayeabudiwa Asia yote na ulimwengu wote, litakuwa halina maana tena na utukufu wake utaondolewa.”
28 Waliposikia maneno haya walighadhabika wakapiga kelele, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 29 Mji mzima ukajaa vurugu, waka kimbilia katika ukumbi wa michezo kwa pamoja wakawakamata Gayo na Aristarko, Wamakedonia waliokuwa wakisafiri na Paulo. 30 Paulo alitaka kuingilia kati lakini wanafunzi wengine wakam zuia; 31 hata baadhi ya viongozi waliokuwa marafiki wa Paulo walituma watu wamsihi asiingie katika ule ukumbi. 32 Pakawa na kutokuelewana katika ule ukumbi kwa sababu baadhi ya watu wali kuwa wakisema jambo moja na wengine lingine. Ikawa ni fujo; wengi wa watu waliofika hawakujua ni kwa nini walikuwa wamekusanyika huko. 33 Wayahudi wakamchagua Aleksanda azungumze kwa niaba yao naye akawaashiria watu wanyamaze apate kuzungumza. 34 Lakini umati ulipogundua yakuwa yeye ni Myahudi, walipiga kelele kwa kiasi cha saa mbili wakisema, “Artemi wa Waefeso ni mkuu!” 35 Baadaye karani wa mji alipofanikiwa kuwanyamazisha, aliwahu tubia akasema, “Ndugu Waefeso, kila mtu ulimwenguni anajua ya kuwa mji wa Efeso ndio unaotunza hekalu la Artemi aliye mkuu na ile sanamu iliyoanguka kutoka angani. 36 Kwa hiyo, kwa kuwa hakuna anayeweza kukanusha mambo haya, sioni sababu ya ninyi kufanya fujo au kuchukua hatua ambazo baadaye huenda mkazijutia. 37 Kwa maana mmewaleta hawa watu wawili hapa ingawa wao hawaja fanya uharibifu wo wote kwa hekalu la Artemi au kusema maneno ya kufuru juu ya huyu mungu wetu mwanamke. 38 Kama Demetrio na mafundi wenzake wana mashtaka juu ya mtu ye yote, mahakama ziko wazi na mahakimu wapo; wachukue hatua za kisheria. 39 Lakini kama kuna mashauri mengine, itabidi mtumie baraza halali. 40 Hivi sasa tuko katika hatari ya kushtakiwa kwa kufanya fujo kwa maana hatuna sababu ya kuridhisha kuhusu mambo yaliyotokea leo.” 41 Baada ya kusema haya akavunja mkutano.
Copyright © 1989 by Biblica