Old/New Testament
24 Yesu alipoona kuwa amehuzunika, akasema, “Itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. 25 Ni rahisi kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”
26 Watu waliposikia hili, wakasema, “Sasa ni nani anayeweza kuokolewa?”
27 Yesu akajibu, “Lisilowezekana kwa wanadamu, linawezekana kwa Mungu.”
28 Petro akasema, “Tazama! Tumeacha vyote tulivyokuwa navyo na kukufuata.”
29 Yesu akasema, “Ninaahidi kuwa kila aliyeacha nyumba, mke, ndugu, wazazi, au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu, 30 atapokea zaidi ya kile alichoacha. Atapokea mara nyingi zaidi katika maisha haya. Na katika ulimwengu ujao atapata mara nyingi zaidi.”
Yesu Azungumza Tena Kuhusu Kifo Chake
(Mt 20:17-19; Mk 10:32-34)
31 Kisha Yesu alizungumza na mitume wake kumi na mbili wakiwa peke yao. Akawaaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu. Kila kitu ambacho Mungu aliwaambia manabii waandike kuhusu Mwana wa Adamu kitatokea. 32 Atakabidhiwa kwa wasio Wayahudi, ambao watamcheka, watamtukana na kumtemea mate. 33 Watamchapa kwa mijeledi kisha watamuua. Lakini katika siku ya tatu baada ya kifo chake, atafufuka kutoka kwa wafu.” 34 Mitume walijaribu kulielewa hili, lakini hawakuweza; maana yake ilifichwa wasiielewe.
Yesu Amponya Asiyeona
(Mt 20:29-34; Mk 10:46-52)
35 Yesu alipofika karibu na mji wa Yeriko, mwanaume mmoja asiyeona alikuwa amekaa kando ya barabara, akiomba pesa. 36 Aliposikia kundi la watu linapita barabarani, akauliza, “Nini kimetokea?”
37 Walimwambia, “Yesu kutoka Nazareti anapitia hapa.”
38 Kipofu akapasa sauti yake, akaita, “Yesu, Mwana wa Daudi, tafadhali nisaidie!”
39 Watu waliotangulia, wakiongoza kundi, wakamkanya asiyeona, wakamwambia anyamaze. Lakini alizidi sana kupaza sauti zaidi na zaidi, “Mwana wa Daudi, tafadhali unisaidie!”
40 Yesu alisimama pale na akasema, “Mleteni yule asiyeona kwangu!” Yule asiyeona alipofika kwa Yesu, Yesu akamwuliza, 41 “Unataka nikufanyie nini?”
Asiyeona akasema, “Bwana, nataka kuona.”
42 Yesu akamwambia, “Unaweza kuona sasa. Umeponywa kwa sababu uliamini.”
43 Yule mtu akaanza kuona saa ile ile. Akamfuata Yesu, akimshukuru Mungu. Kila mtu aliyeliona hili alimsifu Mungu.
© 2017 Bible League International