Beginning
1 Kutoka kwa Paulo, aliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo, na Sosthene ndugu yetu.
2 Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wote waliota kaswa katika Kristo Yesu, wakaitwa wawe watakatifu, pamoja na wengine wote ambao kila mahali wanalikiri jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wao na Bwana wetu. 3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Baraka Zitokazo Kwa Kristo
4 Ninamshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema aliyowapa ndani ya Kristo Yesu. 5 Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kunena kwenu, katika maarifa yote, 6 kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. 7 Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Yeye atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.
Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa
10 Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane ninyi kwa ninyi, na pasiwepo na utengano kati yenu. Muungane pamoja kikamilifu katika kuwaza na katika kuamua. 11 Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa watu wa nyumbani kwa Kloe kwamba kuna ugomvi kati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: mmoja wenu anasema, “Mimi ni wa Paulo,” mwin gine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”
13 Je, Kristo amegawanyika? Je, ni Paulo aliyewafia msala bani? Au mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwa sababu sikumbatiza mtu ye yote isipokuwa Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyo hakuna mtu kati yenu anayeweza kusema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 Ndiyo nakumbuka, pia niliwabatiza Stefano na watu wa nyumbani kwake. Lakini zaidi ya hao sikumbuki kama nilimbatiza mtu mwingine. 17 Kwa maana Kristo hakunituma kubatiza bali kuhu biri Injili na nifanye hivyo pasipo kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu, ili nguvu ya kifo cha Kristo msalabani iwe dhahiri.
Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu
18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Maan diko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.” 20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22 Way ahudi wanataka ishara, Wagiriki wanatafuta hekima. 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa msalabani, ujumbe ambao ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa Wagiriki ni upuuzi. 24 Lakini kwa walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25 Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa Mungu alipowaita. Si wengi mlikuwa na hekima kwa kipimo cha kibinadamu. Si wengi mli kuwa na vyeo na si wengi mlikuwa wa jamaa za kifahari. 27 Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu alichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa humu duniani, vitu ambavyo si kitu, ili avibatilishe vile ambavyo vinaonekana kuwa vya maana; 29 ili mtu ye yote asijisifu mbele yake. 30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi 31 Kwa hiyo, kama Maan diko yasemavyo: “Mtu ye yote anayetaka kujisifu, basi ajisifu kwa ajili ya Bwana.”
Ujumbe Wa Msalaba
2 Nilipokuja kwenu ndugu zangu, sikuja kuhubiri siri ya mpango wa Mungu kwa kutumia ufasaha wa kuzungumza au hekima ya binadamu.
2 Kwa kuwa niliamua kwamba wakati nikiwa nanyi nitasahau kila kitu isipokuwa Yesu Kristo; Kristo aliyesulubiwa msalabani. 3 Nilikuja kwenu nikiwa mdhaifu, mwenye woga na nikitetemeka sana. 4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa na hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali ujumbe wangu ulidhihirisha wazi nguvu za Roho, 5 ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali ijengwe katika nguvu ya Mungu.
Hekima Ya Mungu
6 Lakini miongoni mwa watu waliokua kiroho, tunafundisha maneno ya hekima, hii si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa nyakati hizi ambao watatoweka. 7 Hekima tunayofundisha ni hekima ya siri ya Mungu ambayo imefichwa kwa wanadamu, na ambayo Mungu aliipanga kabla ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 8 Watawala wa nyakati zetu hawakuielewa hekima hii. Kwa maana kama wangeliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa Utukufu.
9 Lakini, kama Maandiko yasemavyo, “Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao.” 10 Lakini Mungu amekidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu. 11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12 Sisi hat ukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure. 13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho. 14 Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu kwa sababu mambo hayo ni upuuzi kwake; na hawezi kuyaelewa kwa kuwa hayo yanaeleweka tu kwa msaada wa Roho.
15 Mtu wa kiroho anao uwezo wa kupima kila kitu, lakini yeye hapimwi na mtu. 16 “Kwa maana ni nani amefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumshauri?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Mgawanyiko Katika Kanisa
3 Lakini ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwili, na kama watoto wachanga katika Kristo. 2 Niliwalisha maziwa, sio chakula kigumu; kwa kuwa mli kuwa hamjawa tayari kukipokea. 3 Kwa maana ninyi bado mnatawaliwa na mambo ya mwili. Je, wakati kuna wivu na kugombana kati yenu, ninyi si watu wa mwili wenye tabia kama za watu wa kawaida? 4 Kwa maana mmoja anaposema, “Mimi ni wa Paulo,” na mwingine, “Mimi ni wa Apolo” hamfanyi kama watu wa kawaida?
5 Hata hivyo, Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Sisi ni watum ishi tu ambao kama Bwana alivyotupangia kila mmoja kazi yake, mliamini kwa msaada wetu. 6 Mimi nilipanda mbegu, na Apolo akaimwagilia maji, lakini ni Mungu aliyefanya mbegu iote. 7 Kwa hiyo anayepanda mbegu na anayemwagilia maji si kitu, bali Mungu pekee ndiye aliyefanya mbegu iote. 8 Anayepanda mbegu ni sawa na yule anayemwagilia maji. Kila mmoja wao atapokea malipo yake kulingana na kazi yake. 9 Sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu; ninyi ni jengo la Mungu.
10 Kwa neema niliyopewa na Mungu nilijenga msingi kama mjenzi hodari, na mtu mwingine ana jenga juu ya msingi huo. Lakini kila mmoja awe mwangalifu anavyojenga juu yake. 11 Kwa maana hakuna mtu anayeweza kuweka msingi mwingine isipokuwa ule uliokwisha jengwa, ambao ni Yesu Kristo. 12 Kama mtu ye yote atajenga juu ya msingi huu akitumia dhahabu, fedha, mawe ya tha mani, mbao, majani au nyasi, 13 kazi yake itaonekana; kwa kuwa ile siku itaidhihirisha kazi yake. Itadhihirishwa kwa moto, na moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. 14 Kama alichojenga hakitaharibiwa kwa moto, atapokea tuzo. 15 Kama kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo. 18 Mtu asijidanganye mwenyewe. Kama kuna mtu miongoni mwenu anadhani kuwa yeye ana hekima kwa kipimo cha nyakati hizi, basi afadhali awe mjinga ili apate kuwa na hekima ya kweli. 19 Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuuzi mbele za Mungu. Kama Maandiko yasemavyo, “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao.’ ’ 20 Na tena, “Bwana anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni bure.”
21 Kwa hiyo mtu asijivune kwa sababu ya watu. Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu, 22 kama ni Paulo au Apolo au Petro au dunia au maisha au kifo, au wakati uliopo au wakati unaokuja, haya yote ni yenu; 23 na ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
Mitume Wa Kristo
4 Basi, mtuhesabu sisi kuwa watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu. 2 Zaidi ya hayo, mawakili wanatakiwa wawe waaminifu. 3 Mimi sijali kama ninyi mkinihukumu au nikihukumiwa na mahakama ya wanadamu; kwa kweli hata mimi mwenyewe sijihukumu 4 Dhamiri yangu hainishitaki; lakini hilo halinifanyi nisiwe na hatia. Bwana ndiye anayenihukumu. 5 Kwa hiyo msitoe hukumu kabla ya wakati wake, kabla Bwana hajaja. Yeye atafichua mambo yaliyof ichwa gizani na kwa kuweka wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mtu atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
6 Basi ndugu zangu nimetumia mfano wa Apolo na mimi kwa faida yenu ili muweze kujifunza kutoka kwetu maana ya usemi, “Usivuke mpaka wa yale yaliyoandikwa.” Na hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine. 7 Ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na watu wengine wote? Mna kitu gani ambacho hamkupokea? Basi ikiwa mmepokea, mbona mnajivuna kana kwamba hayo mliyonayo si zawadi?
8 Mmekwisha pata kila kitu mnachohitaji! Mmekuwa matajiri! Mmekuwa wafalme pasipo msaada wetu! Lakini laiti kama mngekuwa wafalme kweli ili na sisi tuwe wafalme pamoja nanyi! 9 Kwa sababu inaonekana kwamba Mungu ametuweka sisi mitume katika nafasi ya mwisho kabisa katika msafara wa maonyesho kama watu waliohukumiwa kufa hadharani, kwa sababu tumekuwa maonyesho kwa ulimwengu wote, kwa malaika na kwa wanadamu pia.
10 Kwa ajili ya Kristo sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima ndani ya Kristo. Sisi ni dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa. 11 Mpaka wakati huu tuna njaa na kiu, tumevaa matambara, tumeteswa, hatuna makao. 12 Tunafanya kazi ngumu kwa mikono yetu. Tunapolaaniwa, tunabar iki; tunapoteswa tunavumilia. 13 Tunaposingiziwa tunajibu kwa maneno ya upole. Tumekuwa kama takataka ya dunia hii, na uchafu wa ulimwengu mpaka leo hii.
14 Nawaandikia mambo haya, si kwa sababu nataka muone aibu, bali nataka niwaonye kama wanangu wapendwa. 15 Ingawa mnao viongozi wasiohesabika katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili. 16 Basi nawasihi mfuate mfano wangu. 17 Kwa sababu hii ninam tuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu maisha yangu katika Kristo ambayo yanakubal iana na mafundisho yangu katika kila kanisa ninalotembelea.
18 Baadhi yenu mmekuwa na kiburi mkidhani kuwa sitafika kwenu. 19 Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, zaidi ya maneno yao hawa watu wenye kiburi wana uwezo gani? 20 Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu bali ni nguvu. 21 Ninyi amueni. Nije kwenu na fimbo kuwaadhibu, au nije na upendo kwa roho ya upole?
Copyright © 1989 by Biblica