Print Page Options Listen to Acts 1-3
Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Matendo Ya Mitume 1-3

Mpendwa Teofilo, Katika Kitabu changu cha kwanza nilikuan dikia kuhusu mambo yote aliyotenda Yesu, hadi wakati alipopaa mbinguni. Kabla hajachukuliwa juu, aliwapa mitume wake maagizo kwa njia ya Roho Mtakatifu. Alijionyesha kwao akiwa hai muda wa siku arobaini baada ya kufufuka kwake. Akawahakikishia kwa njia nyingi ya kuwa ni yeye na akaongea nao kuhusu Ufalme wa Mungu.

Wakati mmoja alipokuwa nao, aliwapa amri hii, “Msiondoke Yerusalemu, mpaka mtakapopokea ahadi aliyotoa Baba, ambayo mmeni sikia nikiizungumzia. Kwa maana Yohana aliwabatiza kwa maji lakini baada ya siku chache mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”

Yesu Apaa Mbinguni

Mitume walipokutana na Yesu walimwuliza, “Bwana, wakati huu ndipo utawarudishia Waisraeli ufalme ?”

Yesu akawaambia, “Si juu yenu kufahamu wakati na majira ambayo yamewekwa na Baba kwa mamlaka yake. Lakini mtapokea nguvu akishawajilia Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria, hadi mwisho wa dunia.”

Baada ya kusema haya, wakiwa wanatazama, alichukuliwa juu, na wingu likamficha wasimwone tena. 10 Walikuwa bado wakikaza macho yao mawinguni alipokuwa akienda, ndipo ghafla, wanaume wawili waliovaa mavazi meupe walisimama karibu nao, 11 wakasema, “Ninyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama hapa mkitazama mbin guni? Yesu huyu huyu aliyechukuliwa mbinguni atarudi tena kama mlivyomwona akienda mbinguni.”

12 Ndipo mitume waliporudi Yerusalemu kutoka mlima wa Mizeituni ulioko umbali wa kama kilometa moja kutoka mjini. 13 Walipoingia mjini Yerusalemu walikwenda katika chumba cha ghorofani walipokuwa wakiishi: Petro, Yohana, Yakobo na Andrea, Filipo, Tomaso, Bartholomayo na Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo na Simoni aliyeitwa Mzalendo, na Yuda mwana wa Yakobo.

14 Hawa wote waliamua kwa kauli moja kutumia muda wao wote kusali, wakiwa pamoja na wale akina mama, Mariamu mama yake Yesu pamoja na ndugu zake.

15 Ilikuwa ni katika siku hizo ambapo Petro alisimama kati ya waamini wote, watu wapatao mia moja na ishirini, 16 akasema, “Ndugu zangu, ilibidi Maandiko ambayo Roho Mtakatifu alitabiri kupitia kwa Daudi kumhusu Yuda aliyewaongoza wale waliomkamata Yesu, yatimie. 17 Yuda alikuwa mmoja wetu, kwa maana na yeye alichaguliwa ashiriki katika huduma hii.” 18 Yuda alinunua shamba kwa zile fedha alizopata kutokana na uovu wake na akiwa huko shambani alianguka kifudifudi akapasuka na matumbo yote yakatoka nje. 19 Kila mkazi wa Yerusalemu alisikia habari hizi, kwa hiyo wakapaita mahali hapo kwa lugha yao, Akeldama, yaani ‘shamba la Damu.’ 20 Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Zab uri, ‘Mahali pake pasiwe na kitu wala asiwepo mtu atakayekaa hapo,’ na, ‘Nafasi yake ichukuliwe na mwingine.”’

Mathiya Achaguliwa

21 “Kwa hiyo inatubidi tumchague mtu mwingine kati ya wale ambao wamekuwa pamoja nasi 22 tangu wakati Yesu alipobatizwa na Yohana mpaka siku aliyochukuliwa mbinguni. Mmoja wao inabidi aun gane nasi kama shahidi wa ufufuo wa Yesu.”

23 Wakapendekeza majina ya watu wawili. Yusufu, aitwaye Barsaba, pia alijulikana kama Yusto, na Mathiya. 24 Wakaomba, “Bwana ujuaye mioyo ya watu wote, tunakuomba utuonyeshe ni yupi kati ya hawa wawili uliyemchagua 25 achukue nafasi ya huduma na utume ambayo Yuda aliiacha akaenda panapomstahili.”

26 Kisha wakapiga kura na Mathiya akachaguliwa. Basi akain gizwa katika kundi la wale mitume kumi na mmoja.

Kushuka Kwa Roho Mtakatifu

Ilipofika siku ya Pentekoste, waamini wote walikuwa wameku tana mahali pamoja. Ghafla, sauti kama mvumo mkubwa wa upepo uliwashukia kutoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wamekaa. Pakatokea kitu kama ndimi za moto ambao uligawanyika ukakaa juu ya kila mmoja wao. Wote walijazwa Roho Mtakatifu wakaamza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kusema.

Wakati huo walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka nchi zote za dunia. Waliposikia kelele hizi, walikusany ika kwa wingi. Wote walishangaa kwa sababu waliwasikia waamini wakiongea lugha ya kila mmoja wao.

Wakastaajabu sana, wakasema, “Hawa wote wanaozungumza ni Wagalilaya. Imekuwaje basi tunawasikia wakinena lugha ya kila mmoja wetu? Hapa kuna Waparthi, Wamedi, Waelami, wakazi wa Mesopotamia, Yudea Kapadokia, Ponto na Asia, 10 Frigia, Pom filia, Misri na pande za Libya karibu na Kirene; na wageni kutoka Rumi, Wayahudi na watu walioingia dini ya Kiyahudi. 11 Watu wen gine wametoka Krete na Uarabuni. Sisi sote tunasikia watu hawa wakisema katika lugha zetu wenyewe mambo makuu ya ajabu aliyofa nya Mungu.” 12 Wakiwa wameshangaa wakaulizana, “Ni nini maana ya mambo haya?” 13 Lakini wengine waliwadhihaki wakasema, “Hawa wamelewa divai mpya!”

Mahubiri Ya Petro

14 Ndipo Petro akasimama na wale mitume kumi na mmoja, aka hutubia ule umati wa watu kwa sauti kuu akasema, “Wayahudi wen zangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu. Nisikilizeni kwa makini niwaambie jambo hili maana yake ni nini! 15 Hawa watu hawakulewa kama mnavyodhania, kwa maana sasa ni mapema mno, saa tatu asu buhi. 16 La, jambo hili lilitabiriwa na Nabii Yoeli aliposema, 17 ‘Mungu alisema, siku za mwisho nitawamiminia binadamu wote Roho yangu: wavulana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wataota ndoto. 18 Ndio, hata watumishi wangu wa kiume na wa kike nitawamiminia Roho yangu, nao watata biri. 19 Nami nitafanya maajabu angani, na duniani nitaonyesha ishara, damu na moto na moshi mnene. 20 Jua litageuka kuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya siku ya Bwana kuwa dia, siku ambayo itakuwa ya kutisha. 21 Lakini ye yote ata kayetubu na kukiri jina la Bwana, ataokoka.’

22 “Nawasihi ninyi Waisraeli mnisikilize. Yesu wa Nazareti alikuwa mtu aliyethibitishwa kwenu na Mungu kwa njia ya miujiza, maajabu na ishara, kama ninyi wenyewe mjuavyo. 23 Huyu Yesu ali tiwa mikononi mwenu kwa mpango na makusudi ya Mungu aliyoyafahamu tangu awali. Nanyi mlimwua kwa kumtundika na kumpigilia misumari msalabani, mkisaidiwa na watu waovu. 24 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu hata kifo kisingaliweza kumzuia. 25 Daudi alisema hivi juu yake, ‘Nilimwona Bwana akiwa mbele yangu wakati wote, Bwana yuko upande wangu wa kulia ili nisiogope. 26 Kwa hiyo moyo wangu unafurahi na ulimi wangu unashangilia; mwili wangu nao una matumaini ya uzima. 27 Kwa maana wewe Bwana hutaniacha kuzimu; wala hutaacha mtakatifu wako ateseke na kuoza. 28 Wewe umenionyesha njia inifikishayo uzimani. Na uwepo wako ukiwepo nami nitajawa na furaha.’

29 “Ndugu zangu, nataka niwaambie wazi kwamba mfalme Daudi alikufa na kuzikwa, na kaburi lake lipo hata leo. 30 Lakini ali kuwa nabii, na alijua ya kuwa Mungu aliahidi kwa kiapo kwamba angempa mmoja wa uzao wake kiti chake cha ufalme. 31 Kwa hiyo Daudi akaona mambo ambayo yangetokea, akatamka juu ya kufufuka kwa Kristo, kwamba asingeachwa kuzimu, wala mwili wake usingehar ibiwa kwa kuoza. 32 Huyu Yesu, Mungu alimfufua, na sisi ni mash ahidi wa tukio hilo.

33 “Basi akiwa ametukuzwa na kukaa upande wa kulia wa Mungu, alipokea Roho Mtakatifu aliyeahidiwa na Baba yake. Huyo Roho Mtakatifu ndiye aliyetumiminia haya mnayoyaona na kuyasikia. 34 Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini alisema, ‘Bwana alim wambia Bwana wangu: kaa upande wangu wa kulia, 35 mpaka nitaka powafanya maadui zako kiegemezo cha miguu yako.’

36 “Basi nataka niwahakikishie Waisraeli wote ya kuwa, Mungu amemfanya huyu Yesu ambaye ninyi mlimsulubisha, kuwa ndiye

Ongezeko La Waamini

37 Watu waliposikia maneno haya yaliwachoma moyoni, wakawau liza Petro na wale mitume wengine, “Tufanye nini ndugu zetu?” 38 Petro aliwajibu, “Tubuni, muache dhambi na kila mmoja wenu abatizwe katika jina la Yesu Kristo, ili msamehewe dhambi zenu; nanyi mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu. 39 Kwa maana ahadi hii ilitolewa na Mungu kwa ajili yenu na watoto wenu, na wale wote walio nchi za mbali, na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu anamwita kwake.”

40 Petro aliwasihi kwa maneno mengine mengi na kuwaonya akisema, “Jiepusheni na kizazi hiki kiovu.” 41 Wote waliopokea ujumbe wa Petro walibatizwa na zaidi ya watu elfu tatu wal iongezeka katika kundi la waamini siku hiyo.

Ushirika Wa Waamini

42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali. 43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu yalifanywa na mitume.

44 Waamini wote waliishi pamoja na kushirikiana kila kitu walichokuwa nacho kwa pamoja. 45 Waliuza mali zao na vitu waliv yokuwa navyo wakagawiana fedha walizopata, kila mtu akapata kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote waliendelea kuabudu katika Hekalu na kushiriki chakula cha Bwana nyumbani mwao na kula pamoja kwa furaha na shukrani, 47 huku wakimsifu Mungu na kupendwa na watu wote. Na kila siku Bwana alikuwa akiongeza katika kundi lao watu aliokuwa akiwaokoa.

Petro Amponya Mlemavu Kwa Jina La Yesu

Siku moja Petro na Yohana walikwenda Hekaluni saa tisa kwa sala ya adhuhuri. Karibu na mlango uitwao Mzuri, palikuwa na mtu aliyekuwa amelemaa tangu kuzaliwa. Kila siku huyo mlemavu aliwekwa karibu na lango la Hekalu akawa akiomba fedha kwa watu waliokuwa wakiingia ndani ya Hekalu. Alipowaona Petro na Yohana wakielekea Hekaluni, aliwaomba wampe cho chote. Wakamkazia macho, kisha Petro akamwambia, “Tuangalie!” Akawakodolea macho akitazamia kupata kitu kutoka kwao.

Lakini Petro akamwambia, “Sina fedha wala dhahabu za kukupa, lakini nitakupa kile nilicho nacho. Kwa jina la Yesu wa Nazareti nakuamuru, tembea!” Petro akamshika yule mtu mkono, akamwinua, akasimama kwa miguu yake mwenyewe. Mara miguu na viungo vyake vikapata nguvu. Akaruka juu, akasimama, akaingia Hekaluni pamoja na Petro na Yohana, huku akirukaruka na kumsifu Mungu. Watu wote walimwona akitembea na kumsifu Mungu 10 wakam tambua kuwa ni yule mlemavu aliyekuwa akiketi nje ya Hekalu penye lango akiomba omba. Wakashangaa mno kuhusu maajabu yaliyomtokea.

Petro Anashuhudia Kuwa Yesu Aponya

11 Yule mtu aliyeponywa alipokuwa bado anawang’ang’ania Petro na Yohana, watu wakawakimbilia mpaka kwenye ukumbi wa Sule mani wakiwa wamejawa na mshangao.

12 Petro alipoona watu wamekusanyika aliwaambia, “Watu wa Israeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao? Mnadhani ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemwezesha mtu huyu kutembea? 13 Sivyo! Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo na wa baba zetu amemtukuza mtumishi wake Yesu kwa muujiza huu. Ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato ijapokuwa Pilato alitaka kufuta mashtaka na kumwachilia. 14 Ninyi mlimkataa aliyekuwa Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 15 Hivyo mkamwua aliye chanzo cha Uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Sisi ni mashahidi wa mambo haya. 16 Imani katika jina la Yesu imempa nguvu huyu mtu ambaye mnamwona na kumfahamu. Ni kwa jina la Yesu na imani inay opatikana kwake ambayo imemponya huyu mtu kabisa, kama ninyi wenyewe mnavyoona.

17 “Na sasa ndugu zangu, najua ya kuwa mambo mliyomtendea Yesu, ninyi na viongozi wenu, mliyafanya kwa kutokujua. 18 Lakini Mungu alikuwa ametabiri kwa njia ya manabii wake wote kwamba Kristo angeteswa, na hivi ndivyo alivyotimiza utabiri huo. 19 Kwa hiyo tubuni mumgeukie Mungu, ili azifute dhambi zenu, 20 na mpate nguvu za kiroho kutoka kwa Bwana. Naye atampeleka Kristo, yaani Yesu, ambaye alichaguliwa tangu awali kwa ajili yenu. 21 Yeye hana budi kukaa mbinguni mpaka wakati Mungu ataka pofanya kila kitu kuwa kipya tena, kama alivyotamka tangu zamani, kwa kupitia kwa manabii wake watakatifu. 22 Kama Musa alivy osema, ‘Bwana Mungu atawateulia nabii kati ya ndugu zenu kama alivyoniteua mimi. Mtamtii huyo kwa kila jambo atakalowaambia. 23 Mtu ye yote ambaye hatamsikiliza huyo nabii, atatengwa daima na watu wake na kuangamizwa.’

24 “Manabii wote tangu wakati wa Samweli na kuendelea pia walitabiri kuhusu siku hizi. 25 Ninyi ni wana wa manabii na wa ile ahadi ambayo Mungu aliwapa baba zenu, alipomwambia Abrahamu, ‘Kutokana na uzao wako familia zote ulimwenguni zitabarikiwa.’ 26 Mungu alipomfufua mtumishi wake alimtuma kwenu kwanza ili awaletee baraka kwa kuwawezesha kuacha uovu wenu.”

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica