Beginning
Mfano Wa Abrahamu
4 Tusemeje basi kuhusu baba yetu Abrahamu? Yeye alijifunza nini? 2 Ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, basi anacho kitu cha kujivunia, lakini si mbele za Mungu. 3 Maandiko yanase maje? “Abrahamu alimwamini Mungu na kwa ajili ya imani yake aka hesabiwa haki.”
4 Mtu akifanya kazi, mshahara wake hauhesabiwi kuwa ni zawadi bali ni haki yake. 5 Lakini kwa mtu ambaye hakufanya kazi ila amemtegemea Mungu anayewahesabia haki waovu, imani yake inahesabiwa kuwa haki. 6 Daudi pia ana maana hiyo hiyo anapoongea juu ya baraka apatazo mtu ambaye Mungu amemhesabia haki pasipo kutenda lo lote: 7 “Wamebarikiwa wale ambao makosa yao yamesame hewa, ambao dhambi zao zimefunikwa. 8 Amebarikiwa mtu ambaye Bwana hamhesabii dhambi zake.”
Haki Kabla Ya Tohara
9 Je, baraka hii anayosema Daudi ni ya wale waliotahiriwa tu au pia ni ya wale wasiotahiriwa? Tunasema kwamba imani ya Abra hamu ilihesabiwa kama haki. 10 Je, hii ilitokea wakati gani? Je, ilikuwa ni kabla au baada ya kutahiriwa kwake? Haikuwa baada, ila kabla hajatahiriwa. 11 Na alipewa tohara kama alama na mhuri wa haki aliyoipokea kwa imani hata kabla ya kutahiriwa. Shabaha ya Mungu ilikuwa kwamba Abrahamu awe baba ya wote wenye imani ambao bado hawajatahiriwa ili wao pia wahesabiwe haki. 12 Pia yeye ni baba wa wale waliokwisha kutahiriwa ambao si kwamba wametahiriwa tu, bali pia wanafuata mfano wa imani aliyokuwanayo baba yetu
Haki Haipatikani Kwa Sheria
13 Ahadi ambayo Mungu alimpa Abrahamu na kizazi chake, kwamba ataurithi ulimwengu, haikutolewa kwa kuwa Abrahamu alitii sheria lakini ni kwa sababu alikuwa na imani, na Mungu akaihesabu imani yake kuwa ni haki. 14 Ikiwa wafuatao sheria tu ndio wata kaopewa urithi ulioahidiwa na Mungu, basi imani si kitu na ahadi hiyo haina thamani. 15 Kwa maana sheria huleta ghadhabu ya Mungu na ambapo hakuna sheria basi hakuna makosa.
16 Ndio maana ahadi hiyo ilitolewa kwa msingi wa imani, ili ipatikane bure kwa neema na ithibitishwe kwa vizazi vyote vya Abrahamu, si wale tu walio na sheria, bali pia na wale wenye imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sote. 17 Kama ilivyoandikwa: “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Yeye ni baba yetu mbele za Mungu aliyemwamini. Mungu ambaye ana wapa wafu uhai na ambaye huamuru vitu ambavyo havipo viwepo.
Mfano Wa Imani Ya Abrahamu
18 Ijapokuwa ilionekana kama matumaini ya Ibrahimu yalikuwa ya bure, yeye alimtumaini na kumwamini Mungu na kwa kufanya hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kama alivyokuwa ameahidiwa kwamba, “Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.” 19 Ijapokuwa mwili wake hau kuwa tena na uwezo wa kuzaa, alikuwa na umri upatao miaka mia moja na Sara alishapita umri wa kuzaa, imani yake haikufifia. 20 Abrahamu hakuacha kuamini wala hakuwa na mashaka juu ya ahadi ya Mungu. Imani yake ilimtia nguvu, akamtukuza Mungu, 21 akiwa na hakika kabisa kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kutimiza ali loahidi. 22 Ndio sababu imani yake, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.” 23 Maneno haya, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki,” hay akuandikwa kwa ajili yake peke yake 24 bali kwetu pia. Tutahe sabiwa haki sisi tunaomwamini Mungu aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka kwa wafu. 25 Yesu aliuawa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuliwa ili tuhesabiwe haki.
Kuwa Na Amani Na Mungu
5 Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa imani, tuna amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. 2 Kwa kupitia kwake tumepata njia ya kufikia neema hii ambayo inatuwezesha kusimama imara, tukifurahia tumaini letu la kushiriki utukufu wa Mungu. 3 Zaidi ya hayo, pia tunafurahia mateso yetu kwa sababu tunafahamu kuwa mateso huleta subira; 4 na subira huleta uthabiti wa moyo; na uthabiti wa moyo hujenga tumaini. 5 Tukiwa na tumaini hatuwezi kukata tamaa kwa sababu Mungu amekwisha kumimina upendo wake mioyoni mwetu kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye ni zawadi tuliyopewa na Mungu.
6 Tulipokuwa tungali wanyonge, wakati aliochagua Mungu, Kristo aliwafia wenye dhambi. 7 Ni vigumu sana kwa mtu kujitolea kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa yawezekana mtu akajitolea kufa kwa ajili ya mtu mwema. 8 Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo ali kufa kwa ajili yetu.
9 Basi, kwa kuwa tumekwisha kuhesabiwa haki kwa damu yake, bila shaka atatuokoa kutoka katika ghadhabu ya Mungu. 10 Kwa kuwa kama tulipokuwa maadui wa Mungu tulipatanishwa kwa kifo cha Mwanae, bila shaka sasa kwa kuwa tumepatanishwa, tutaokolewa kwa uzima wake. 11 Si hivyo tu, bali pia tunamfurahia Mungu katika Bwana wetu Yesu Kristo ambaye kwa ajili yake tumepokea upatanisho wetu.
Adamu Alileta Kifo, Yesu Ameleta Uzima
12 Kwa hiyo kama vile ambavyo dhambi iliingia ulimwenguni kupitia kwa mtu mmoja, na dhambi ikaleta kifo, na kwa njia hiyo kifo kikawajia watu wote kwa kuwa wote walitenda dhambi -
13 kwa maana kabla sheria haijatolewa dhambi ilikuwepo ulimwenguni. Lakini dhambi haihesabiwi ambapo hakuna sheria. 14 Hata hivyo tangu wakati wa Adamu hadi wakati wa Musa, kifo kiliwatawala watuwote hata wale ambao dhambi zao hazikuwa kama uasi wa Adamu. Adamu alikuwa mfano wa yule ambaye angalikuja. 15 Lakini zawadi iliyotolewa bure haiwezi kulinganishwa na ule uasi. Kwa maana ikiwa watu wengi walikufa kwa sababu ya uasi wa mtu mmoja, basi neema ya Mungu na zawadi iliyotolewa kwa ajili ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imemiminika kwa wingi zaidi kwa watu wengi. 16 Pia zawadi ya Mungu sio kama matukio ya ile dhambi ya mtu mmoja. Kwa maana hukumu iliyotokana na uasi huo ilileta laana, lakini zawadi iliyopatikana bure baada ya dhambi nyingi, inaleta haki ya Mungu. 17 Na ikiwa kutokana na uasi wa mtu mmoja kifo kilitawala kupitia huyo mtu mmoja, wale wanaopokea wingi wa neema na zawadi ya bure ya kuhesabiwa haki, watatawala zaidi sana katika maisha kwa ajili ya huyo mtu mmoja, Yesu Kristo. 18 Kwa hiyo, kama vile uasi wa mtu mmoja ulivyoleta hukumu kwa watu wote, hali kadhalika, tendo la haki la mtu mmoja linawafanya watu wote waachiliwe huru na kupewa uzima. 19 Na kama vile ambavyo watu wengi walifanywa kuwa wenye dhambi kwa ajili ya kutokutii kwa mtu mmoja, vivyo hivyo wengi watahesabiwa haki na Mungu kwa ajili ya utii wa mtu mmoja.
20 Sheria ililetwa ili dhambi iongezeke. Lakini dhambi ili poongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21 Kama vile ambavyo dhambi ilitawala kwa njia ya kifo, vivyo hivyo neema ya Mungu iweze kutawala kwa njia ya haki, ikileta uzima wa milele katika Yesu
Uhai Katika Kristo
6 Tusemeje basi? Tuendelee kutenda dhambi ili neema izidi kuongezeka? 2 Hata kidogo! Itawezekanaje sisi tuliokufa kwa mambo ya dhambi, tuendelee tena kuishi humo? 3 Au hamfahamu kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? 4 Kwa hiyo tulikufa na kuzikwa naye kwa njia ya ubatizo ili kama vile Kristo alivyofufuliwa kutoka kwa wafu kwa nguvu na utukufu wa Baba, sisi pia tupate kuishi maisha mapya.
5 Kwa maana ikiwa tumeunganika naye katika kifo chake, basi tutaunganika naye katika kufufuka kwake. 6 Tunafahamu kwamba mwili wetu wa asili ulisulubiwa msalabani pamoja na Kristo ili mwili wetu wa dhambi uharibiwe kabisa na tusiwe tena watumwa wa dhambi. 7 Kwa maana mtu anapokufa anakuwa huru na mambo ya dhambi. 8 Lakini ikiwa tumekufa na Kristo, tunaamini kwamba pia tutaishi pamoja naye. 9 Kama tujuavyo, Kristo alikwisha kufufu liwa kutoka kwa wafu kwa hiyo hafi tena; kifo hakina mamlaka juu yake tena. 10 Alikufa kwa ajili ya dhambi mara moja tu, lakini maisha anayoishi anamwishia Mungu.
11 Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kujihesabu kuwa wafu kwa mambo ya dhambi bali hai kwa Mungu mkiwa ndani ya Kristo Yesu.
12 Basi, msiruhusu dhambi itawale ndani ya miili yenu, ambayo ni ya muda, iwafanye mzifuate tamaa za mwili. 13 Msiku bali kutoa sehemu yo yote ya miili yenu itumike kama vyombo vya uovu kutenda dhambi. Bali jitoeni kwa Mungu kama watu waliotolewa kutoka katika kifo wakaingizwa uzimani. Pia toeni sehemu zote za miili yenu zitumike kama vyombo vya haki. 14 Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu kwa sababu hamtawaliwi na sheria bali mnatawaliwa na neema. Watumwa Wa Haki
15 Tufanyeje basi? Tuendelee kutenda dhambi kwa kuwa hatutawa liwi na sheria bali tuko chini ya neema? La , sivyo! 16 Hamfahamu kuwa kama mkijitoa kumtumikia mtu na kumtii kama watumwa basi mnakuwa watumwa wa huyo mnayemtii? Mnaweza kuwa watumwa wa dhambi ambayo matokeo yake ni mauti au mnaweza kuwa watumwa wa utii ambao huleta haki. 17 Lakini Mungu ashukuriwe kwa kuwa ninyi ambao mlikuwa watumwa wa dhambi mmetii kwa moyo wote mafundi sho mliyopewa. 18 Mmewekwa huru, mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa haki. 19 Ninatumia mifano ya kibinadamu kwa sababu ya upungufu wenu wa hali ya asili. Kama mlivyokuwa mkiitoa miili yenu kwa ajili ya mambo ya uchafu na uovu uliokuwa ukiongezeka zaidi na zaidi, sasa itoeni miili yenu itumike kwa ajili ya haki na utakatifu.
20 Mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa hamtawaliwi na haki. 21 Lakini mlipata faida gani kwa mambo hayo ambayo sasa mnayaonea aibu? Mwisho wa mambo hayo ni kifo. 22 Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru kutokana na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakaso, na hatimaye, uzima wa milele. 23 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Mkristo Hafungwi Na Sheria
7 Ndugu zangu, kwa kuwa sasa ninasema na wale wanaoifahamu sheria, bila shaka mnaelewa kwamba mtu akifa hafungwi tena na sheria. 2 Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa hufungwa kisheria kwa mumewe wakati wote mumewe akiwa hai. Lakini mumewe akifa mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa. 3 Endapo mwanamke huyo ataishi namwanaume mwingine wakati mumewe yu hai, ataitwa mzinzi. Lakini mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na she ria ya ndoa, na akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.
Kazi Ya Sheria
4 Kadhalika ndugu zangu, ninyi pia mmekufa kuhusu maagizo ya sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili tumzalie Mungu matunda. 5 Tulipokuwa tukitawaliwa na hali yetu ya dhambi, tamaa zetu za dhambi zikiwa zinachochewa na sheria, zilikuwa zikifanya kazi katika miili yetu, tukatumikishwa katika huduma ya dhambi ambayo matunda yake ni kifo. 6 Lakini sasa tumekuwa huru kutoka katika kifungo cha sheria kwa kuwa tumekufa kuhusu yale mambo yaliyotu funga, ili tuhudumu katika maisha mapya ya Roho na wala si katika ile njia ya zamani ya sheria iliyoandikwa.
7 Tusemeje basi? Kwamba sheria ni dhambi? La, sivyo! Kama isingekuwapo sheria, nisingalifahamu dhambi ni nini. Hakika nisi ngalijua tamaa ni nini kama sheria haikusema, “Usitamani.” 8 Lakini dhambi ilipata nafasi katika amri hii ikazaa ndani yangu kila aina ya tamaa. Kwa maana pasipo sheria, dhambi ime kufa. 9 Kabla ya kuwapo sheria, nilikuwa hai pasipo sheria, lakini amri ilipowasili dhambi nayo ilikuwa hai, nami nikafa. 10 Ile amri iliyokusudiwa kuleta uzima, ilileta kifo. 11 Dhambi ilipata nafasi katika amri, ikanidanganya, na kwa kutumia amri, ikaniletea kifo.
12 Kwa hiyo sheria yenyewe ni takatifu na amri ni takatifu, na ya haki, tena ni njema.
13 Je, hii ina maana kwamba sheria ambayo ni njema ilinile tea kifo? La, sivyo. Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, iliniletea kifo kwa njia ya sheria ambayo ni nzuri; kusudi kwa njia ya sheria, dhambi ionekane kuwa mbaya kabisa.
Mgongano Kati Ya Mwili Na Roho
14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya. 16 Kwa hiyo kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, hii ina maana kwamba nakubali kuwa sheria ni njema. 17 Basi, kwa kweli si mimi hasa nitendaye lile nisilolipenda bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 18 Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna wema wo wote ndani yangu mimi, yaani katika mwili wangu wa asili. Ingawa nina nia ya kutenda lililo jema, lakini ninashindwa kulitenda. 19 Sitendi lile jema nipendalo bali lile ovu nisilopenda, ndilo nitendalo. 20 Basi kama ninafanya lile nisilopenda kufanya, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
21 Kwa hiyo imekuwa kama ni sheria: kila ninapotaka kufanya jambo jema, jambo ovu hujitokeza. 22 Kwa maana ndani yangu ninaifurahia sheria ya Mungu. 23 Lakini ninaona kuna sheria nyin gine mwilini mwangu inayopingana na ile sheria ninayoikubali akilini mwangu. Sheria hii inanifanya kuwa mateka wa sheria ya dhambi ambayo inafanya kazi mwilini mwangu.
24 Ole wangu, mimi mnyonge! Ni nani atakayeniokoa na huu mwili wa kifo? 25 Ninamshukuru Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa hiyo basi, mimi kwa moyo wangu, ninaitumikia sheria ya Mungu, lakini kwa mwili wangu wa asili ninaitumikia sheria ya dhambi.
Copyright © 1989 by Biblica