Beginning
1 Kutoka kwa Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo na mtume niliyecha guliwa na kuitwa kuhubiri Habari Njema ya Mungu. 2 Habari hii aliiahidi tangu zamani kwa njia ya manabii wake katika Maandiko matakatifu.
3 Habari hii njema ni kuhusu Mwana wa Mungu ambaye kimwili alizaliwa katika ukoo wa Daudi, 4 na ambaye alidhihiri shwa kuwa Mwana wa Mungu kwa uwezo wa Roho wa utakatifu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Yeye ndiye Yesu Kristo Bwana wetu, 5 ambaye kutoka kwake, na kwa ajili yake, tumepokea neema na agizo la kuwaongoza watu wa mataifa yote wasiomjua Mungu, wapate kumwamini na kumtii. 6 Ninyi pia ni miongoni mwa watu walioitwa kuwa wafuasi wa Yesu Kristo.
7 Basi, nawatakieni ninyi nyote mlioko huko Roma, ambao ni wapendwa wa Mungu mlioitwa muwe watakatifu, neema na amani ito kayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Maombi Na Shukrani
8 Kwanza kabisa, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inatangazwa duniani kote. 9 Mungu ninayemtumikia kwa moyo wangu wote ninapo hubiri Habari Njema ya Mwanae, anajua jinsi ninavyowakumbuka siku zote 10 katika sala zangu kila ninapoomba. Namwomba Mungu, akipenda, hatimaye sasa nipate nafasi ya kuja kwenu. 11 Ninata mani sana kuwaona ili niwagawie zawadi ya kiroho ya kuwaima risha, 12 yaani tuimarishane: mimi nitiwe moyo kwa imani yenu na ninyi mtiwe moyo kwa imani yangu.
13 Ndugu zangu, napenda mfahamu kwamba mara nyingi nimeku sudia kuja kwenu, ingawa mpaka sasa nimezuiliwa. Ningependa kupata mavuno ya waamini kati yenu kama nilivyofanikiwa kupata waamini kati ya watu wa mataifa mengine.
14 Ninawajibika kwa watu wote, Wagiriki na wasiokuwa Wagi riki; wenye elimu na wasiokuwa na elimu. 15 Ndio maana ninata mani sana kuhubiri Injili kwenu ninyi pia mlioko Roma.
16 Mimi siionei aibu Injili kwa maanani nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza, na watu wa mataifa mengine pia. 17 Kwa maana Habari hii Njema inaonyesha wazi haki inayotoka kwa Mungu. Haki hii hupatikana kwa imani tangu mwanzo hadi mwisho. Kama ilivyoandikwa: “Wenye haki wataishi kwa imani.”
Ghadhabu Ya Mungu Kwa Wanadamu
18 Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wa wanadamu ambao kwa uovu wao wanauficha ukweli usijulikane. 19 Kwa maana yote yanayoweza kujulikana kumhusu Mungu ni dhahiri kwao kwa sababu Mungu mwenyewe ameyaweka wazi. 20 Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uwezo wake wa milele na Uungu wake, umedhihirika wazi wazi kutokana na vitu alivyoviumba. Kwa hiyo watu hawana kisingizio.
21 Ingawa walimjua Mungu, hawakumpa heshima na utukufu anaostahili wala kumshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao zilizopumbaa zikatiwa giza. 22 Wakijidai kuwa ni werevu, wakawa wajinga. 23 Wakauacha utukufu wa Mungu aishiye milele wakageukia sanamu zinazofanana na mwanadamu ambaye hufa, na ndege na wanyama na viumbe vitambaavyo.
24 Kwa hiyo, Mungu aliwaacha waendelee kufuata tamaa mbaya za mioyo yao na kutenda matendo ya unajisi nakufanyiana mambo ya aibu katika miili yao. 25 Hii ni kwa sababu walikataa ukweli ku husu Mungu wakaamua kuamini uongo; wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba ahimidiwaye milele! Amina.
26 Kwa hiyo, Mungu aliwaachia wafuate tamaa zao za aibu. Hata wanawake wao waliacha matumizi ya asili ya maumbile yao wakatumia miili yao isivyokusudiwa. 27 Hali kadhalika wanaume waliacha uhusiano wa asili kati ya waume na wake wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume walifanyiana mambo ya aibu, nao waka pata katika miili yao adhabu waliyostahili kama matokeo ya uovu wao.
28 Zaidi ya hayo, kwa sababu walikataa kumtambua Mungu, yeye aliwaacha katika nia zao za upotovu watende mambo yasiyosta hili kutendwa. 29 Wamejawa na udhalimu wa kila namna, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na husuda, uuaji, fitina, hadaa, nia mbaya. Wao pia ni wasengenyaji, 30 wasingiziaji, wanaomchukia Mu ngu, wajeuri, wenye kiburi na majivuno; wenye hila, wasiotii wazazi wao; 31 niwajinga, wasioamini, wasio na huruma nawaka tili. 32 Ingawa wanafahamu sheria ya Mungu kwamba watu wanaoishi maisha ya namna hii wanastahili mauti, bado wanaendelea kutenda mambo haya na kuwasifu wengine wafanyao kama wao.
Hukumu Ya Mungu
2 Kwa hiyo huna udhuru wo wote, hata ukiwa nani, unapowahu kumu wengine. Kwa maana unapowahukumu wengine unajihukumu mwe nyewe, kwa kuwa wewe uliye hakimu unafanya mambo hayo hayo. 2 Tunajua kwamba hukumu ya Mungu huwafikia kwa halali wote wanaotenda mambo haya. 3 Je, wewe uliye binadamu tu, unapowahuku mu watu wanaofanya mambo hayo na huku wewe mwenyewe pia unafanya hayo hayo, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? 4 Au labda unad harau wingi wa huruma, uvumilivu na subira ya Mungu, ukasahau kwamba wema wake una shabaha ya kukufanya utubu?
5 Lakini kwa sababu ya ugumu na ukaidi wa moyo wako usioku bali kutubu, unajiwekea ghadhabu kwa siku ile ambapo ghadhabu ya Mungu na hukumu yake ya haki itadhihirishwa. 6 Siku hiyo, Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. 7 Wale ambao hutenda wema wakati wote na kutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyo haribika, Mungu atawapa uzima wa milele. 8 Lakini wote watafu tao kujinufaisha, wanaokataa kweli na kufuatauovu, watapokea ghadhabu na hasira ya Mungu. 9 Kwa maana kila binadamu atendaye uovu atapata mateso na shida, kuanzia kwa Myahudi na kisha kwa mtu wa mataifa mengine. 10 Lakini Mungu atawapa utukufu, heshima na amani wote watendao mema; Wayahudi kwanza na kisha watu wa mataifa mengine. 11 Kwa maana Mungu hana upendeleo.
12 Watu wote waliotenda dhambi pasipokuwa na sheria ya Musa wataangamia pasipo sheria; na wale wote waliotenda dhambi chini ya sheria ya Musa watahukumiwa kwa sheria iyo hiyo. 13 Kwa maana wanaohesabiwa haki mbele ya Mungu si wale wanaosikia bali ni wal ewanaotii maagizo ya sheria. 14 Watu wa mataifa mengine ambao hawana sheria ya Musa, wanapoamua kutenda yale ambayo yameagizwa na sheria kwa kuongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa wamejiwekea sheria, ingawa hawana sheria ya Musa. 15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea. 16 Kwa hiyo, kama Habari Njema ninay ohubiri inavyosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile ambayo Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, atayahukumu mawazo ya siri ya wanadamu.
Wayahudi Na Sheria Ya Musa
17 Na wewe je? Wewe unayejiita Myahudi: unaitegemea sheria ya Musa na kujisifia uhusiano wako na Mungu; 18 unajua mapenzi ya Mungu na unatambua lililo bora kutokana na hiyo sheria. 19 Kama unatambua kuwa wewe ni kiongozi wa vipofu na mwanga kwa wale walioko gizani; 20 mkufunzi wa wajinga na mwalimu wa watoto wachanga, kwa kuwa una hakika kwamba ndani ya hiyo sheria mna maarifa na kweli yote: 21 wewe unayewafundisha wengine, mbona hujifunzi mwenyewe? Wewe unayehubiri kwamba watu wasiibe, wewe huibi? 22 Wewe unayewaambia watu wasizini, wewe huzini? Wewe uchukiaye miungu ya sanamu, huibi katika mahekalu? 23 Wewe unayejisifia sheria, humwaibishi Mungu kwa kuvunja sheria? 24 Kwa maana Maandiko yanasema, “Kwa ajili yenu ninyi Wayahudi, jina la Mungu linatukanwa miongoni mwa mataifa ya watu wasiom jua Mungu.”
25 Kutahiriwa kuna thamani tu iwapo unatii sheria, lakini kama unavunja sheria, umekuwa kama hukutahiriwa. 26 Kwa hiyo kama watu ambao hawakutahiriwa wanatimiza maagizo ya she ria, je, Mungu hatawahesabu kuwa kama waliotahiriwa? 27 Ndipo wale ambao kimwili hawakutahiriwa lakini wanatii sheria watawa hukumu ninyi mlio na Maandiko ya sheria nakutahiriwa lakini mna vunja sheria. 28 Kwamaana Myahudi wa kweli si yule anayeonekana kwa dalili za nje, wala tohara ya kweli si kitu cha kimwili. 29 Myahudi wa kweli ni yule aliye Myahudi kwa ndani, na tohara ya kweli ni jambo la moyoni, jambo la kiroho, wala si la sheria iliyoandikwa. Mtu wa jinsi hii anapata sifa kutoka kwa Mungu, wala si kutoka kwa wanadamu.
Uaminifu Wa Mungu
3 Basi kuna faida gani kuwa Myahudi? Je, kutahiriwa kuna faida yo yote? 2 Ndio, zipo faida nyingi. Kwanza, Mungu aliwaka bidhi Wayahudi maagizo yake. 3 Na hata kama baadhi yao hawaku amini,je, kutokuamini kwao kutamfanya Mungu aache kuwa mwaminifu? 4 Hata kidogo!Mungu ataendelea kuwa wa kweli hata kama kila mwan adamu atakuwa mwongo. Kama ilivyoandikwa katika Maandiko,“Wewe Mungu, uthibitishwe kuwa wahaki katika maneno yako, na mshindi katika hukumu.”
5 Lakini iwapo uovu wetu unadhihirisha wazi kwamba Mungu ni mwenye haki, tusemeje basi? Je, tuseme kuwa Mungu hana haki kutuadhibu? Hapa ninasema kibinadamu. 6 La hasha! Mun gu ana haki kabisa kutughadhibikia! Kama sivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? 7 Mtu anaweza kusema,“Kama uongo wangu unasaidia kuonyesha ukweli wa Mungu na hivyo kudhihirisha utukufu wake, kwa nini basi ninahukumiwa kama mwenye dhambi?” 8 Kwa nini tusiseme, kama wengine wanavyotusingizia kuwa tunasema, “Tutende maovu ili wema udhihirike”? Hakika hukumu wanayoipata ni ya haki.
Wote Wametenda Dhambi
9 Tusemeje basi? Sisi Wayahudi tunayo nafuu yo yote? Hata kidogo! Kama tulivyokwisha kusema, Wayahudi na Wagiriki, wote wanatawaliwa na nguvu ya dhambi. 10 Kama Maandiko yase mavyo:“Hakuna hata mmoja mwenye haki; 11 hakuna hata mmoja mwe nye kuelewa, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu. 1 2Wote wamepotoka na kwa pamoja hawana thamani yo yote; hakuna atendaye mema hata mmoja. 13 Makoo yao ni kama makaburi wazi, wanatumia ndimi zao kudanganya. Kwenye midomo yao mnasumu kama ya nyoka. 14 Vinywa vyao vimejaa laana na ukali. 15 Miguu yao huen da mbio kumwaga damu, 16 njia zote wanazopita huacha uharibifu na huzuni kuu, na 17 wala njia ya amani hawaifahamu. 18 Kumcha Mungu hakupo machonipao.”
Mungu hakupo machonipao.”
19 Basi tunafahamu ya kwamba maagizo yote ya sheria ya Musa yanawahusu wale walio chini ya sheria hiyo. Kusudi la sheria ni kuwafanya watu wote wasiwe na kisingizio na kuuweka ulimwengu wote chini ya hukumu ya Mungu. 20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi.
Haki Kwa Njia Ya Imani
21 Lakini sasa, njia ya Mungu ya kuwahesabia watu haki pasipo sheria, njia ambayo sheria na manabii huishuhudia, imekwisha dhihirishwa. 22 Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa kumwaminiYesu Kristo. Mungu huwatendea hivi watu wote wamwa minio Kristo pasipo kubagua, 23 kwa maana wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; 24 wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kwa ukombozi ulioletwa na Yesu Kristo. 25 Mungu alimtoa awe dhabihu ya upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alifanya hivi ili kuonyesha haki yake, kwani kwa uvumilivu wake hakuziadhibu dhambi za zamani. 26 Pia alifanya hivi ili kuonyesha kwa wakati huu kuwa yeye ni wa haki na kwamba yeye ndiye anayewahesabia haki watu wote wamwaminio Yesu.
Umuhimu Wa Kuwa Na Imani
27 Sasa kujivuna kwetu kuko wapi basi? Hakupo. Je kumeondo lewa kwa msingi gani? Kwa msingi wa kutimiza sheria? La. Kumeon dolewa kwa msingi wa imani. 28 Kwa maana tunasisitiza kwamba mwanadamu anahesabiwa haki kwa njia ya imani na wala si kwa kutenda maagizo ya sheria. 29 Je, Mungu ni Mungu wa Wayahudi peke yao? Je, yeye si Mungu wa watu wa mataifa mengine pia? Ndio, yeye ni Mungu wa watu wa mataifa mengine pia. 30 Basi kwa kuwa Mungu ni mmoja, atawahesabia haki wale waliotahiriwa kutokana na imani yao na wale wasiotahiriwa kutokana na imani yao. 31 Je, ina maana kwamba tunaifuta sheria kwa imani hii? La, sivyo. Kiny ume chake: tunaithibitisha sheria.
Copyright © 1989 by Biblica