Print Page Options Listen to Acts 11-13
Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Matendo Ya Mitume 11-13

Petro Aeleza Alivyotumwa Kwa Mataifa

11 Baadaye mitume na waamini wa sehemu zote za Yudea wakapata habari kwamba watu wasiokuwa Wayahudi nao wamepokea neno la Mungu. Kwa hiyo Petro alipokwenda Yerusalemu, wale waliokuwa wakishikilia sheria ya tohara walimshutumu wakasema, “Kwa nini ulikwenda kwa watu wasiotahiriwa na kula pamoja nao?” Ndipo Petro akaanza kuwaeleza mambo yote yalivyotokea akasema, “Nil ikuwa nikiomba katika mji wa Jopa, nikaona katika ndoto kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kwa ncha zake nne, kutoka mbinguni, nayo ikanifikia. Nilipotazama kwa makini nikaona wanyama wa kila aina, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani. Nikasikia sauti ikiniambia, ‘Amka Petro, chinja, ule!’ Nami nikasema, ‘La, Bwana! Sijawahi kula kitu cho chote kili chokatazwa na sheria zetu.’ Lakini ile sauti kutoka mbinguni ikasema kwa mara ya pili, ‘Usiite kitu cho chote alichokitakasa Mungu kuwa ni uchafu.’ 10 Jambo hili lilitokea mara tatu ndipo vyote vikachukuliwa tena mpaka mbinguni. 11 Wakati huo huo watu watatu waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria wakawasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. 12 Roho akaniambia niende nao bila kusita. Nikaenda nao nikisindikizwa na hawa ndugu sita, tukaingia katika nyumba ya Kornelio. 13 Kornelio akatuambia jinsi malaika alivyomtokea akamwambia, ‘Tuma watu Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. 14 Yeye anao ujumbe utakaokuokoa wewe na wote walio nyum bani mwako.’ 15 Nami nilipokuwa nikisema nao, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama alivyotushukia sisi mwanzoni. 16 Nami nikakumbuka jinsi Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’ 17 Basi kwa kuwa Mungu ndiye aliyewapa hawa watu karama ile ile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu, mimi ni nani hata nimpinge Mungu?” 18 Nao waliposikia maneno haya hawakuwa na la kusema. Wakamsifu Mungu, wakasema, “Mungu amewapa watu wa mataifa nafasi ya kutubu na kupokea uzima wa milele.’ ’

Kanisa Laenea Antiokia

19 Wale waamini waliotawanyika kutoka Yerusalemu wakati wa mateso yaliyotokana na kifo cha Stefano, walisafiri hadi Foinike na Kipro na Antiokia. Wakawa wakihubiri Habari Njema kwa Wayahudi peke yake. 20 Lakini baadhi yao walikwenda Antiokia wakitokea Kipro na Kirene. Wakawaambia Wagiriki Habari Njema za Bwana Yesu. 21 Roho wa Bwana alikuwa pamoja nao kwa hiyo watu wengi wakaamini na kumgeukia Bwana. 22 Habari hizi zilipowafikia vion gozi wa kanisa huko Yerusalemu, walimtuma Barnaba aende Antiokia. 23 Alipofika akaona jinsi Mungu alivyokuwa akiwabariki watu kwa neema yake, alifurahi sana akawatia moyo waendelee kwa juhudi kuwa waaminifu kwa Bwana. 24 Barnaba alikuwa mtu mwema aliyejawa Roho Mtakatifu, mwenye imani kuu; na watu wengi waliongoka wakam wamini Bwana. 25 Kisha Barnaba akasafiri kwenda Tarso kumtafuta Sauli. 26 Alipompata akaja naye mpaka Antiokia. Na wote wawili wakakaa huko kwa mwaka mzima, wakiwafundisha wengi walioamini katika kanisa la Antiokia. Hapo Antiokia ndipo waamini waliitwa ‘Wakristo’ kwa mara ya kwanza.

27 Wakati huu manabii walitoka Yerusalemu wakaenda Antiokia. 28 Na mmoja wao, jina lake Agabo, akasimama katika mkutano aka tabiri kwa uweza wa Roho kwamba pangetokea njaa kubwa dunia nzima. Njaa hiyo ilitokea wakati Klaudio alipokuwa mtawala. 29 Waamini wakaamua kwamba kila mtu, kulingana na uwezo alio nao, atoe msaada upelekwe kwa ndugu waliokuwa wanaishi Yudea. 30 Wakafanya hivyo, na misaada ikapelekwa na Barnaba na Sauli kwa wazee wa kanisa.

Malaika Amtoa Petro Gerezani

12 Wakati huu mfalme Herode aliwatesa vikali baadhi ya waamini katika kanisa. Akaamuru Yakobo, ndugu yake Yohana, auawe kwa upanga. Alipoona kuwa kitendo hicho kimewapendeza Wayahudi, akaamuru Petro akamatwe. Hii ilitokea wakati wa Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu. Baada ya kumkamata Petro walimweka jela chini ya ulinzi wa vikundi vinne vya askari, kila kikundi kikiwa na askari wanne. Herode alikuwa amepanga kumtoa Petro mbele ya Wayahudi baada ya Pasaka. Kwa hiyo Petro akawekwa gerezani; lakini kanisa lilikuwa likimwombea kwa Mungu kwa bidii. Usiku ule ambao Herode alikuwa ameamua kumtoa kwa watu, Petro alikuwa amelala kati ya askari wawili. Alikuwa amefungwa kwa minyororo miwili, na askari wengine walikuwa wakilinda nje ya lango la gereza. Mara malaika wa Bwana akatokea, na mwanga ukamulika ndani ya chumba. Yule malaika akampiga Petro ubavuni akamwamsha, akisema, “Haraka! Amka!” Na mara ile minyororo ikaanguka toka mikononi mwa Petro. Yule malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Kisha akamwambia, “Vaa koti lako unifuate.” Petro alitoka mle gere zani akifuatana na malaika. Hakujua wakati huo kuwa yaliyokuwa yakitokea yalikuwa kweli. Alidhani alikuwa katika ndoto. 10 Wal ipita kituo cha askari wa kwanza, na kituo cha askari wa pili, ndipo wakafika katika lango la chuma la kutokea kuelekea mjini. Lango likafunguka lenyewe, wakatoka nje wakaelekea katika bara bara mojawapo . Mara yule malaika akamwacha Petro. 11 Ndipo Petro alipopata fahamu sawa sawa, akasema, “Sasa nina hakika ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake aniokoe kutoka kwa Herode na maovu yote ambayo Wayahudi walikuwa wamekusudia kunitendea.”

12 Baada ya kutambua alipokuwa, Petro alikwenda nyumbani kwa Maria, mama yake Yohana Marko, ambako waamini wengi walikuwa wamekutana kwa maombi. 13 Petro alipobisha hodi mlangoni, mfany akazi msichana aitwaye Roda, akaja kumfungulia.

Lakini ali potambua sauti ya Petro, alirudi mbio kwa furaha kuwaambia wen gine kuwa Petro yuko nje, hata akasahau kumfungulia . 15 Wakam wambia yule msichana, “Una kichaa!” Lakini yeye alisisitiza kwamba ilikuwa ni kweli amesikia sauti ya Petro. Wakasema, “Ni malaika wake.” 16 Wakati huo Petro aliendelea kugonga mlangoni; nao walipofungua mlango wakamwona Petro, walistaajabu sana. 17 Lakini yeye aliwaashiria wakae kimya, akawaeleza jinsi Bwana alivyomtoa jela. Akawaambia, “Waelezeni Yakobo na ndugu wengine habari hizi.” Akaondoka akaenda sehemu nyingine. 18 Kulipopam bazuka kukawa na hekaheka huko gerezani. Askari wakawa wanauli zana kuhusu yaliyompata Petro. 19 Herode akaamuru msako ufanyike lakini waliposhindwa kumpata Petro, aliwahoji wale askari walinzi kisha akatoa amri hao askari wauawe. Basi Herode akatoka Yudea akaenda Kaisaria, akakaa huko.

Kifo Cha Herode

20 Herode alikuwa amekasirishwa sana na watu wa Tiro na Sidoni. Watu wa miji hiyo miwili wakaungana pamoja wakapeleka wajumbe wakaonane na Herode. Wajumbe hao wakapata kibali cha Blasto, mtumishi mwaminifu wa Mfalme Herode, ili waonane na mfalme kutaka amani kwa kuwa miji hiyo ilipata chakula chake kutoka katika milki ya mfalme. 21 Siku ya hao wajumbe kumwona mfalme ilipofika, Herode alivaa mavazi rasmi ya kifalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi akaanza kutoa hotuba. 22 Alipokuwa akihutubu watu walimshangilia, wakapiga kelele wakisema, “Hii ni sauti ya Mungu! Sio sauti ya mwanadamu!” 23 Mara malaika wa Bwana akampiga Herode; akaliwa na funza akafa kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. 24 Lakini neno la Mungu liliendelea kuenea na waamini wakaongezeka sana. 25 Barnaba na Sauli walipomaliza kazi yao walirudi Yerusalemu wakiwa pamoja na Yohana Marko.

Barnaba Na Sauli Wachaguliwa Kwa Kazi Maalumu

13 Katika Kanisa la Antiokia Walikuwako manabii na waalimu wafuatao: Barnaba, Simeoni aitwaye mtu mweusi, Lukio kutoka Kirene, Manaeni aliyekuwa nduguye mfalme Herode, na Sauli. Wal ipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu aliwaambia, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi maalumu niliyowaitia.” Kwa hiyo baada ya kufunga na kuomba, waliwawekea mikono Sauli na Barnaba wakawaaga.

Barnaba Na Sauli Waenda Kipro

Barnaba na Sauli wakaongozwa na Roho Mtakatifu wakaenda mpaka Seleukia, na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro . Nao walipowasili katika mji wa Salami, walihubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Walikuwa wameongozana na Yohana Marko kama msaidizi wao.

Bar-Yesu Alaaniwa Na Mitume

Baada ya kuhubiri sehemu zote za kisiwa cha Kipro walifika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, aitwaye Bar-Yesu. Bar-Yesu alikuwa rafiki wa liwali ait waye Sergio Paulo, mtu mwenye hekima. Liwali huyu alituma Sauli na Barnaba waletwe kwake kwa sababu alitaka kusikia Neno la Mungu. Lakini yule mchawi ambaye jina lake kwa Kigiriki ni Elima, alijaribu kuwapinga Barnaba na Sauli na kumshawishi yule liwali asiwasikilize. Ndipo Sauli ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho yule mchawi, 10 akamwambia, “Wewe mwana wa Shetani! Wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa hila, na uovu. Je, utaacha lini kujaribu kugeuza kweli ya Bwana kuwa uongo? 11 Na sasa tazama mkono wa Bwana uko juu yako kukuadhibu, nawe utakuwa kipofu; hutaona kwa muda.” Na mara ukungu na giza likafunika macho ya Elima akaanza kutanga-tanga akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. 12 Yule liwali alipoona mambo haya, akaamini, kwa maana alistaajabishwa na mafundisho ya Bwana.

13 Basi Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo mpaka Perge huko Pamfilia. Yohana Marko akawaacha huko akarejea Yerusalemu. 14 Lakini Barnaba na Paulo wakaendelea hadi Antiokia, mji ulioko katika jimbo la Pisidia. Na siku ya sabato waliingia ndani ya sinagogi wakaketi . 15 Baada ya kusoma kutoka katika vitabu vya sheria za Musa na Maandiko ya manabii, viongozi wa lile sinagogi waliwatumia ujumbe pale walipokaa wakisema, “Ndugu, kama mna neno la mafundisho kwetu, njooni mkaliseme watu walisikie. 16 Paulo akasimama akawapungia mkono akasema, “Watu wa Israeli, na ninyi wote mnaomcha Mungu, sikilizeni. 17 Mungu wa taifa la Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kuwa taifa kubwa wakati walipoishi katika nchi ya Misri na akawatoa katika utumwa wa Misri kwa nguvu za ajabu. 18 Kwa muda wa miaka arobaini aliwavu milia walipokuwa jangwani. 19 Na baada ya kuwaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao kwa muda wa miaka mia nne na hamsini. 20 Kisha akawapa Waamuzi wakatawala mpaka wakati wa nabii Samweli. 21 Hatimaye wakataka wawe na mfalme. Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, wa kabila la Benjamini, akawatawala kwa miaka arobaini. 22 Mungu akamwondoa Sauli katika ufalme, akamta waza Daudi mwana wa Yese, akamshuhudia akisema, ‘Nimempata Daudi mwana wa Yese, ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Yeye atafanya mapenzi yangu .’ 23 Katika uzao wa Daudi, Mungu amewaletea Wais raeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi. 24 Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli. 25 Kabla Yohana Mbatizaji hajamaliza kazi yake, alisema, ‘Mna nidhania mimi ni nani? Mimi siye yule mnayemtazamia. Lakini anayekuja baada yangu mimi sistahili hata kufungua viatu vyake.’

26 “Ndugu zangu, wana wa Ibrahimu, na ninyi mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu ni kwa ajili yetu. 27 Watu wa Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua Yesu kuwa ni Mwokozi. Lakini kwa kum hukumu kifo walitimiza maneno ya manabii yaliyokuwa yaliyokuwa yakisomwa kila siku ya sabato. Hata hivyo wameyafanya maneno ya manabii kutimilika walipomshitaki Yesu. 28 Ijapo kuwa hawakupata sababu yo yote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato amtoe auawe. 29 Na baada ya kufanya kila kitu kilichotabiriwa katika Maandiko kumhusu, wakamshusha kutoka msalabani wakamweka kaburini. 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. 31 Na kwa siku nyingi akawatokea wale waliosafiri naye kutoka Galilaya kwenda Yerusalemu. Wao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wote.

32 “Nasi tunawaletea Habari Njema kwamba yale Mungu aliy oahidi baba zetu, 33 sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya Pili, ‘Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako.’ 34 Na kuhusu kufufuka kwake, na kwamba hataona tena uharibifu, Mungu alisema hivi, ‘Nitakupa wewe baraka takatifu za hakika ambazo nilimwahidi Daudi.’ 35 Na pia Maandiko yanasema katika sehemu nyingine, ‘Wewe hutaruhusu Mtakatifu wako aone uharibifu.’ 36 Kwa maana Daudi alipokwisha kamilisha mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alikufa akazikwa pamoja na baba zake, mwili wake ukaharibika. 37 Lakini yule ambaye Mungu alimwinua kutoka kwa wafu, mwili wake haukuharibika. 38 Kwa hiyo ndugu zangu, fahamuni kwamba katika huyu Yesu, msa mahawa dhambi unatangazwa kwenu. 39 Kwa ajili yake, kila mtu amwaminiye anawekwa huru na yale yote ambayo sheria ya Musa haikuweza kuwaweka huru. 40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliy osema manabii yasiwapate: 41 ‘Tazameni ninyi wenye kudharau, mkapate kushangaa na kuangamia kwa maana nitatenda jambo wakati wenu, ambalo hamtalisadiki, hata kama mtu akiwatangazia.’

42 Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi watu waliwasihi warudi tena sabato ifuatayo wawaambie zaidi kuhusu mambo haya. 43 Baada ya mkutano wa sinagogi kumalizika Wayahudi wengi na waongofu wa dini ya Kiyahudi waliwafuata Paulo na Bar naba, nao wakazungumza na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. 44 Sabato iliyofuata karibu watu wote wa mji ule walikuja kusikiliza neno la Mungu. 45 Lakini Wayahudi walipoona lile kusanyiko kubwa la watu, waliona wivu, wakakanusha mafundisho ya Paulo na kumtukana. 46 Paulo na Barnaba wakazidi kufundisha kwa ujasiri, wakisema, “Ilikuwa ni lazima neno la Mungu lihubiriwe kwanza kwenu Wayahudi. Lakini kwa kuwa mnalikataa, mnajihukumu wenyewe kuwa hamstahili kupata uzima wa milele. Tutawahubiria watu wa mataifa mengine. 47 Kwa maana Bwana ametuagiza akisema, ‘Nimewaweka ninyi kuwa nuru kwa watu wa mataifa, ili mpeleke wokovu hadi pembe zote za dunia.”’ 48 Watu wa mataifa mengine waliposikia maneno haya walifurahi, wakalitukuza neno la Mungu; na wote waliochaguliwa kwa ajili ya uzima wa milele wakaamini. 49 Neno la Mungu likaenea sehemu zote katika jimbo lile. 50 Lakini Wayahudi waliwachochea wanawake waheshimiwa wamchao Mungu pamoja na viongozi maarufu wa mji, wakaanza kuwatesa Paulo na Barnaba na kisha wakawafukuza kutoka wilaya ile. 51 Paulo na Barnaba wakakung’uta mavumbi miguuni mwao kuwapinga, wakaenda mji wa Ikonio. 52 Na Wanafunzi wakajazwa na furaha ya Roho Mtaka tifu.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica