Beginning
23 Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumem wona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.” 3 Basi Pilato akamwuliza Yesu, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?” Yesu akamjibu, “Ni kama ulivyosema.” 4 Pilato akawaambia maku hani wakuu na watu wote waliokuwapo, “Sioni sababu ya kutosha kumshtaki huyu mtu!” 5 Lakini wao wakakazana kusema, “Anawa chochea watu kwa mafundisho yake katika Yudea yote. Alianzia huko
Yesu Apelekwa Kwa Herode
6 Pilato aliposikia hayo akauliza, ‘Huyu mtu ni Mgalilaya?” 7 Alipofahamu kwamba Yesu alitoka katika mkoa unaotawaliwa na Herode, akampeleka kwa Herode ambaye wakati huo alikuwa Yerus alemu. 8 Herode alifurahi sana kumwona Yesu. Alikuwa amesikia habari zake na kwa muda mrefu akatamani sana kumwona; na pia alitegemea kumwona Yesu akifanya mwujiza. 9 Kwa hiyo akamwuliza Yesu maswali mengi, lakini yeye hakumjibu neno. 10 Wakati huo, makuhani wakuu na walimu wa sheria walikuwepo wakitoa mashtaka yao kwa nguvu sana. 11 Herode na maaskari wake wakamkashifu Yesu na kumzomea. Wakamvika vazi la kifahari, wakamrudisha kwa Pilato. 12 Siku hiyo, Herode na Pilato, ambao kabla ya hapo walikuwa maadui, wakawa marafiki.
Yesu Ahukumiwa Kifo
13 Pilato akawaita makuhani wakuu, viongozi na watu 14 aka waambia, “Mmemleta huyu mtu kwangu mkamshtaki kuwa anataka kuwa potosha watu. Nimemhoji mbele yenu, na sikuona kuwa ana hatia kutokana na mashtaka mliyoleta. 15 Hata Herode hakumwona na kosa lo lote; ndio sababu amemrudisha kwetu. Kama mnavyoona, mtu huyu hakufanya jambo lo lote linalostahili adhabu ya kifo. 16 Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko, kisha nimwachilie.” [ 17 Kwa kawaida, kila sikukuu ya Pasaka ilimlazimu Pilato kuwafungulia mfungwa mmoja].
18 Watu wote wakapiga kelele kwa pamoja, “ Auawe huyo! Tufungulie Baraba!” 19 Baraba alikuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini. 20 Pilato ali taka sana kumwachilia Yesu kwa hiyo akasema nao tena. 21 Lakini wao wakazidi kupiga kelele, “Msulubishe! Msulubishe!” 22 Kwa mara ya tatu Pilato akasema nao tena, “Amefanya kosa gani huyu mtu? Sioni sababu yo yote ya kutosha kumhukumu adhabu ya kifo. Kwa hiyo nitaamuru apigwe viboko kisha nimwachilie .”
23 Lakini watu wakazidi kupiga kelele kwa nguvu na kusisi tiza kwamba Yesu asulubiwe. Hatimaye, kelele zao zikashinda. 24 Pilato akaamua kutoa hukumu waliyoitaka. 25 Akamwachia huru yule mtu aliyekuwa amefungwa gerezani kwa kuhusika katika fujo na mauaji yaliyotokea mjini; akamkabidhi Yesu mikononi mwao, wamfa nyie watakavyo. Yesu Asulubiwa Msalabani
26 Na walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja ait waye Simoni wa Kirene aliyekuwa anatoka mashambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha atembee nyuma ya Yesu. 27 Umati mkubwa wa watu wakamfuata Yesu ikiwa ni pamoja na wanawake waliokuwa wakimlilia na kuomboleza. 28 Lakini Yesu akawageukia, akawaam bia, “Enyi akina mama wa Yerusalemu, msinililie mimi bali jilil ieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 29 Kwa maana wakati utafika ambapo mtasema, ‘Wamebarikiwa akina mama tasa, ambao hawakuzaa na matiti yao hayakunyonyesha.’ 30 Na watu wataiambia milima, ‘Tuangukieni’ na vilima, ‘Tufunikeni’. 31 Kwa maana kama watu wanafanya mambo haya wakati mti ni mbichi, itakuwaje utakapo kauka?”
32 Wahalifu wengine wawili pia walipelekwa wakasulubiwe pamoja na Yesu. 33 Walipofika mahali paitwapo “Fuvu la kichwa,” wakamsulubisha Yesu hapo pamoja na hao wahalifu; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.
34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui wali tendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura. 35 Watu wakasi mama pale wakimwangalia. Viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Si aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama kweli yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36 Askari nao wakam wendea, wakamdhihaki. Wakamletea siki anywe, 37 wakamwambia, “Kama wewe ni mfalme wa Wayahudi, jiokoe tuone.”
38 Na maandishi haya yaliwekwa kwenye msalaba juu ya kichwa chake: “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.” 39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”
40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”
Yesu Afa Msalabani
44 Ilikuwa kama saa sita mchana. Kukawa na giza nchi nzima mpaka saa tisa, 45 kwa maana jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likapasuka katikati kukawa na vipande viwili. 46 Yesu akapaza sauti akasema, “Baba, mikononi mwako ninaikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.
47 Mkuu wa maaskari alipoona yaliyotokea, akamsifu Mungu akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 48 Na watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hilo walipoy aona hayo, walirudi makwao wakijipiga vifua kwa huzuni.
49 Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wanawake wal iokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyata zama mambo haya. Yesu Azikwa Kaburini
50 Kulikuwa na mtu mmoja jina lake Yusufu mwenyeji wa mji wa Arimathaya, ambaye alikuwa anautazamia Ufalme wa Mungu. Yeye ali kuwa mjumbe wa Baraza na pia alikuwa mtu mwema na mwenye kuheshi mika. 51 Lakini yeye hakukubaliana na wajumbe wenzake katika uamuzi wao na kitendo cha kumsulubisha Yesu. 52 Basi, Yusufu alikwenda kwa Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. 53 Akaushusha kutoka msalabani, akauzungushia sanda, akauhifadhi katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kaburi hilo lilikuwa halijatumika bado. 54 Siku hiyo ilikuwa Ijumaa, Siku ya Maandalizi, na sabato ilikuwa karibu ianze. 55 Wale wanawake waliokuwa wamefuatana na Yesu kutoka Galilaya wakamfuata Yusufu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa humo. 56 Kisha wakarudi nyumbani wakaandaa marashi na manukato ya kuupaka huo mwili. Lakini waka pumzika siku ya sabato kama ilivyoamriwa.
24 Siku ya Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake wali chukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa wakaenda kaburini. 2 Wakakuta jiwe limeondolewa kwenye mlango wa kaburi. 3 Lakini walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu. 4 Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hilo, ghafla, watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayong’aa sana, wakasimama karibu nao. 5 Wale wanawake, kwa hofu, wakainamisha nyuso zao chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai mahali pa wafu? 6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa Gali laya, 7 kwamba ilikuwa lazima Mwana wa Adamu awekwe mikononi mwa watu waovu, asulubiwe na siku ya tatu afufuke.” 8 Wakayakumbuka maneno ya Yesu. 9 Waliporudi kutoka huko kaburini wakaeleza mambo haya kwa wale wanafunzi kumi na mmoja pamoja na wengine wote. 10 Hao wanawake walikuwa ni Mariamu Magdalene, Yoana na Mariamu mama yake Yakobo pamoja na wengine waliofuatana nao. 11 Maelezo yao yalionekana kama upuuzi kwa hiyo hawakuwaamini. 12 Bali Petro akaondoka mbio, akaenda kaburini. Alipoinama, akaiona ile sanda, ila hakuona kitu kingine zaidi. Akarudi nyumbani akis taajabia yaliyotokea.
Yesu Awatokea Wanafunzi Wawili
13 Siku hiyo hiyo, wanafunzi wawili wa Yesu walikuwa wanak wenda kijiji cha Emau, yapata maili saba kutoka Yerusalemu, 14 nao walikuwa wakizungumzia mambo yote yaliyotokea. 15 Wali pokuwa wakizungumza, Yesu mwenyewe alikuja akatembea pamoja nao, 16 lakini wao hawakumtambua. 17 Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumzia wakati mnatembea?” Wakasimama , nyuso zao zikionyesha huzuni. 18 Mmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamwambia, “Nadhani ni wewe tu katika watu wote wanaoishi Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotokea siku hizi chache zilizopita.”
19 Akawauliza, “Mambo gani?” Wakamjibu “Mambo yaliyompata Yesu Mnazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo mkuu katika maneno yake na matendo yake, mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 20 Makuhani wakuu na viongozi wetu walimtoa ahukumiwe kufa na wakamsulubisha. 21 Na sisi tulikuwa tumetegemea kwamba yeye ndiye angeliikomboa Israeli. Zaidi ya hayo leo ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee. 22 Isitoshe, baadhi ya wanawake katika kundi letu wametushtua; walikwenda kaburini leo alfajiri 23 lakini hawakuukuta mwili wake. Waliporudi walisema wamewaona malaika ambao waliwaambia kwamba Yesu yu hai. 24 Baadhi yetu walikwenda kaburini wakakuta mambo ni kama walivyoelezea wale wanawake, ila yeye mwenyewe hawakumwona.”
25 Kisha Yesu akawaambia, “Ninyi ni watu wajinga. Mbona mnaona ugumu kuamini mambo yote yaliyosemwa na Manabii? 26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa na kwa njia hiyo aingie katika utukufu wake?” 27 Akawafafanulia maandiko yalivyosema kumhusu yeye, akianzia na maandiko ya Musa na kupitia maandiko yote ya manabii.
28 Walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea na safari. 29 Lakini wakamsihi akae nao wakisema, “Kaa hapa nasi kwa maana sasa ni jioni na usiku unain gia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30 Alipokuwa nao mezani, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia. 31 Ndipo macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua! Lakini akatoweka, hawakumwona tena.
32 Wakaulizana, “Je, mioyo yetu haikuchangamka kwa furaha alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?” 33 Wakaondoka mara moja, wakarudi Yerusalemu. Wakawakuta wale wanafunzi kumi na mmoja na wale waliokuwa pamoja nao, wamekusany ika 34 wakisema, “Ni kweli Bwana amefufuka! Amemtokea Simoni.” 35 Kisha wale wanafunzi wawili wakaeleza yaliyotokea njiani na jinsi walivyomtambua Yesu alipoumega mkate. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake
36 Wakati walipokuwa wanazungumza hayo, Yesu mwenyewe akasi mama katikati yao akawasalimu, “Amani iwe nanyi.”
37 Wakashtuka na kuogopa wakidhani wameona mzimu. 38 Lakini akawauliza, “Kwa nini mnaogopa? Kwa nini mna mashaka mioyoni mwenu? 39 Tazameni mikono yangu na miguu yangu mwone kuwa ni mimi. Niguseni mwone. Mzimu hana nyama na mifupa kama mnion avyo.” 40 Aliposema haya aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. 41 Wakashindwa kuamini kwa ajili ya furaha na mshangao waliokuwa nao. Akawauliza, “Mna chakula cho chote hapa?” 42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa, 43 akakichukua akakila mbele yao.
44 Akawaambia, “Haya ndiyo mambo niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi; kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika she ria ya Musa, katika Maandiko ya manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.” 45 Akawapa uwezo wa kuyaelewa Maandiko, 46 aka waambia, “Haya ndiyo yaliyoandikwa: Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka kwa wafu. 47 Habari hii ya wokovu itatan gazwa kwanza Yerusalemu hadi kwa mataifa yote, kwamba: kuna msa maha wa dhambi kwa wote watakaotubu na kunigeukia mimi. 48 Ninyi ni mashahidi wa mambo haya. 49 Na sasa nitawapelekea Roho Mtaka tifu kama alivyoahidi Baba yangu; lakini kaeni humu Yerusalemu mpaka mtakapopewa nguvu ya Roho Mtakatifu kutoka mbinguni.”
Yesu Apaa Mbinguni
50 Kisha akawaongoza nje ya mji mpaka Bethania, akainua mikono yake, akawabariki. 51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. 52 Wakamwabudu na kisha wakarudi Yerus alemu wamejawa na furaha;
Copyright © 1989 by Biblica