Beginning
Paulo Asafirishwa Kwenda Rumi
27 Ilipoamuliwa kwamba twende Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa askari mmoja aitwaye Juliasi ambaye alikuwa wa kikosi cha Kaisari Agusto. 2 Tulipakia meli iliyotoka Adrami tio ambayo ilikuwa ikielekea kwenye bandari zilizopo pwani ya Asia. Tukaanza safari yetu tukiongozana na Aristarko, Mmakedonia wa kutoka Thesalonike. 3 Kesho yake tulifika Sidoni. Juliasi akamfanyia wema Paulo, akamruhusu aende kuwaona rafiki zake wam hudumie. 4 Kutoka huko tuliendelea na safari yetu, na kwa kuwa tulikuwa tunakabili upepo, tukapitia upande wa kisiwa cha Kipro usioelekea upepo. 5 Tukavuka bahari, kutoka upande wa Kilikia, na Pamfilia, tukafika Mira, katika jimbo la Likia. 6 Yule askari akapata meli iliyokuwa inatoka Aleksandria ikielekea Italia, akatupakia humo. 7 Tukasafiri pole pole kwa siku nyingi, na kwa shida na hatimaye tukafika karibu na bandari ya Nido. Lakini kwa kuwa upepo mkali ulikuwa ukivuma kutoka tulikokuwa tukielekea, hatukuweza kuendelea moja kwa moja na safari yetu, bali tulipitia upande wa pili wa Krete tukaizunguka ncha ya Salmone. 8 Baada ya kuizunguka kwa shida tulifika sehemu iitwayo Bandari Nzuri, kar ibu na mji wa Lasea.
9 Tulikuwa tumepoteza muda mrefu baharini na kwa wakati huu safari ilikuwa ya hatari kwa maana majira ya kufunga yalikuwa yamekwisha pita. Paulo akawaonya marubani wa ile meli akasema, 10 ‘ ‘Mabwana, naona tukiendelea na safari hii patatokea maafa na hasara kubwa kwa meli na shehena na hata maisha yetu yatakuwa hatarini.” 11 Lakini yule askari akaamua kusikiliza zaidi ushauri wa nahodha na mwenye meli kuliko maneno ya Paulo. 12 Kwa kuwa ile bandari ilikuwa haifai kukaa wakati wa majira ya baridi, wengi wakashauri kwamba waendelee na safari na pengine kwa bahati wangeweza kufika Foinike. Hii ni bandari iliyoko katika kisiwa cha Krete na ambayo inatazama upande wa kusini-magharibi na kas kazini-magharibi, kwa hiyo wangeweza kukaa huko mpaka majira ya baridi yaishe.
Dhoruba Baharini
13 Upepo ulipoanza kuvuma taratibu toka kusini, wakadhani kuwa hii ilikuwa ni dalili nzuri kwamba wangeweza kuendelea na safari. Kwa hiyo wakang’oa nanga wakasafiri wakipita kando kando ya pwani ya kisiwa cha Krete. 14 Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali uitwao ‘Kaskazi-mashariki’ ukavuma toka nchi kavu; 15 ukaipiga ile meli, na kwa kuwa haikuwa rahisi kushindana nao, tukaiachilia meli isukumwe kuelekea kule upepo unakokwenda. 16 Hatimaye tukasafiri kupitia nyuma ya kisiwa kidogo kiitwacho Kauda, ambapo kwa kuwa tulikuwa tumekingiwa upepo na hicho kisiwa, tuliweza kwa shida kuifunga mashua ya kuokolea watu. 17 Watu walipokwisha ivuta mashua hiyo wakaiingiza katika meli, waliifunga kwa kamba kwenye meli. Kisha, kwa kuogopa kwamba wangesukumwa na upepo mkali na kukwama kwenye mchanga karibu na pwani ya Sirti, walishusha matanga wakaiacha meli ielee. 18 Kesho yake dhoruba kali iliendelea kuvuma, kwa hiyo wakaanza kuitupa shehena baharini. 19 Siku ya tatu wakaanza kutupa vifaa vya meli baharini kwa mikono yao wenyewe. 20 Kwa siku nyingi hatukuona jua wala nyota, na dhoruba kali ilikuwa inaendelea kuvuma. Kwa hiyo tukakata tamaa kabisa kwamba tungeokolewa.
21 Kwa kuwa walikuwa wamekaa siku kadhaa bila kula cho chote, Paulo akasimama kati yao akasema, “Mngenisikiliza wala msingeondoka Krete na kupata mkasa huu na hasara hii. 22 Lakini sasa nawaomba mjipe moyo. Hakuna hata mmoja wenu atakayepoteza maisha yake ila meli hii itaangamia. 23 Jana usiku, malaika wa Mungu wangu ambaye mimi namwabudu alisimama karibu yangu 24 akasema, ‘Usiogope Paulo; huna budi kujitetea katika kesi yako mbele ya Kaisari; na kwa neema yake, Mungu amekupa maisha ya watu wote wanaosafiri pamoja na wewe.’ 25 Kwa hiyo muwe na matu maini kwa maana nina imani kwa Mungu kwamba mambo yatakuwa kama nilivyoambiwa. 26 Lakini hata hiyo meli yetu itakwama kwenye kisiwa fulani. ”
27 Siku ya kumi na nne, mnamo saa sita za usiku, tulipokuwa bado tunasukumwa na upepo katika bahari ya Adria, mabaharia wali hisi kwamba walikuwa wanakaribia nchi kavu. 28 Kwa hiyo wakapima kina cha bahari wakakuta kilikuwa mita thelathini na tano hivi, na baada ya kitambo kidogo wakapima tena wakapata kina cha mita ishirini na sita hivi. 29 Wakaogopa kwamba meli yetu ingegonga kwenye miamba, kwa hiyo wakashusha nanga nne nyuma ya meli, wakawa wanaomba kupambazuke. 30 Mabaharia walikuwa wanataka kutoroka kutoka mle melini, wakashusha mashua baharini wakidanga nya kuwa walikuwa wanakwenda kuweka nanga upande wa mbele ya meli. Ndipo 31 Paulo akawaambia wale maaskari na maofisa wao, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokolewa.” 32 Basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua kwenye meli wakaiacha mashua ichukuliwe baharini. 33 Mapambazuko yalipokaribia, Paulo akawasihi watu wote wale chakula akisema, “Leo ni siku ya kumi na nne mmekuwa katika wasiwasi bila kula cho chote. 34 Kwa hiyo nawasihi mle chakula kwa maana mnakihi taji ili muweze kuishi. Hakuna mmoja wenu atakayepoteza hata unywele mmoja kichwani mwake.” 35 Baada ya maneno haya, Paulo akachukua mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote, akaumega akaanza kula. 36 Ndipo wote wakatiwa moyo, wakaanza kula chak ula. 37 Ndani ya meli tulikuwa jumla ya watu mia mbili na sabini na sita. 38 Baada ya wote kula chakula cha kutosha, wakapunguza uzito wa meli kwa kutupa ngano baharini.
39 Kulipokucha, mabaharia hawakuitambua ile nchi, lakini waliona ghuba yenye ufuko wa mchanga ambako walitaka waielekeze meli kama ingewezekana, ili wafike pwani. 40 Kwa hiyo wakatupa nanga zote baharini, wakalegeza kamba zilizokuwa zikishikilia usukani wa meli, na kutweka tanga la mbele lishike upepo na kuisukuma meli kuelekea pwani. 41 Lakini ile meli ikagonga mwamba ikakwama kwenye mchanga na upande wa mbele wa meli uka banwa kwenye mwamba wala usingeweza kuondolewa tena. Na upande wa nyuma ulivunjika vipande kwa nguvu ya yale mawimbi. 42 Wale askari walikuwa wamepanga kuwaua wafungwa wote ili wasije wakaogelea hadi pwani na kutoroka. 43 Lakini yule Ofisa wa maas kari alitaka kumwokoa Paulo, kwa hiyo akawazuia wasitekeleze mpango wao. Akaamuru wale wanaoweza kuogelea wajitupe baharini kwanza, na waogelee kuelekea pwani; 44 na wengine wajishikize kwenye vipande vya meli waelee navyo. Kwa jinsi hii, watu wote waliokolewa wakafika nchi kavu. 28 1 Tulipofika salama nchi kavu, tuligundua kwamba tuko katika kisiwa kiitwacho Melita. 2 Wenyeji wa kisiwa hicho walitufanyia ukarimu wa ajabu, wakawasha moto na kutukaribisha kwa maana mvua ilikuwa inanyesha na kulikuwa na baridi kali. 3 Paulo alikuwa amekusanya kuni nyingi na alipokuwa akiziweka kwenye moto, aka toka humo nyoka mwenye sumu akikimbia ule moto akajisokotea kwe nye mkono wa Paulo. 4 Wale wenyeji walipomwona yule nyoka ameji sokota kwenye mkono wa Paulo, wakaambiana, “Bila shaka mtu huyu ni muuaji, ijapokuwa ameokoka kufa maji baharini, haki haikumru husu aishi.” 5 Lakini Paulo akamkung’utia yule nyoka ndani ya moto wala yeye hakupata madhara yo yote. 6 Wakangojea wakitarajia kwamba atavimba au ataanguka ghafla na kufa. Lakini baada ya kungoja kwa muda mrefu na hawakuona dalili yo yote mbaya ikimto kea, wakabadili mawazo yao, wakasema yeye ni mungu.
7 Karibu na pwani ile, kulikuwa na shamba kubwa la gavana wa kisiwa kile aliyeitwa Publio. Huyu gavana alitukaribisha kwa ukarimu mkubwa, akatufanyia sherehe kwa muda wa siku tatu. 8 Baba yake Publio alikuwa mgonjwa amelala, ana homa kali na kuhara damu. Paulo akaenda kumwona, akamwekea mikono akamwombea; naye akapona. 9 Jambo hili lilipotokea, watu wote wa kisiwa kile wal iokuwa wagonjwa wakaja, nao wakaponywa. 10 Kwa hiyo wakatuletea zawadi nyingi, nasi tulipokuwa tukijiandaa kuondoka walitupatia kila kitu tulichohitaji kwa ajili ya safari.
Paulo Anawasili Rumi
11 Baada ya miezi mitatu tuliondoka kwa meli iliyokuwa ime toka Aleksandria ikawa imetia nanga katika kisiwa cha Melita mpaka majira ya baridi yaishe. Meli hiyo ilikuwa na picha ya miungu pacha Kasta na Poluksi. 12 Kituo chetu cha kwanza kili kuwa Sirakusa ambako tulikaa kwa siku tatu. 13 Kutoka huko tuka zunguka tukafika Regio; na baada ya siku moja, upepo mkali uka vuma kutoka kusini, na siku ya pili tukafika Puteoli. 14 Na hapa tuliwakuta waamini ambao walitukaribisha tukae nao kwa siku saba. Ndipo tukaendelea na safari mpaka tukafika Rumi. 15 Ndugu waamini wa Rumi walipopata habari zetu, walikuja mpaka soko la Apio na wengine wakaja mpaka mahali paitwapo ‘Mikahawa Mitatu’ kutulaki. Paulo alipowaona, alimshukuru Mungu akachangamka. 16 Tulipofika Rumi, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake akiwa na askari wa kumlinda.
Paulo Ahubiri Rumi
17 Baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja viongozi wa Kiy ahudi wa Roma na walipofika Paulo akawaambia, “Ndugu zangu, ingawa sikufanya jambo lo lote kuwadhuru watu wetu au kinyume cha mila za baba zetu, hata hivyo nilikamatwa Yerusalemu nikakabid hiwa kwa utawala wa Kirumi. 18 Wao walipokwisha kunihoji wali taka kuniachilia huru kwa sababu hawakuona kosa lo lote nililoli fanya linalostahili adhabu ya kifo. 19 Lakini Wayahudi walipinga uamuzi huo, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisari, ijapokuwa sikuwa na lalamiko lo lote juu ya taifa langu. 20 Hii ndio sababu nimeomba kuonana nanyi niwaeleze mambo haya. Kwa maana kusema kweli, nimevaa pingu hizi kwa sababu ya tumaini la Israeli.” 21 Wakamwambia, “Hatujapokea barua zo zote zinazoku husu wewe kutoka Yudea, wala hakuna ndugu ye yote aliyefika hapa ambaye ameleta ripoti mbaya kukuhusu. 22 Lakini tungependa kusi kia mawazo yako kwa sababu tunajua kwamba kila mahali watu wana zungumza mabaya kuhusu dhehebu hili.” 23 Basi wakapanga siku ya kumsikiliza, na ilipofika, wakaja watu wengi mahali alipokuwa anakaa Paulo. Akawaeleza kuhusu Ufalme wa Mungu tangu asubuhi hadi jioni, akijaribu kuwahakikishia juu ya Yesu akitumia Maan diko ya Musa na Manabii. 24 Baadhi yao wakakubali, wakaamini, lakini wengine wakakataa kuamini. 25 Kwa kuwa hawakukubaliana kati yao, wakaamua kuondoka, na walipokuwa tayari kuondoka, Paulo akawaambia, “Roho Mtakatifu alisema kweli alipowaambia baba zenu kupitia nabii Isaya: 26 ‘Nenda ukawaambie watu hawa, mtasikiliza na kusikiliza, lakini hamtaelewa. Mtatazama na kutazama lakini hamtatambua. 27 Kwa sababu mioyo ya watu hawa imepumbaa, masikio yao hayasikii na wamefunga macho yao. Kama si hivyo, wangeona kwa macho yao, wangesikia kwa masikio yao, wangeelewa kwa mioyo yao na kunigeukia; nami ningewaponya.’ 28 Kwa hiyo napenda mfahamu ya kuwa wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa mataifa; wao wata sikiliza.” 29 Baada ya Paulo kusema maneno haya Wayahudi wakaondoka wakibishana vikali wao kwa wao.] 30 Kwa muda wa miaka miwili Paulo aliishi katika nyumba ya kupangisha akiwakaribisha wote waliokuja kumwona.
Copyright © 1989 by Biblica