Beginning
Yesu Amponya Mtu Aliyezaliwa Kipofu
9 Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. 2 Wanafunzi wake wakamwuliza, “Bwana, ni nani aliyet enda dhambi ya kusababisha mtu huyu azaliwe kipofu, ni yeye au wazazi wake?”
3 Yesu akawajibu, “Huyu hakuzaliwa kipofu kwa sababu yeye au wazazi wake walitenda dhambi. Jambo hili lilitokea ili nguvu za Mungu zionekane zikifanya kazi katika maisha yake. 4 Yatupasa tutende kazi yake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana kwa maana usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. 5 Wakati nipo ulimwenguni, Mimi ni nuru ya ulimwengu.”
6 Baada ya kusema haya, akatema mate kwenye udongo aka tengeneza tope kwa mate yake akampaka yule kipofu machoni. 7 Kisha akamwambia, “Nenda kanawe uso katika kijito cha Siloamu.” Neno ‘Siloamu’ maana yake ni ‘aliyetumwa.’ Yule kipofu akaenda akanawa na akarudi akiwa anaona!
8 Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona akiomba omba wakauliza, “Huyu si yule kipofu aliyekuwa akiketi hapa akiomba msaada?” 9 Baadhi wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “Siye, bali wamefanana.” Lakini yeye akawahakikishia kuwa yeye ndiye yule kipofu ambaye sasa anaona.
10 Wakamwuliza, “Macho yako yalifumbuliwaje?” 11 Akawaam bia, “Yule mtu aitwaye Yesu alitengeneza tope akanipaka machoni akaniambia niende nikaoshe uso katika kijito cha Siloamu. Nikaenda na mara baada ya kuosha uso nikaweza kuona!” 12 Wakam wuliza, “Huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.”
Mafarisayo Wachunguza Kuponywa Kwa Kipofu
13 Wakampeleka yule mtu aliyeponywa upofu kwa Mafarisayo. 14 Siku hiyo Yesu aliyomponya ilikuwa siku ya sabato. 15 Mafar isayo nao wakamwambia awaeleze jinsi alivyopata kuponywa. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho, nikanawa uso na sasa naona.” 16 Baadhi ya Mafarisayo wakamwambia, “Huyu mtu ali yekuponya hawezi kuwa ametoka kwa Mungu kwa sababu hatimizi she ria ya kutokufanya kazi siku ya sabato.” Lakini wengine wakab isha, wakiuliza, “Anawezaje mtu mwenye dhambi kufanya maajabu ya jinsi hii?” Pakawepo na kutokuelewana kati yao . 17 Kwa hiyo wakamgeukia tena yule aliyeponywa wakamwuliza, “Wewe unamwonaje huyu mtu ambaye amekufanya ukaweza kuona?” Yeye akawajibu, “Mimi nadhani yeye ni nabii.”
18 Wale viongozi wa Wayahudi hawakuamini ya kuwa yule mtu aliwahi kuwa kipofu, mpaka walipoamuru wazazi wake waletwe; 19 wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu ambaye alizaliwa kipofu? Ikiwa ndiye, imekuwaje sasa anaweza kuona?” 20 Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu ambaye ali zaliwa kipofu. 21 Lakini hatujui jinsi alivyoponywa akaweza kuona, wala hatujui ni nani aliyemwezesha kuona. Mwulizeni, yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.” 22 Walisema hivi kwa tahadhari kwa sababu viongozi wa Wayahudi walikuwa wamekubal iana kuwa mtu ye yote atakayetamka kuwa Yesu ndiye Kristo atafu kuzwa kutoka katika ushirika wa sinagogi. 23 Ndio maana wakasema “Mwulizeni, yeye ni mtu mzima.”
24 Kwa hiyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu wakamwambia, “Tuambie kweli mbele ya Mungu. Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.” 25 Akawajibu, “Kama yeye ni mwenye dhambi au sio, mimi sijui. Lakini nina hakika na jambo moja: nil ikuwa kipofu na sasa naona.”
26 Wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?” 27 Akawajibu, “Nimekwisha waambia aliyonifanyia lakini hamtaki kusikia. Mbona mnataka niwaeleze tena? Au na ninyi mna taka kuwa wafuasi wake?” 28 Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ni mfuasi wake. Sisi ni wafuasi wa Musa. 29 Tunajua kwamba Mungu alisema na Musa. Lakini huyu mtu hatujui anakotoka.” 30 Akawa jibu, “Hii kweli ni ajabu! Hamjui anakotoka naye ameniponya upofu wangu! 31 Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomwabudu na kumtii. 32 Haijawahi kutokea tangu ulimwengu kuumbwa kwamba mtu amemponya kipofu wa kuzaliwa. 33 Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufa nya lo lote.” 34 Wao wakamjibu, Wewe ulizaliwa katika dhambi! Utawezaje kutufundisha?” Wakamfukuzia nje.
Vipofu Wa Kiroho
35 Yesu alipopata habari kuwa yule mtu aliyemfumbua macho amefukuzwa kutoka katika sinagogi, alimtafuta akamwuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?” 36 Yule mtu akamjibu, “Tafadhali nifahamishe yeye ni nani ili nipate kumwamini.” 37 Yesu akam jibu “Umekwisha mwona naye ni mimi ninayezungumza nawe.” 38 Yule mtu akamjibu huku akipiga magoti, “Bwana, naamini.”
39 Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu; ili wale walio vipofu wapate kuona; na wale wanaodhani wanaona, waonekane kuwa vipofu.”
40 Baadhi ya Mafarisayo waliomsikia akisema hivi wakauliza, “Je, unataka kusema kuwa sisi pia ni vipofu?” 41 Yesu akawa jibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, hamngekuwa na hatia. Lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi bado mna hatia.”
Mchungaji Mwema
10 “Ninawaambia hakika, mtu asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya ndani kwa kupitia njia nyin gine, ni mwizi na mnyang’anyi. 2 Anayepitia mlangoni ndiye mchun gaji wa kondoo. 3 Mlinzi humfungulia mlango na kondoo hutambua sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwaongoza nje ya zizi. 4 Akiisha watoa wote nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaifahamu sauti yake. 5 Kondoo hawam fuati mtu wasiyemfahamu bali humkimbia, kwa sababu hawatambui sauti ya mgeni.” 6 Yesu alitumia mfano huu lakini wao hawakuel ewa maana yake.
7 Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni mlango wa kupitia kondoo. 8 Wote walionitangulia ni wezi na wany ang’anyi. Hata hivyo kondoo hawakuwafuata. 9 Mimi ni mlango; mtu ye yote anayeingia zizini kwa kupitia kwangu atakuwa salama, naye ataingia na kutoka na kupata malisho. 10 Mwizi huja kwa nia ya kuiba, kuua na kuharibu. Nimekuja ili watu wapate uzima; uzima ulio kamili. 11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.
14 Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15 kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”
19 Maneno haya yalisababisha mafarakano tena kati ya Way ahudi. 20 Wengi wao walisema, “Huyu amepagawa na shetani, kwa nini tuendelee kumsikiliza?” 21 Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na shetani. Je, shetani anaweza kumpo nya kipofu?”
Yesu Anajitambulisha
22 Ilikuwa sikukuu ya Utakaso wa Hekalu wakati wa majira ya baridi, 23 na Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Sulemani. 24 Wayahudi wakamzunguka wakamwuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo utuambie wazi wazi.” 25 Yesu akawajibu, “Nimewaambia lakini hamuamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yan anishuhudia. 26 Lakini hamuamini kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 27 Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata; 28 nami ninawapa uzima wa milele. Hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono yangu. 29 Baba yangu ambaye amenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa hawa kutoka katika mikono yake. 30 Mimi na Baba yangu tu mmoja.”
31 Kwa mara nyingine wale Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo. 32 Yesu akawauliza, “Nimewaonyesha mambo mengi mazuri kutoka kwa Baba yangu. Kati ya hayo ni lipi linalosababisha mtake kunipiga mawe?” 33 Wao wakamjibu, “Tunataka kukupiga mawe si kwa sababu ya mambo mema uliyotenda bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
Wewe ni mtu tu lakini unajiita Mungu.”
34 Yesu akawauliza, “Je, haikuandikwa katika Maandiko yenu ya sheria, ‘Nimesema, ninyi ni miungu’? 35 Ikiwa Maandiko, ambayo ni kweli daima, yanawataja wale waliyoyapokea kuwa ni ‘miungu 36 itakuwaje mseme ninakufuru ninaposema ‘mimi ni Mwana wa Mungu,’ ambapo mimi Baba ameniteua niwe wake na akani tuma ulimwenguni? 37 Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msi niamini; 38 lakini ikiwa nafanya kazi za Mungu, mziamini hizo; hata kama hamniamini mimi. Mkifanya hivyo, mtaelewa na kutambua kuwa Baba yangu yuko ndani yangu na mimi ni ndani yake.”
39 Kwa mara nyingine Wayahudi wakajaribu kumkamata, lakini yeye aka waponyoka.
40 Kisha akaenda ng’ambo ya mto Yordani mpaka pale mahali ambapo Yohana alianzia kubatiza, akakaa huko. 41 Watu wengi wakamfuata, nao wakawa wakiambiana, “Yohana hakufanya muujiza wo wote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 42 Na wengi wakamwamini Yesu.
Copyright © 1989 by Biblica