Print Page Options Listen to Acts 14-15
Previous Prev Day Next DayNext

Beginning

Read the Bible from start to finish, from Genesis to Revelation.
Duration: 365 days
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Version
Matendo Ya Mitume 14-15

Mahubiri ya Injili huko Ikonio

14 Basi huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi. Wakahubiri kwa uwezo mkuu na umati mkubwa wa watu wakaamini, Wayahudi pamoja na watu wa mataifa mengine. Lakini wale Wayahudi ambao hawakupokea neno la Mungu, waliwa chochea watu wa mataifa dhidi ya wale walioamini. Paulo na Bar naba wakakaa huko kwa muda mrefu wakifundisha kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha kuwa mahubiri yao yalikuwa ni neno la neema yake; akawapa uwezo wa kutenda ishara na maajabu. Hata hivyo watu wa mji ule waligawanyika. Wengine wakaungana na wale Wayahudi na wengine wakawa upande wa mitume. Watu wa mataifa na Wayahudi walijiunga na baadhi ya viongozi wakafanya mpango wa kuwasumbua mitume na kisha kuwapiga mawe. Lakini wao walipopata habari hizi walitoroka wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya wilaya ya Likaonia, na sehemu zilizopakana nayo. Huko waliende lea kuhubiri Habari Njema.

Kiwete Aponywa Huko Listra

Katika mji wa Listra, alikuwepo kiwete amekaa, ambaye ali kuwa amelemaa miguu yote miwili tangu alipozaliwa, na hakuwahi kutembea kamwe. Alimsikiliza Paulo alipokuwa akihubiri, na Paulo alipomtazama aliona kuwa anayo imani ya kuponywa. 10 Kwa hiyo Paulo akasema kwa sauti, “Simama kwa miguu yako!” Mara yule mtu akaruka juu akaanza kutembea! 11 Wale watu walipoona maajabu aliyofanya Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao, wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!” 12 Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye alikuwa msemaji mkuu. 13 Kuhani mkuu wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua aki taka kuwatolea sadaka penye lango la mji pamoja na ule umati wa watu. 14 Lakini Paulo na Barnaba waliposikia na kuona mambo haya waliyotaka kufanya, walirarua nguo zao, wakawakimbilia wale watu, wakisema, 15 ‘ ‘Kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni binadamu tu, kama ninyi! Tumekuja kuwatangazia Habari Njema; mziache hizi ibada zisizo na maana na mumgeukie Mungu aliye hai ambaye aliumba mbingu na nchi na bahari, na vyote vilivyoko. 16 Wakati wa vizazi vilivyopita aliwaachia watu waishi walivyotaka. 17 Hata hivyo hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake. Kwa maana aliwatendea mema akawaletea mvua kutoka mbinguni na mazao kwa majira yake, akawatosheleza kwa vyakula na raha.” 18 Hata pamoja na maneno yote haya haikuwa rahisi kuwazuia wale watu waache kuwatolea sadaka zao.

19 Wakaja watu kutoka Antiokia na Ikonio wakawashawishi wale watu, wakampiga Paulo kwa mawe, wakamkokota hadi nje ya mji, wakidhani amekufa. 20 Lakini waamini walipokusanyika kumzunguka, aliamka, akarudi nao mjini. Kesho yake akaondoka na Barnaba wakaenda mpaka Derbe.

Paulo Na Barnaba Warudi Antiokia

21 Walipokwisha hubiri Habari Njema katika mji ule na watu wengi wakaamini wakawa wanafunzi, walirudi Listra na Ikonio na Antiokia. 22 Huko waliwatia nguvu wanafunzi na kuwashauri waendelee kukua katika imani. Wakawaonya wakisema, “Tunalazimika kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika mateso mengi.” 23 Na baada ya kuwachagulia wazee viongozi katika kila kanisa, wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini kwa maombi na kufunga. 24 Basi wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. 25 Na baada ya kufundisha neno la Mungu huko Perga, walikwenda upande wa kusini hadi Atalia. 26 Kutoka huko wakasafiri kwa mashua mpaka Anti okia, ambako walikuwa wameombewa neema ya Mungu kwa kazi ambayo walikuwa wameikamilisha. 27 Walipowasili Antiokia waliwakusanya waamini pamoja wakawaeleza yale yote ambayo Mungu alikuwa amewa tendea, na jinsi Mungu alivyotoa nafasi ya imani kwa watu wasio Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.

Wayahudi. 28 Wakakaa huko na wale wanafunzi kwa muda mrefu.

Baraza La Yerusalemu

15 Watu wengine walikuja Antiokia kutoka Yudea wakawa wakiwa fundisha ndugu walioamini kwamba, “Kama hamkutahiriwa kufuatana na desturi iliyofundishwa na Musa hamwezi kuokolewa.” Paulo na Barnaba walikuwa na mabishano makali nao wakipinga mafundisho haya. Ikaamuliwa kwamba Paulo na Barnaba na waamini wengine waende Yerusalemu wakawaulize mitume na wazee juu ya jambo hili. Kwa hiyo, wakiwa wametumwa na kanisa, njiani walipitia makanisa ya Foenike na Samaria wakatoa taarifa jinsi watu wa mataifa men gine walivyokuwa wakimgeukia Bwana. Habari hizi ziliwafurahisha sana hao ndugu. Walipofika Yerusalemu walipokelewa na kanisa, mitume na wazee; nao wakatoa taarifa kuhusu mambo yote ambayo Mungu aliyafanya kwa kuwatumia wao. Lakini baadhi ya waamini waliokuwa wakishikilia desturi za Mafarisayo wakasema, “Ni lazima watahiriwe na wafundishwe kushika sheria ya Musa.”

Mitume na wazee wa kanisa wakakutana kushauriana juu ya jambo hili. Baada ya majadiliano marefu, Petro akasimama na kusema, “Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za mwanzo Mungu alini chagua ili kwa midomo yangu watu wa mataifa mengine wapate kusi kia Habari Njema na kuamini. Na Mungu ambaye anajua mioyo ya watu alishuhudia kwamba anawakubali watu wa mataifa kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama alivyotupa na sisi. Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa sababu waliamini. 10 Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuwatwika hawa ndugu wanafunzi mzigo wa sheria ambao baba zetu na sisi tumesh indwa kuubeba? 11 Sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana wetu Yesu, kama na wao wanavyookolewa.” 12 Baraza lote likakaa kimya; wakawasikiliza Paulo na Barnaba wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu wa mataifa. 13 Walipomaliza maelezo yao, Yakobo akasema, “Ndugu zangu, nisikilizeni. 14 Simoni amekwisha kutueleza jinsi, kwa mara ya kwanza, Mungu amejichagulia waamini kutoka kwa watu wa mataifa. 15 Hata maneno ya manabii yanakubaliana kabisa na jambo hili. Kama ilivyoandikwa: 16 ‘ Baada ya mambo haya nitarudi, nami nitajenga upya nyumba ya Daudi ambayo imeanguka. Nitajenga tena magofu yake na kuisimamisha, 17 ili binadamu wengine wote wamtafute Bwana, pamoja na watu wa mataifa yote ambao wanaitwa kwa jina langu; 18 asema Bwana, ambaye ametufahamisha mambo hayo tangu kale.’

19 “Kwa hiyo uamuzi wangu ni kwamba, tusiwasumbue watu wa mataifa wanaomgeukia Mungu kwa desturi zetu; 20 badala yake, tuwaandikie barua tuwaambie wajiepushe na uchafu wa ibada za sanamu, na zinaa na waache kula nyama ya wanyama walionyongwa au kunywa damu. 21 Kwa maana sheria za Musa zimekuwa zikihubiriwa katika kila mji na kusomwa katika masinagogi kila sabato tangu vizazi vya awali.”

Barua Kwa Waamini Wa Mataifa Mengine

22 Mitume na wazee na kanisa zima wakakubaliana. Wakachagua watu waongozane na Paulo na Barnaba kwenda Antiokia. Walimchagua Yuda aitwaye Barsaba na Sila. Hawa wawili walikuwa viongozi wal ioheshimiwa miongoni mwa ndugu wote. 23 Wakatumwa na barua ifu atayo: “Sisi mitume na wazee, ndugu zenu, tunawasalimu ninyi wa mataifa mlioamini huko Antiokia, Siria na Kilikia. 24 Kwa kuwa tumesikia kwamba kuna baadhi ya watu kati yetu waliokuja huko bila kibali chetu kutatanisha mawazo yenu kwa maneno yao, 25 tumeona ni vyema, kwa kauli moja, kuwachagua watu waje huko pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo, 26 ambao wamehatarisha maisha yao kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. 27 Tumewatuma hawa ndugu, Yuda na Sila, wawaeleze kwa mdomo mambo haya tunayow aandikia. 28 Kwa maana Roho Mtakatifu ameona vyema na sisi tume kubaliana tusiwatwike mzigo mkubwa zaidi ya mambo yafuatayo ambayo ni ya lazima: 29 kwamba msile cho chote kilichotolewa sadaka katika ibada za sanamu, kunywa damu, nyama ya wanyama wal ionyongwa; na muepukane na uasherati. Mkijitenga na mambo haya mtakuwa mmefanya vyema. Kwaherini.”

30 Wale wajumbe walipokwisha kuagwa, wakaondoka wakaenda Antiokia, wakakusanya ushirika wote wa waamini, wakawapa ile barua. 31 Nao watu walipokwisha kuisoma, wakafurahishwa sana na ujumbe wake wa kutia moyo. 32 Yuda na Sila, ambao walikuwa mana bii wa kawapa ushauri mwingi wa kuwatia moyo na kuwajenga katika imani. 33 Wakakaa Antiokia kwa muda na kisha waamini wakawaaga. Wakarudi kwa amani kwa wale waliowatuma. [ 34 Lakini Sila aliona ni vema kukaa huko.] 35 Lakini Paulo na Barnaba walibaki Anti okia pamoja na wengine wengi wakifundisha na kuhubiri neno la

Paulo Na Barnaba Wanatengana

36 Baada ya siku chache Paulo alimwambia Barnaba, “Twende tukawatembelee ndugu katika miji yote ambamo tulihubiri neno la Bwana tuone jinsi waamini wanavyoendelea.” 37 Barnaba alitaka wamchukue Yohana Marko waende naye. 38 Lakini Paulo aliona si vizuri kumchukua kwa sababu aliwahi kuwakimbia walipokuwa huko Pamfilia, akakataa kuendelea kufanya kazi nao. 39 Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba juu ya jambo hili, wakaten gana. Barnaba akamchukua Yohana Marko akaenda naye Kipro. 40 Paulo akamchagua Sila akaondoka baada ya ndugu kuwatakia neema ya Bwana. 41 Naye akapitia Siria na Kilikia wakaimarisha makanisa ya huko.

Neno: Bibilia Takatifu (SNT)

Copyright © 1989 by Biblica