Book of Common Prayer
Kazi ya Paulo kwa Ajili ya Kanisa
24 Nina furaha kwa sababu ya mateso ninayopata kwa manufaa yenu. Yapo mambo mengi ambayo kupitia hayo Kristo bado anateseka. Nami ninayapokea mateso haya kwa furaha katika mwili wangu kwa ajili ya mwili wake, yaani Kanisa. 25 Nilifanyika kuwa mtumishi wa kanisa kwa sababu Mungu alinipa kazi maalum ya kufanya. Kazi hii inawasaidia ninyi, nayo ni kuuhubiri ujumbe kamili wa Mungu. 26 Ujumbe huu ni ukweli wenye siri uliofichwa tangu mwanzo wa nyakati. Nao ulifichwa kutoka kwa kila mtu kwa muda mrefu, lakini sasa umedhihirishwa kwa watakatifu wa Mungu. 27 Mungu aliamua kuwajulisha watu wake namna Kweli hii ilivyo na utajiri na utukufu. Siri hii ya kweli hii, ambayo ni kwa ajili ya watu wote, ni kwamba Kristo anaishi ndani yenu. Yeye ndiye tumaini la kushiriki katika utukufu wake. 28 Hivyo tunaendelea kuwaambia watu juu ya Kristo. Tunatumia hekima yote kumshauri na kumfundisha kila mtu. Tunajaribu kumleta kila mtu mbele za Mungu kama watu waliokomaa kiroho katika uhusiano wao na Kristo. 29 Kwa kufanya hivi, ninafanya kazi kwa bidii, nikijitahidi na kutumia nguvu kubwa aliyonipa Kristo. Nguvu hiyo inafanya kazi katika maisha yangu.
2 Ninataka mfahamu ni kwa kiwango gani ninawajali ninyi pamoja na ndugu waishio Laodikia na wengine ambao hawajawahi kuniona. 2 Ninataka ninyi nyote pamoja na wao mtiwe moyo na kuunganishwa pamoja katika upendo na kupata uhakika unaoletwa kwa kuielewa ile kweli. Pia, ninataka waijue kweli iliyokuwa siri ambayo sasa imefunuliwa na Mungu. Kweli hiyo ni Kristo mwenyewe. 3 Yeye peke yake ndiye ambaye ndani yake watu wanaweza kupata hazina zote za hekima na ufahamu zilizofichwa katika Kristo.
4 Nawaambia hili ili asiwepo yeyote atakaye wadanganya kwa maneno na hoja zinazoonekana kuwa ni nzuri, lakini ni mbaya. 5 Ingawa niko mbali kimwili, niko pamoja nanyi katika roho. Ninafurahi kuona jinsi mnavyofanya kazi vizuri pamoja na jinsi imani yenu ilivyo thabiti katika Kristo.
Endeleeni Kumfuata Kristo Yesu
6 Mlimpokea Kristo Yesu kama Bwana, hivyo mwendelee kumfuata yeye. 7 Na mizizi yenu ikue hata ndani ya Kristo, na maisha yenu yajengwe juu yake. Kama mlivyofundishwa imani ya kweli mwendelee kuwa imara katika ufahamu wenu katika hilo. Na msiache kumshukuru Mungu.
Yesu Ajaribiwa na Shetani
(Mk 1:12-13; Lk 4:1-13)
4 Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza Yesu hadi nyikani ili akajaribiwe na Shetani. 2 Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana. 3 Mjaribu[a] akamwendea na akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, basi yaamuru mawe haya yawe mikate.”
4 Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”(A)
5 Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. 6 Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema,
‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea,
ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”(B)
7 Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”(C)
8 Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani. 9 Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.”
10 Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake!’”(D)
11 Baada ya hayo, Shetani akamwacha. Ndipo malaika wakaja kumhudumia.
© 2017 Bible League International