Book of Common Prayer
14 Hivyo rafiki zangu wapenzi, zikimbieni ibada za sanamu. 15 Ninyi ni watu wenye akili. Upimeni ukweli wa haya ninayosema sasa. 16 Kikombe cha baraka[a] tunachokitolea shukrani ni ushirika wa sadaka ya damu ya Kristo, sawa? Na mkate ule tunaomega, ni ushirika wa mwili wa Kristo, sawa? 17 Kuna mkate mmoja, nasi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki katika mkate huo mmoja.
27 Hivyo, ukiula mkate na kukinywea kikombe cha Bwana isivyostahili, unautendea dhambi mwili na damu ya Bwana. 28 Unapaswa kujichunguza mwenendo wako kabla ya kula mkate na kunywa kikombe. 29 Ukila na kunywa bila kuwajali wale ambao ndiyo mwili wa Bwana, kula na kunywa kwako kutasababisha uhukumiwe kuwa mwenye hatia. 30 Ndiyo sababu watu wengi katika kanisa lenu ni wagonjwa na dhaifu, na wengi wameshakufa. 31 Lakini ikiwa tungejichunguza kwa usahihi, Mungu asingetuhukumu. 32 Lakini Bwana anapotuhukumu, anatuadhibu ili kutuonesha njia sahihi. Hufanya hivi ili tusishutumiwe kuwa wakosa na tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.
Karamu ya Pasaka
(Mt 26:17-25; Lk 22:7-14,21-23; Yh 13:21-30)
12 Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambapo kila mara mwana kondoo alitolewa sadaka kwa ajili ya Pasaka. Wanafunzi wa Yesu wakamwendea na kumwuliza, “Ni wapi unapotaka tuende kukuandalia ili uweze kuila Karamu ya Pasaka?”
13 Hivyo Yesu aliwatuma wanafunzi wake wawili, naye akawaeleza, “ingieni mjini, na mtakutana na mtu mmoja aliyebeba gudulia la maji. Mfuateni, 14 popote pale atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba ile, ‘mwalimu anasema, utuonyeshe chumba ambacho yeye na wanafunzi wake wanaweza kuila Karamu ya Pasaka.’ 15 Naye atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, klichoandaliwa tayari kwa ajili yetu. Basi mtuandalie chakula pale.”
16 Wanafunzi wa Yesu waliondoka na kuelekea mjini. Huko walikuta kila kitu kama vile Yesu alivyowaeleza Hivyo, waliandaa mlo wa Pasaka.
17 Wakati wa jioni Yesu alienda pamoja na wanafunzi wake kumi na mbili katika nyumba ile. 18 Wote walipokuwa wameketi mezani wakila, Yesu akasema, “Mniamini ninapowambia kwamba mmoja wenu, yule anayekula nami sasa atanitoa kwa maadui zangu.”
19 Wanafunzi walihuzunika sana kusikia jambo hili. Kila mmoja akamwambia Yesu, “Hakika siyo mimi?”
20 Akawaambia, “Ni mmoja wa wale kumi na mbili; na ni yule atakayechovya mkate katika bakuli pamoja nami. 21 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama ilivyoandikwa juu yake. Lakini itakuwa ya kutisha namna gani kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu anasalitiwa. Itakuwa bora mtu huyu asingelikuwa amezaliwa.”
Chakula cha Bwana
(Mt 26:26-30; Lk 22:15-20; 1 Kor 11:23-25)
22 Na walipokuwa wakila Yesu aliuchukua mkate, akamshukuru Mungu kwa huo. Akamega vipande, akawapa wanafunzi wake, na kusema, “Chukueni na mle mkate huu. Ni mwili wangu.”
23 Kisha akakichukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu kwa hicho, akawapa. Wote wakanywa toka kile kikombe. 24 Kisha akasema, “Kinywaji hiki ni damu yangu ambayo kwayo Mungu anafanya agano na watu wake. Damu yangu inamwagika kwa manufaa ya watu wengi. 25 Ninawaambia kweli sitakunywa diva tena mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya katika Ufalme wa Mungu.”
© 2017 Bible League International