Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Lev for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Yakobo 1:2-8

Imani na Hekima

Kaka na dada zangu, jueni kuwa mtakutana na adha za kila aina. Lakini hilo liwape ninyi sababu ya kuwa na furaha zaidi. Kwa sababu mnajua kuwa imani yenu inapojaribiwa ndipo mnapojifunza kuwa wavumilivu. Na uvumilivu unapaswa kukamilisha kazi yake, ili kwamba muwe watu waliokomaa na wakamilifu msiopungukiwa na kitu cho chote.

Hivyo kama mmoja wenu atapungukiwa na hekima, anapaswa kumwomba Mungu anayewapa watu wote kwa ukarimu, naye atampa hekima. Lakini anapaswa kuwa na imani anapoomba pasipo mashaka yo yote, kwani yule aliye na mashaka ni kama wimbi la baharini, linalosukumwa na upepo na kusukwa sukwa. Mtu wa jinsi hiyo asidhani kuwa anaweza kupokea cho chote kutoka kwa Bwana; yeye ni mwenye mashaka na hufikiria mambo mawili tofauti kwa wakati mmoja.

Yakobo 1:16-18

16 Kaka zangu na dada zangu wapendwa msikubali kudanganywa, 17 Kila karama njema na kila tuzo kamilifu hutoka juu; hushuka chini kutoka kwa Baba aliyeumba nuru zote zilizoko mawinguni ambamo kwake yeye hakuna mabadiliko kama vile vivuli vinavyosababishwa na mzunguko wa sayari. 18 Kwa uamuzi wake mwenyewe Mungu alituzaa sisi na kuwa watoto wake kwa njia ya ujumbe wa kweli ili tuwe mazao ya kwanza[a] yenye heshima ya pekee miongoni mwa vyote alivyoviumba.

Luka 12:13-21

Yesu Aaonya Kuhusu Ubinafsi

13 Mmoja wa watu katika kundi akamwambia Yesu, “Mwalimu, baba yetu amefariki hivi karibuni na ametuachia vitu, mwambie kaka yangu anigawie baadhi ya vitu hivyo!”

14 Lakini Yesu akamwambia, “Nani amesema mimi ni mwamuzi wa kuwaamulia namna ya ninyi wawili kugawana vitu vya baba yenu?” 15 Ndipo Yesu akawaambia, “Iweni waangalifu na jilindeni dhidi ya kila aina ya ulafi. Maana uhai wa watu hautokani na vitu vingi wanavyomiliki.”

16 Kisha Yesu akawaambia mfano huu: “Alikuwepo tajiri mmoja aliyekuwa na shamba. Shamba lake lilizaa mazao sana. 17 Akasema moyoni mwake, ‘Nitafanya nini? Sina mahali pa kuyaweka mazao yangu yote?’

18 Kisha akasema, ‘Ninajua nitakachofanya. Nitabomoa ghala zangu na kujenga ghala kubwa zaidi! Nitahifadhi nafaka zangu zote na vitu vingine vizuri katika ghala zangu mpya. 19 Kisha nitajisemea mwenyewe, nina vitu vingi vizuri nilivyotunza kwa ajili ya kutumia kwa miaka mingi ijayo. Pumzika, kula, kunywa na furahia maisha!’

20 Lakini Mungu akamwambia yule mtu, ‘Ewe mpumbavu! Leo usiku utakufa. Sasa vipi kuhusu vitu ulivyojiandalia? Nani atavichukua vitu hivyo?’

21 Hivi ndivyo itakavyokuwa kwa mtu anayeweka vitu kwa ajili yake yeye peke yake. Mtu wa namna hiyo si tajiri kwa Mungu.”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International