Book of Common Prayer
Mambo mengine zaidi juu ya Wazee na mengineyo
17 Wazee wanaoliongoza Kanisa katika njia nzuri wanapaswa kupokea heshima mara mbili;[a] hasa wale wanaofanya kazi ya kuhubiri na kufundisha. 18 Kama Maandiko yanavyosema, “Mnyama wa kazi akitumika kutenganisha ngano, usimzuie kula nafaka.”(A) Na Maandiko pia yanasema, “Mfanyakazi anatakiwa kupewa ujira wake.”(B)
19 Usimsikilize yeyote anayemshitaki mzee. Unatakiwa kuwasikiliza tu kama wapo wawili au watatu ambao wanaweza kusema alichokosea mzee. 20 Waambie wazee wanaotenda dhambi kwamba wana hatia, ufanye hivi mbele ya kanisa lote ili wengine wapate kuonywa.
21 Mbele ya Mungu na Kristo Yesu na malaika walioteuliwa, nakuambia fanya hukumu hizo bila upendeleo. Mtendee kila mtu sawa sawa.
22 Fikiri kwa makini kabla ya kuweka mikono yako juu ya yeyote kumfanya mzee. Usishiriki dhambi za wengine, na ujitunze uwe safi.
23 Timotheo, acha kunywa maji tu, kunywa na kiasi kidogo cha mvinyo. Hii itakusaidia tumbo lako, na hutaugua mara kwa mara.
24 Dhambi za watu wengine ni rahisi kuziona, hizo zinaonesha kwamba watahukumiwa. Lakini dhambi za wengine zitajulikana tu hapo baadaye. 25 Inafanana na mambo mazuri wanayofanya watu. Zingine ni rahisi kuonekana. Lakini hata kama si dhahiri sasa, hakuna hata moja itakayojificha milele.
Simulizi Nyingine ya Ufalme
(Mk 4:30-34; Lk 13:18-21)
31 Kisha Yesu akawaambia watu simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na mbegu ya mharadali ambayo mtu alipanda katika shamba lake. 32 Ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote. Lakini unapokua, ni kubwa kuliko mimea yote ya bustanini. Unakuwa mti mkubwa unaotosha ndege kuja na kutengeneza viota kwenye matawi yake.”
33 Kisha Yesu akawaambia simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na chachu ambayo mwanamke huichanganya katika bakuli kubwa la unga ili atengeneze mkate. Chachu hufanya kinyunya chote kiumuke.”
34 Yesu alitumia simulizi akasema mambo yote haya kwa watu. Daima alitumia simulizi kuwafundisha. 35 Hii ilikuwa kuweka wazi maana halisi kama manabii walivyosema:
“Nitazungumza kwa kutumia simulizi;
Nitayasema mambo ambayo yamekuwa siri
tangu ulimwengu ulipoumbwa.”(A)
© 2017 Bible League International