Book of Common Prayer
Maagizo ya Mwisho na Salamu
12 Tunawaomba mwatambue wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao, kama wafuasi wa Bwana, wanatumika kama viongozi wenu na kuwafundisha namna ya kuishi. 13 Wapeni heshima ya hali ya juu na upendo kwa sababu ya kazi wanayofanya.
Ishini kwa amani kila mmoja na mwenzake. 14 Tunawasihi, kuwaonya wale wanaokataa kuishi kwa kuwajibika.[a] Watieni moyo wanaoogopa. Wasaidieni walio dhaifu. Mvumilieni kila mmoja. 15 Asiwepo anae jaribu kulipiza baya kwa baya. Lakini kila mara mfanye lililo jema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.
16 Mwe na furaha daima. 17 Msiache kuomba. 18 Shukuruni kwa kila jambo. Hivi ndivyo Mungu anavyotutaka tuishi katika Kristo Yesu.
19 Msiizimishe kazi ya Roho Mtakatifu. 20 Msiuchukulie unabii kama kitu kisicho cha muhimu. 21 Lakini pimeni kila kitu. Lishikeni lililo jema, 22 na mkae mbali na kila aina ya ovu.
23 Tunaomba kwamba Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, atawafanya muwe watakatifu mkiwa wake. Tunaomba kwamba katika roho yote, nafsi yote, na mwili mzima mtahifadhiwa salama pasipo lawama Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja. 24 Yeye awaitae atawatendea haya. Mnaweza kumtumainia.
25 Kaka na dada zangu, tafadhali mtuombee. 26 Wasalimuni ndugu wote kwa salamu maalum ya watu wa Mungu.[b] 27 Ninawaagiza kwa mamlaka ya Bwana kuusoma walaka huu kwa waamini wote huko. 28 Neema ya Bwana wetu Yesu kristo iwe nanyi nyote.
Huwezi Kuwatumikia Mabwana Wawili
(Lk 12:33-34; 11:34-36; 16:13)
19 Msijiwekee hazina hapa duniani, mahali nondo na kutu[a] huiharibu. Na wezi wanaweza kuvunja nyumba yako na kuziiba. 20 Badala yake jiwekeeni hazina mbinguni ambako haziwezi kuharibiwa na nondo wala kutu na ambako wezi hawawezi kuvunja na kuziiba. 21 Kwa kuwa roho yako itakuwa mahali ilipo hazina yako.
22 Jinsi unavyowaangalia watu wengine ndivyo inavyoonyesha jinsi wewe mwenyewe ulivyo ndani yako. Ukiwaangalia watu kwa nia njema utajawa na nuru ndani yako. 23 Lakini ukiwaangalia watu kwa nia mbaya, utajawa na giza ndani yako. Na ikiwa yote yanayoonekana ndani yako ni giza peke yake, basi unalo giza baya zaidi![b]
24 Hamwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Mtamchukia mmoja na kumpenda yule mwingine au mtakuwa waaminifu kwa mmoja na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na pesa.[c]
© 2017 Bible League International