Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Gen for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
1 Yohana 3:1-10

Tu Watoto wa Mungu

Baba ametupenda sisi sana! Hili linaonesha jinsi anavyotupenda: Tunaitwa watoto wa Mungu. Ni kweli kuwa tu watoto wa Mungu. Lakini watu waliomo duniani hawaelewi ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, kwa sababu hawamjui yeye. Wapendwa, sasa tu watoto wa Mungu. Mungu hajatuonyesha bado namna tutakavyokuwa wakati unaoukuja. Lakini tunajua ya kwamba Kristo atakapokuja tena, tutafanana naye. Tutamwona kama alivyo. Ni mtakatifu, na kila aliye na matumaini haya katika yeye huendelea kuwa mtakatifu.

Kila atendaye dhambi huivunja sheria ya Mungu. Ndiyo, kutenda dhambi ni sawa na kuishi kinyume na sheria ya Mungu. Mwajua ya kuwa Kristo alikuja kuziondoa dhambi za watu. Haimo dhambi ndani ya Kristo. Hivyo kila anayeishi katika Kristo haendelei kutenda dhambi. Kama wakiendelea kutenda dhambi, kwa hakika hawajamwelewa Kristo na hawajamjua kamwe.

Watoto wapendwa, msimruhusu mtu yeyote kuwadanganya. Kristo daima alitenda yaliyo haki. Hivyo kuwa mwema kama Kristo, ni lazima utende yaliyo haki. Mwovu amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kila anayeendelea kutenda dhambi ni mali ya Mwovu. Mwana wa Mungu alikuja kwa ajili ya hili: Kuziharibu kazi za Mwovu.

Wale ambao ni watoto wa Mungu hawaendelei kutenda dhambi, kwa sababu wanayo maisha mapya waliyopewa na Mungu.[a] Hawaendelei kutenda dhambi, kwa sababu wamefanyika watoto wa Mungu. 10 Hivyo tunaweza kuwatambua walio watoto wa Mungu na walio watoto wa Mwovu. Hawa ndiyo wasio watoto wa Mungu: Wale wanaotenda mambo yasiyo haki na wale wasiowapenda ndugu zao wa kike na wa kiume katika familia ya Mungu.

Yohana 10:31-42

31 Kwa mara nyingine Wayahudi pale wakaokota mawe ili wamuue Yesu. 32 Lakini Yeye akawaambia, “Mambo mengi mliyoyaona nikiyatenda yanatoka kwa Baba. Ni kwa mambo gani miongoni mwa hayo mazuri mnataka kuniua?”

33 Wakajibu, “Hatukuui kwa ajili ya jambo lo lote zuri ulilofanya. Lakini wewe unasema mambo yanayomkufuru Mungu! Wewe ni mtu tu, lakini unasema uko sawa na Mungu! Ndiyo sababu tunataka kukuua!”

34 Yesu akajibu, “Imeandikwa katika sheria yenu kuwa Mungu alisema, ‘Nilisema ninyi ni miungu.’(A) 35 Maandiko yaliwaita watu hawa miungu; watu waliopokea ujumbe wa Mungu. Na Maandiko siku zote ni ya kweli. 36 Sasa kwa nini mnanilaumu mimi kwa kumkufuru Mungu kwa kusema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu’? 37 Lakini kama sitafanya yale anayoyatenda Baba yangu, basi msiamini ninayosema. 38 Lakini kama nafanya anayofanya Baba, mnapaswa kuyaamini ninayoyafanya. Mnaweza msiniamini mimi, lakini muamini yale ninayotenda. Ndipo mtakapofahamu na kuelewa kwamba Baba yumo ndani yangu nami nimo ndani ya Baba.”

39 Walijaribu kumkamata Yesu tena, lakini yeye akawatoroka.

40 Kisha akarejea tena kwa kuvuka Mto Yordani hadi sehemu ambapo Yohana alipoanzia kazi ya kubatizia watu. Yesu akakaa huko, 41 na watu wengi wakaja kwake. Wakasema, “Yohana hakutenda ishara na miujiza yoyote, lakini kila alichosema kuhusu mtu huyu ni kweli!” 42 Na watu wengi huko wakamwamini Yesu.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International