Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Josh for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Josh for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Warumi 12:9-21

Upendo wenu unapaswa kuwa halisi. Uchukieni uovu. Fanyeni yaliyo mema tu. 10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kama wa familia moja. Na jitahidini kuwa wa kwanza katika kumpa heshima kila mmoja baina yenu. 11 Mnapoendelea kumtumikia Bwana, fanyeni kwa juhudi wala msiwe wavivu. Mchangamke juu ya utumishi wenu kwa Mungu.[a] 12 Mfurahi kwa sababu ya tumaini mlilonalo. Mvumilieni mnapokutana na mateso. Ombeni nyakati zote. 13 Washirikishe ulichonacho watu wa Mungu wanaohitaji msaada. Wakaribisheni katika nyumba zenu wale wanaosafiri au wanaohitaji msaada.

14 Watakieni mema wale wanaowafanyia mabaya. Mwombeni Mungu awabariki, na sio kuwalaani. 15 Furahini pamoja na wanaofurahi. Huzunikeni na wanaohuzunika. 16 Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, lakini iweni radhi kuwa rafiki wa wasio na umuhimu kwa wengine. Msijihesabu kuwa wenye akili kuliko wengine wote.

17 Mtu akikukosea, usimlipize ubaya. Mjaribu kufanya lile ambalo kila mtu anaona kuwa ni sahihi. 18 Mjitahidi kadri mwezavyo kuishi kwa amani na kila mtu. 19 Rafiki zangu, msijaribu kumwadhibu yeyote anayewakosea. Msubiri Mungu katika hasira yake awaadhibu. Katika Maandiko Bwana anasema, “Nitawaadhibu wao kwa ajili ya yale waliyofanya.”(A) 20 Badala yake,

“ikiwa una adui wenye njaa,
    wapeni chakula wale.
Ikiwa wana kiu,
    wapeni kinywaji wanywe.
Kwa kufanya hivyo mtawafanya wajisikie aibu.”[b](B)

21 Msiruhusu uovu uwashinde, bali ushindeni uovu kwa kutenda mema.

Mathayo 26:17-25

Karamu ya Pasaka

(Mk 14:12-21; Lk 22:7-14,21-23; Yh 13:21-30)

17 Ilipofika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, wafuasi wake walimjia Yesu na kumwambia, “Tutaandaa kila kitu kwa ajili yako ili ule mlo wa Pasaka. Unataka tuandae wapi mlo wa Pasaka?”

18 Yesu akajibu, “Nendeni mjini kwa mtu ninayemfahamu. Mwambieni kuwa Mwalimu anasema, ‘Muda uliowekwa kwa ajili yangu umekaribia sana. Mimi na wafuasi wangu tutakula mlo wa Pasaka katika nyumba yako.’” 19 Walitii na kufanya kama Yesu alivyowaambia. Waliandaa mlo wa Pasaka.

20 Jioni ilipowadia, Yesu alikuwa ameketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 21 Walipokuwa wakila Yesu akasema, “Niaminini, ninapowaambia kuwa mmoja wenu ninyi kumi na wawili atanikabidhi kwa maadui zangu.”

22 Wanafunzi walisikitika sana waliposikia hili. Kila mmoja akasema, “Bwana, hakika si mimi!”

23 Yesu akajibu, “Yeye aliyechovya mkate wake katika kikombe kile kile nilichochovya mimi ndiye atakayenisaliti. 24 Mwana wa Adamu atakiendea kifo chake kama Maandiko yanavyosema. Lakini ole wake mtu yule anayemsaliti Mwana wa Adamu ili auawe. Ni bora mtu huyo asingezaliwa.”

25 Ndipo Yuda, ambaye ndiye angemsaliti, akamwambia Yesu, “Mwalimu, hakika si mimi unayemzungumzia, ama ndiye?”

Yesu akamjibu, “hicho ndicho unachosema.”

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International