Book of Common Prayer
1 Salamu toka kwa Paulo, Sila, na Timotheo.
Kwa kanisa lililoko Thesalonike lililo milki ya Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.
Neema na amani ziwe zenu.
Maisha na Imani ya Wathesalonike
2 Kila mara tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu nyote na kuwataja katika maombi yetu. 3 Kila tunapomwomba Mungu baba yetu, tunawakumbuka kwa yote mliyofanya kwa sababu ya imani yenu. Na tunawakumbuka kwa kazi mliyofanya kwa sababu ya upendo wenu. Na tunakumbuka jinsi mlivyo imara kwa sababu ya tumaini lenu katika Bwana wetu Yesu Kristo.
4 Ndugu zetu, Mungu anawapenda. Nasi twajua yakuwa amewachagua muwe watu wake. 5 Tulipowaletea Habari Njema kwenu, tulikuja na yaliyo zaidi ya maneno. Tuliwaletea ile Habari Njema yenye uweza, pamoja na Roho Mtakatifu, na tulikuwa na uhakika kamili hiyo ilikuwa ni Kweli halisi. Pia mnafahamu tulivyo enenda tulipo kuwa pamoja nanyi. Tuliishi hivyo ili kuwasaidia ninyi. 6 Nanyi mkauiga mfano wetu na mfano wa Bwana. Mliteseka sana, lakini bado mliyakubali mafundisho na furaha inayotokana na Roho Mtakatifu.
7 Mlifanyika mfano wa kuigwa na waaminio wote wa Makedonia na Akaya. 8 Mafundisho ya Bwana yameenea toka Makedonia mpaka Akaya na nje ya mipaka yake. Kwa kweli, imani yenu katika Mungu imejulikana kila mahali, hivyo hatuna haja ya kumwambia mtu yeyote kwa habari hii. 9 Watu kila mahali wanasimulia habari ya namna mlivyotupokea vizuri tulipo kuwa pamoja nanyi. Wanasimulia namna mlivyoacha kuiabudu miungu ya uongo na kubadilika na kuanza kumwabudu Mungu aliye hai na wa kweli. 10 Na mkaanza kumngoja mwana wa Mungu aje kutoka mbinguni, Mwana ambaye Baba alimfufua kutoka kwa wafu. Yeye ni Yesu, anayetuokoa kutoka katika hukumu yenye hasira ya Mungu inayokuja.
Viongozi Wawa na Mashaka Kuhusu Mamlaka ya Yesu
(Mt 21:23-27; Mk 11:27-33)
20 Siku moja Yesu alikuwa anawafundisha watu katika eneo la Hekalu. Alikuwa anawahubiri Habari njema. Viongozi wa makuhani, walimu wa sheria, na viongozi wazee wa Kiyahudi walikwenda kuzungumza na Yesu. 2 Wakamwambia, “Tuambie, una mamlaka gani kutenda mambo haya! Ni nani aliyekupa mamlaka hii?”
3 Yesu akawajibu, “Nami nitawauliza swali pia. Niambieni: 4 Yohana alipobatiza watu, mamlaka yake ilitoka kwa Mungu au kwa watu fulani?”
5 Makuhani, walimu wa sheria na viongozi wa Kiyahudi wakajadiliana kwa pamoja kuhusu hili. Wakasema, “Kama tukijibu ‘Ubatizo wa Yohana ulitoka kwa Mungu,’ atasema, ‘Sasa kwa nini hamkumwamini Yohana?’ 6 Lakini kama tukisema ulitoka kwa watu fulani, watu hawa watatupiga kwa mawe mpaka tufe. Kwa sababu wote wanaamini Yohana alikuwa nabii.” 7 Hivyo wakajibu, “Hatujui.”
8 Ndipo Yesu akawaambia, “Hata mimi sitawaambia ni nani alinipa mamlaka kufanya mambo haya.”
© 2017 Bible League International