Print Page Options
Previous Prev Day Next DayNext

Book of Common Prayer

Daily Old and New Testament readings based on the Book of Common Prayer.
Duration: 861 days
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)
Version
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Ps for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Error: Book name not found: Zech for the version: Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi

1 Timotheo 6:12-16

12 Tunatakiwa tupigane kutunza imani yetu. Jaribu kwa bidii kadri unavyoweza kushinda vita vya thawabu. Tunza uzima wa milele. Ni uzima mliyouchagua kuupata mlipoikiri imani yenu katika Yesu; huo ukweli wa ajabu mliousema waziwazi kwa wote kuusikia. 13 Mbele ya Mungu na Kristo Yesu nakupa amri. Yesu ni yule aliyeshuhudia ukweli aliposimama mbele ya Pontio Pilato. Mungu ndiye anayetoa uhai kwa kila kitu. Nakuambia haya sasa: 14 Tenda niliyokuamuru kufanya bila dosari au kulaumu mpaka muda atakapo rudi. 15 Mungu atafanya hayo yatokee wakati utakapotimia. Yeye ni mwenye utukufu zaidi na mtawala pekee, mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana. 16 Mungu pekee hafi, anaishi katika nuru angavu sana ambayo watu hawawezi kusogea karibu. Hakuna mtu aliyemwona Mungu; wala anayeweza kumuona. Heshima na nguvu ni zake milele. Amina.

Mathayo 21:12-17

Yesu Asafisha Eneo la Hekalu

(Mk 11:15-19; Lk 19:45-48; Yh 2:13-22)

12 Yesu alipoingia katika eneo la Hekalu, aliwatoa nje wote waliokuwa wanauza na kununua vitu humo. Alizipindua meza za watu waliokuwa wanabadilishana pesa. Na alipindua viti vya watu waliokuwa wanauza njiwa. 13 Yesu aliwaambia, “Maandiko yanasema, ‘Hekalu langu litaitwa nyumba ya sala.’(A) Lakini mmelibadilisha na kuwa ‘maficho ya wezi’.(B)

14 Baadhi ya watu waliokuwa wasiyeona na walemavu wa miguu walimjia Yesu alipokuwa eneo la Hekalu, naye aliwaponya. 15 Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria waliona mambo ya ajabu aliyokuwa anatenda. Na waliona watoto walivyokuwa wanamsifu wakisema, “Sifa kwa Mwana wa Daudi.” Mambo haya yote yaliwakasirisha makuhani na walimu wa sheria.

16 Wakamwuliza Yesu, “Unasikia wanayosema watoto hawa?”

Akajibu, “Ndiyo. Maandiko yanasema,

‘Umewafundisha watoto wadogo na watoto
    wanyonyao kusifu.’(C)

Hamjasoma Maandiko haya?”

17 Kisha Yesu akawaacha na akaenda katika mji wa Bethania akalala huko.

Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi (TKU)

© 2017 Bible League International