Revised Common Lectionary (Semicontinuous)
10 Yesu Kristo alifanya mambo ambayo Mungu alimtaka ayafanye. Na kwa sababu ya hilo, tunatakaswa kwa njia ya sadaka ya mwili wa Kristo. Kristo aliitoa sadaka hiyo mara moja, inayotosha kwa nyakati zote.
11 Kila siku makuhani husimama na kutekeleza shughuli zao za kidini. Tena na tena hutoa sadaka zilezile, ambazo kamwe haziwezi kuondoa dhambi. 12 Lakini Kristo alitoa sadaka moja tu kwa ajili ya dhambi, na sadaka hiyo ni nzuri kwa nyakati zote. Kisha akakaa mkono wa kuume wa Mungu. 13 Na sasa Kristo anawasubiria hapo adui zake wawekwe chini ya mamlaka yake.[a] 14 Kwa sadaka moja Kristo akawakamilisha watu wake milele. Ndio wale wanaotakaswa.
15 Roho Mtakatifu pia anatuambia juu ya hili. Kwanza anasema:
16 “Hili ndilo agano[b] nitakaloweka
na watu wangu baadaye, asema Bwana.
Nitaziweka sheria zangu ndani ya mioyo yao.
Nitaziandika sheria zangu katika fahamu zao.”(A)
17 Kisha anasema,
“Nitazisahau dhambi zao
na nisikumbuke kamwe uovu walioutenda.”(B)
18 Na baada ya kila kitu kusamehewa, hakuna tena haja ya sadaka ili kuziondoa dhambi.
© 2017 Bible League International